Utabiri wa JK kupata tuzo ya MO Ibrahim akistaafu

Haya nimemsoma leo toka kwa mwandishi mmoja wa hoja ya mzalendo(MTANZANIA 16.10)
Tunajua vigezo vya tuzo ni rais mstaafu aliyesaidia nchi yake kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa utawala bora, kuheshimu haki za binadamu ustawi wa demokrasia na maendeleo ya uchumi. Mwandishi huyu anaposema Jk ana dalili za kutwaa ushindi wa tuzo hiyo atakapostaafu 2016 sijui anakiamini anachokisema au anadhihaki tu. Anazungumzia Jk kuruhusu uhuru mkubwa kwa watu kuwa na uhuru wa kuisema serikali, kukua kwa upinzani na kuwa na uchaguzi huru na haki. Anasema Haki za binadamu zimepewa nafasi kubwa katika uongozi wa Jk. Amezungumzia mengi ambayo mengi ni kichefuchefu mfano kuwa Jk amekua na ujasiri wa kufikisha viongozi wa nyadhifa kubwa washtakiwae mahakamani kwa ufisadi. Wote tunajua nchi hii ina hali mbaya kila upande nchi ambayo kwa sasa :

· Wanayama pori wanaibiwa mchana kweupe na hakuna maelezo
· Katibu mkuu anachangisha fedha ili kutoa rushwa na bado anapeta
· Watanzania wanauwawa na hakuna anayewajibika
· Mchakato wa kuandaa katiba unavurugwa kwa makusudi na hakuna anayejali
· Mali zetu zinaporwa na mfano nyumba za serikali na hakuna anayewajibika
· Wezi wanatunyanganya rasilimali na wanalindwa na sheria na nchi iko kimya, inatuvizia tukupiga kelele wanabadilika mfano – Malipo ya Dowans
· Matumizi mabaya Madaraka:- Wauaji/na wezi wanasamehewa adahabu za kifo na kupewa kifungo kifupi- kwa JK naye kaja na yake ya kusamehe wezi wa EPA (Ikulu haitoi habari wala ufafanuzi kuhusu usahihi wa hatua husika bali wao watuambia siyo JK ni Mkapa, hawasemi wao wanalionaje hilo?)
· Kigugumizi cha kuwachukulia hatua wezi wa Kagoda
· Mapungufu ya wazi na ya makusudi katika chaguzi
· Sheria zinapitishwa kwa manufaa ya watu wan je na siyo watanzania
· Ufisadi umekuwa ni itikadi ya nchi na hakuna anayewajibika
· Uzalendo na utaifa vimekufa na watu wanahamasisha udini, ukabila na ukanda waziwazi na hakuna kiongozi anayekemea na kwa maana nyingine wanayabariki yote
· Wezi wa EPA wanapewa amnesty kuwa warudishe fedha na hawatashughulikiwa kisheria na pia watanzania hawajulishwi kuhusu hii sheria mpya kwa wezi na ikiwezekana iongezwe katika sheria zetu za makosa ya jinai.

Hivi wewe huoni kuwa badala ya kutoa habari serikali inahangaika kuzuia yasijukane? Hivi utabiri huu unaupata katika njozi au wapi?

Nawasilisha!
Anaweza kupata kama ikiwa lazima mtu apatikane!
He was fair president lakini hakuwa na outstanding performance inayohitaji kutunukiwa tuzo, except if tunazungumzia demokrasia Africa, kwa kweli amefanya makubwa kuliko viongozi wengi kama sio wote kwa wakati akiwa madarakani!
Kama combinations ya qualities, nadhani hata nominations hatokuwepo!
 
Je! Damu ya mchana kweupe nyololo kiijijini?mawazo wa cdm?dr mvungi naye je! Escrow na stanbic nazo je? Kwa hizo 100 percent ka nazo sisi tubaki na tuko yetu
 
Anaweza kupata kama ikiwa lazima mtu apatikane!
He was fair president lakini hakuwa na outstanding performance inayohitaji kutunukiwa tuzo, except if tunazungumzia demokrasia Africa, kwa kweli amefanya makubwa kuliko viongozi wengi kama sio wote kwa wakati akiwa madarakani!
Kama combinations ya qualities, nadhani hata nominations hatokuwepo!
Sio lazima apatikane, miaka kibao imekuwa ikipita bila kupatikana, so akipata atakuwa ame deserve
 
Haya nimemsoma leo toka kwa mwandishi mmoja wa hoja ya mzalendo(MTANZANIA 16.10)
Tunajua vigezo vya tuzo ni rais mstaafu aliyesaidia nchi yake kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa utawala bora, kuheshimu haki za binadamu ustawi wa demokrasia na maendeleo ya uchumi. Mwandishi huyu anaposema Jk ana dalili za kutwaa ushindi wa tuzo hiyo atakapostaafu 2016 sijui anakiamini anachokisema au anadhihaki tu. Anazungumzia Jk kuruhusu uhuru mkubwa kwa watu kuwa na uhuru wa kuisema serikali, kukua kwa upinzani na kuwa na uchaguzi huru na haki. Anasema Haki za binadamu zimepewa nafasi kubwa katika uongozi wa Jk. Amezungumzia mengi ambayo mengi ni kichefuchefu mfano kuwa Jk amekua na ujasiri wa kufikisha viongozi wa nyadhifa kubwa washtakiwae mahakamani kwa ufisadi. Wote tunajua nchi hii ina hali mbaya kila upande nchi ambayo kwa sasa :

· Wanayama pori wanaibiwa mchana kweupe na hakuna maelezo
· Katibu mkuu anachangisha fedha ili kutoa rushwa na bado anapeta
· Watanzania wanauwawa na hakuna anayewajibika
· Mchakato wa kuandaa katiba unavurugwa kwa makusudi na hakuna anayejali
· Mali zetu zinaporwa na mfano nyumba za serikali na hakuna anayewajibika
· Wezi wanatunyanganya rasilimali na wanalindwa na sheria na nchi iko kimya, inatuvizia tukupiga kelele wanabadilika mfano – Malipo ya Dowans
· Matumizi mabaya Madaraka:- Wauaji/na wezi wanasamehewa adahabu za kifo na kupewa kifungo kifupi- kwa JK naye kaja na yake ya kusamehe wezi wa EPA (Ikulu haitoi habari wala ufafanuzi kuhusu usahihi wa hatua husika bali wao watuambia siyo JK ni Mkapa, hawasemi wao wanalionaje hilo?)
· Kigugumizi cha kuwachukulia hatua wezi wa Kagoda
· Mapungufu ya wazi na ya makusudi katika chaguzi
· Sheria zinapitishwa kwa manufaa ya watu wan je na siyo watanzania
· Ufisadi umekuwa ni itikadi ya nchi na hakuna anayewajibika
· Uzalendo na utaifa vimekufa na watu wanahamasisha udini, ukabila na ukanda waziwazi na hakuna kiongozi anayekemea na kwa maana nyingine wanayabariki yote
· Wezi wa EPA wanapewa amnesty kuwa warudishe fedha na hawatashughulikiwa kisheria na pia watanzania hawajulishwi kuhusu hii sheria mpya kwa wezi na ikiwezekana iongezwe katika sheria zetu za makosa ya jinai.

Hivi wewe huoni kuwa badala ya kutoa habari serikali inahangaika kuzuia yasijukane? Hivi utabiri huu unaupata katika njozi au wapi?

Nawasilisha!
Labda huyu muandishi anapima upepo wa hali ya hewa ipo vipi nje ya watawala
 
Tunakuombea Baba. Walikusema sanaaaaa mwishowe wanaaibika. UN wanakukubali ona hivi karibuni unaenda kukamata tuzo nyingine ya kimataifa New York. Asante baba.
 
Fikiria kabla ya kuandika nyie ndio ambao mnaqifanya hii JF kwa sasa ionekane ni sehemu ya watu kubwabwaja na kujiondolea ile sifa yake ya Great Thinkers. Hata hao walio pewa ni binaadamu na kuna makosa walifanya km hayo kwenye nchi zao , sio kwamba walikuwa clean 100% , hakuna binaadamu wa hivyo labda sasa useme wenye kupewa tunzo hiyo ni malaika tutakuelewa.
Makosa yapo lakini mengine ni UZEMBE wa makusudi
 
Ulifanya makubwa baba ikiwemo kujenga UDOM pia kuwezesha wanawake katika uongozi Hongera baba.
 
Back
Top Bottom