Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,319
- 17,474
Mwl. Nyerere alikuwa na maono ya kipekee sana. Mambo mengi aliyoyaongea miaka mingi iliyopita yametokea na mengine yanaendelea kutokea. Moja ya jambo alilolisema na kutokea ni hili lililosimuliwa na Prof. Kabudi wakati wa mdahalo wa katiba 4 Aug 2014. Na haya ndiyo aliyosema Prof.Kabudi;
Nimekumbua maneno haya baada ya kusikia yaliyotokea zimbabwe, kama vile yalivyotokea Libya, Egypt, Yemen, Syria, Bahrain na Ivory coast miaka ya nyuma.
Je ni mambo gani mengine mwalimu alitabiri nakuja kutokea?
.Na ndiyo yanayonifanya nimalize kwa kuyakumbuka maneno ya mwalimu mwaka 1993 nikiwa Berlin mwanafunzi, amekuja kumzika Willy Brandt, Willy Brandt! Tumekusanyika... alikaa... yeye na Kaunda walikaa... marafiki wakubwa wa Willy Brandt. Tukaa.. dada mmoja sitamtaja jina leo, akamuuliza, "mwalimu huko nyumbani mmeruhusuje vyama vyingi, wakati walio taka ni wachache?" Mwalimu akamtazama akacheka... akasema, "binti! We si unaishi hapa Berlin si umemuona Ceaușescu, wametungua Helicopter eh, ikadondoka eh, wakamuua yeye na mke wake... wakavuta maiti, ni kwasababu Ceaușescu alisubiri wanaomkataa wawe wengi, wakamtungua!"