Utabiri wa Mwl. Nyerere na Prof. Kabudi

Nataka nijue kama Mwl Nyerere alikwisha wahi kutabiri hii ania ya Demokrasia iliyo buniwa juzi usiku hapo Zimbambwe?

Zipi ni sifa za hao criminals wanao mzunguka Mugabe ambao jeshi la huko linawasaka kwa udi na uvumba?
 
Mwl. Nyerere alikuwa na maono ya kipekee sana. Mambo mengi aliyoyaongea miaka mingi iliyopita yametokea na mengine yanaendelea kutokea. Moja ya jambo alilolisema na kutokea ni hili lililosimuliwa na Prof. Kabudi wakati wa mdahalo wa katiba 4 Aug 2014. Na haya ndiyo aliyosema Prof.Kabudi;

.


Nimekumbua maneno haya baada ya kusikia yaliyotokea zimbabwe, kama vile yalivyotokea Libya, Egypt, Yemen, Syria, Bahrain na Ivory coast miaka ya nyuma.

Je ni mambo gani mengine mwalimu alitabiri nakuja kutokea?

Umejitahidi kunukuu lakini si kila alichosema Nyerere ni lazima kitokee, na si lazima kiwe sahihi. Mfano habari ya Libya imetokea hivi karibuni Mwalimu alishafariki siku nyingi na wewe umeiweka kama nukuu. Hii ni aibu kwako wewe. Ghadaffi hakusubili wamchukie watu wske, Ghadaffi ni hiyana ya Marekani na Waingereza, watu walimpenda sana, Tanzania ni 20% kwa 80%, hiyo inajulikana. Je Libya ni asilimia ngapi? Na nchi ulizozitaja ni % ngapi? Au wewe umekariri tu kila likisemwa na Prof. Basi kwako ni sahihi? Tafadhali ukisoma au kusikia jambo kabla ya kulitoa hewani ongeza na zakwako. Ni aibu sana vijana kuwa na mawazo tegemezi. Huenda baada ya kusoma mawazo haya utaishia kutukana badala ya kujenga hoja kwa haya niloyoyatilia shaka. Au huenda utakodi watukanaji ambao akili zao zilishafyatuka siku nyingi.
 
Njaa! Ni tatizo kubwa kwa wasomi wengi wa Tanzania. Hawa kina Polepole na Prof Kabudi ukiwasikiliza sasa hivi huwezi amini kabisa ni wao.
 
Wasomi wa Tz ni sheeedah! kuna yule le-prof. aliyesema 'raisi asiteue mafrofesa kutoka vyuo vikuu kwani atadumaza elimu' alipoteuliwa tu kesho yake alionekana mwenge akinunua suti ya kuapishwa.
 
Mwalimu alikuwa anasoma, anatafuta habari, anajifunza, hakuacha ku analyse mambo

alikuwa mwingi wa ujuvi, hakujifanya anajua bila references

Na yote hayo katika wakati ambao upatikanaji wa taarifa na maandiko mbalimbali haukuwa rahisi kama kipindi chetu.

Kweli kabisa tena kipindi hicho hatukuwa tumetafuniwa kwa urahisi wa kupata habari kama sasa.
 
Kile kichwa kilikua kinajishughulisha sana na issues. Alisoma kila andishi lililopita mbele yake na bila kujali upuuzi aunumakini wa hilo andiko yote aliyatafakari kwa kina sana
Hili ni jambo tunalotakiwa kujifunza sana katika zama hizi.
 
Huyu si ndio waziri wa sasa wa Katiba na sheria?. Mbona matendo yake ya sasa hayaendani na maneno yake ya wakati huo.
Au ndo utapeli uleule tunaofanyiwa na wasomi wetu wanapokuwa na njaa wanapiga kelele sana kuikosoa serikali wakionjeshwa kimya serikali inakuwa malaika
Ni matendo gani hayo ambayo hayaendani na maneno yake?
 
Back
Top Bottom