Utabiri wa Sheikh Yahya mbioni kufanyiwa kazi ndani ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utabiri wa Sheikh Yahya mbioni kufanyiwa kazi ndani ya Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RMA, Mar 9, 2011.

 1. R

  RMA JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais anataka kutimiza utabiri wa kishirikina wa mlinzi wake wa majini, Sheikh Yahya? Anatafuta kukutana na Chadema. Bila kupambana na ufisadi kwanza huko si kutapatapa? Hiyo ni danganya toto kwa vile ameona maji yako shingoni kwani hapo tulipofikia, hata taahira anahisi kuwa upepo sio mzuri! Kuna kila dalili kwamba moto waweza kulipuka wakati wowote.

  Hata Sheikh Yahya anajua hivyo, kwamba pamoja na ushirikina, sasa watanzania wako standby, na wako tayari kwa lolote. Harakati za kutaka kukutana na Chadema tu, bila kujibu kwanza tuhuma za Chadema kuhusu ufisadi na umaskini wa watanzania, ni ufukunyuku! Na mikakati yenyewe haina tija kwa vile ni mikakati ya kishirikina!
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Badilisha heading mkuu.
   
 3. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Utabiri upi wa sheikh yahya? Au umeuficha na unaujua we mwenyewe? Naungana na birigita badili hiyo title other wise unajaribu kudanganya watu
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kichwa cha habari > content?= 0
   
 5. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  RMA una bore usikurupuke kuandika vitu na ukisha andika kipitie kuhariri unacholisha uma..!!! Were Great Thinkers bana
   
 6. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Title imaweza kusomeka hivi "CCM isikutane na Chadema, ijibu hoja na kutekeleza madai yao" Chama cha demokrasia na maendeleo CDM haKina mgogoro na CCM bali kina mgogoro na hali ngumu ya maisha kwa ujumla. Kwa maana hivo basi suluhisho linalotakiwa sio ccm kukutana na chadema bali ni serikali ya ccm kujibu hoja za chadema ili kuwapunguzia ukali wa maisha unaowakabili. Mapendezo yanayotolewa kutaka rais kikwete akutane na chadema hayana tija kwa kuwa hata wakikutana bila kutekelezeka kwa hoja zinazozungumzwa na chadema bado itakuwa ni kazi bure. Chadema hawana ugonvi binafsi na ccm. Naishauri serikali ya ccm iyafanyie kazi madai ya chadema na kama kuna haja ya ccm kukutana na chadema basi wakutane kuzungumza namna ya kuumaliza mgogoro wa Arusha uliotokana na uchaguzi wa umeya ambao bado unaendelea kufukuta.
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hicho kichwa cha habari umeandika maksudi kuvuta attention ya wadau ?
   
Loading...