Utabiri Wa Saadani Kandoro Umetimia ndani ya miaka 50 ya uhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utabiri Wa Saadani Kandoro Umetimia ndani ya miaka 50 ya uhuru?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njaare, Aug 11, 2011.

 1. N

  Njaare JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wana JF,

  Kwa wale wapenzi wa Mashairi wanaweza wakamkumbuka Marehemu Saadan Kandoro na kitabu chake cha Mashairi ya Saadani. Katika kitabu hicho kuna shairi moja lenye kichwa cha kisemacho, "siafu wamekazana". Shairi hili lilitungwa kabla ya uhuru kuelezea jinsi waafrika (siafu) walivyokazana kumwondoa mkoloni (nyoka). Ila alionya kuwa mkoloni akiondoka, waafrika wataanza kuoneana kwa kusema, "Kupo na kukanyagana, nyoka akishaondoka".
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo unamaanisha kuwa Jk na nani wanakanyagana?
   
 3. w

  woyowoyo Senior Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tukuite andanenga?
   
 4. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha mbali sana, pia kulikuwa na lile la "kwa nini na kwa nini?"

  CCM imepoteza dira na mwelekeo hata kiongozi anashangaa kwa nini nchi ni masikini.
   
 5. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mimi naona siafu sasa wanakula siafu wenzao na kuhakikisha nyoka wanaishi kwa amani.
   
 6. MANI

  MANI Platinum Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Umenena Mamengazi hongea !
   
 7. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwao kwetu kwa nini? Kwetu kwao kwa nini? S.A. Kandoro
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Linaitwa kwetu ni kwao kwanini?


  Ngoja nikupe ubeti mmoja ninaoweza kuukumbuka haraka haraka.

  Mtu uuliza nini, kitu hichi ni cha nani,
  Kitu hichi ni cha nani, na hichi kitu cha nani,
  nacho kinaitwa nini, ni cha nani na kwanini.
  Kwetu ni kwao kwanini. na kwao si kwetu kwanini.


  Huyu aliitwa Saadan Abdul kandoro (jina la ushairi ni staharaki)
   
 9. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kumbe wapo watu walikuwa na vision kuhusu tz muda mrefu tu!ccm ni nini,na hiki ni chanani?
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kasome kitabu cha Animal Farm. Haya ni mambo yanayotokea pale uhuru unapopewa nchi zisizokuwa tayari kuupata!!
   
 11. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwenye red ilikuwa ni ''KWA NINI KWETU KWAO?''
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2013
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Nimekukubali.
  Nilipenda sana mashairi ya huyu mzee. Je huyu Mzee Kandoro wana uhusiano gani na huyu Mkuu wa mkoa wa Mbeya bwana Abas Kandoro?
   
 13. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2013
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,634
  Likes Received: 2,063
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu maana siku hizi hakuna wanafalsafa kwani kila utakachokifiria utakuta tayari kuna mtu alishakitoa miaka 40 iliyopita pia kutokana na kisa hiki nimetambua kwanini tunajifunza HISTORY, kumbe ili kujifunza mistake walizofanya babu zetu ili zisitokee kwa kizazi hiki cha sasa maana matukio haya Chifu Mangungu wa Usagara enzi hizo na mikataba feki kwa uongozi wa hivi karibuni ni visa vinavyofanana though vimetokea nyakati tofauti.
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2013
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Cha msingi sasa ni kujisahihisha pale mlipokosea na kusonga mbele.
   
 15. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2013
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kile kitabu cha George Orwell kimesema yote.
  Napoleon na Nguruwe wengne wanapoamua kuwatawala wanyama wenzao kwa mkono wa chuma kwa faida yao, wakitumia jeshi la mbwa.
  Kisha wanamkaribisha mwanadam mkoloni na jina la shamba linarudi kuwa Manor farm!
  Aliona mbali sana.
   
 16. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2013
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  wale nguruwe Mwerevu? na Mbishi? walikuwa kiboko....

  unamkumbuka yule farasi aliyefanya kazi kwa bidii akiahidiwa nchi ya asali na maziwa alipotenguka kiuno jamaa wakaenda kumpatanisha kwa nchinjaji akaenda kulamba kisu?

  unakumuka jinsi nguruwe wakaendelea kutandika mayai ya kuku wakati wakiwwahidi kuku kuwa wataawaachia mayai yao waongezeke?

  unakumbuka wale kunguru walikuwa wanapewa kazi ya kupiga talalia kuwa kuna nchi za mbali walkiruka wanaziona zimejaa maziwa na asali?

  kweli yule jamaa alikuwa kiboko!
   
 17. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2013
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  wale nguruwe Mwerevu? na Mbishi? walikuwa kiboko....

  unamkumbuka yule farasi aliyefanya kazi kwa bidii akiahidiwa nchi ya asali na maziwa alipotenguka kiuno jamaa wakaenda kumpatanisha kwa nchinjaji akaenda kulamba kisu?

  unakumuka jinsi nguruwe wakaendelea kutandika mayai ya kuku wakati wakiwwahidi kuku kuwa wataawaachia mayai yao waongezeke?

  unakumbuka wale kunguru walikuwa wanapewa kazi ya kupiga talalia kuwa kuna nchi za mbali walkiruka wanaziona zimejaa maziwa na asali?

  unakumbuka jinsi nguruwe walivyokuwa wanajigonga udrinko na matafrija kwa kuendelea kuwauza wenzao?

  kweli yule jamaa alikuwa kiboko!
   
Loading...