Elections 2010 Utabiri wa Shekhe Yahya wakwama

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
1,000
Utabiri wa Shekhe Yahya wakwama.


Na Mwandishi Wetu

LICHA ya utabiri wa Mnajimu maarufu nchini, Shekhe Yahya Hussein kubainisha kuwa mwaka huu kusingekuwa na Uchaguzi Mkuu, hali imekuwa tofauti na
uchaguzi huo ukafanyika nchini kote jana, isipokuwa katika majimbo saba, ambako uliahirishwa kutokana na kasoro za karatasi za kura.

Ukiondoa majimbo hayo saba ya Wete, Mwanakwerekwe, Mtoni, Magogoni, Mpanda Vijijini, Mpanda Mjini na Nkenge, maeneo mengine uchaguzi ulifanyika kama ilivyopangwa.

Vyanzo vya habari vilivyozungumza na Majira vilisema kuwa kufanyika kwa uchaguzi huo ni ishara tosha kuwa utabiri huo wa Shekhe Yahya haukuwa kweli.

Februari 4, mwaka huu, gazeti hili lilimkariri Shekhe Yahya Hussein akitabiri kuwa hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka huu nchini.

Habari hiyo ilitokana na mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Channel Ten katika kipindi cha masaula ya nyota, ambako alionekana akisisitiza utabiri huo mara kwa mara.

Huku akionekana kufafanua utabiri huo, Shekhe Yahya alisema, "nasema hakuna uchaguzi mwaka huu, uchaguzi utaahirishwa, siwezi kusema sana, maana karibuni nilitoa utabiri
kuwa kuna mtu anaweza kufa katika kugombea urais, watu wamesema sana," alisema.

Juhudi za gazeti hili kumpata mnajimu huyo kuzungumzia utabiri wake hazikuzaa matunda, kwa kuwa simu yake ilikuwa ikiita muda wote bila majibu.

Tangu mwishoni mwa mwaka jana Shekhe Yahya alikuwa katikati ya mijadala ya kisiasa nchini, hasa ile inayohusiana na uchaguzi baada ya kutoa utabiri uliopingwa vikali, kuwa mwanachama yeyote ndani ya CCM ambaye angesimama kumpinga Rais Jakaya Kikwete katika nafasi ya urais angekufa ghafla.

Hata hivyo, hakuna mwanachama wa CCM aliyejitokeza kumpinga rais huyo hadi akatangazwa mgombea pekee, baada ya aliyekuwa amesema angempinga, Bw. John Shibuda kuamua kuachia ngazi hata kabla ya kuchukua fomu.

source:
majiri
 
Serikali ya JK ilikuwa ikiongozwa na wanajimu na waganga wa Jadi..sasa kwishnei..Wapi REDET na vibaraka wake? AIBU KUBWA KWA WAZANDIKI HAWA!!
 
Hatuwezi kusikliza maneno ya mwehu na kuyaweka vichwani mwetu. Jibu zuri kwa mjinga ni kumnyamazia....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom