Utabiri wa JK kupata tuzo ya MO Ibrahim akistaafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utabiri wa JK kupata tuzo ya MO Ibrahim akistaafu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Oct 16, 2011.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Haya nimemsoma leo toka kwa mwandishi mmoja wa hoja ya mzalendo(MTANZANIA 16.10)
  Tunajua vigezo vya tuzo ni rais mstaafu aliyesaidia nchi yake kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa utawala bora, kuheshimu haki za binadamu ustawi wa demokrasia na maendeleo ya uchumi. Mwandishi huyu anaposema Jk ana dalili za kutwaa ushindi wa tuzo hiyo atakapostaafu 2016 sijui anakiamini anachokisema au anadhihaki tu. Anazungumzia Jk kuruhusu uhuru mkubwa kwa watu kuwa na uhuru wa kuisema serikali, kukua kwa upinzani na kuwa na uchaguzi huru na haki. Anasema Haki za binadamu zimepewa nafasi kubwa katika uongozi wa Jk. Amezungumzia mengi ambayo mengi ni kichefuchefu mfano kuwa Jk amekua na ujasiri wa kufikisha viongozi wa nyadhifa kubwa washtakiwae mahakamani kwa ufisadi. Wote tunajua nchi hii ina hali mbaya kila upande nchi ambayo kwa sasa :

  · Wanayama pori wanaibiwa mchana kweupe na hakuna maelezo
  · Katibu mkuu anachangisha fedha ili kutoa rushwa na bado anapeta
  · Watanzania wanauwawa na hakuna anayewajibika
  · Mchakato wa kuandaa katiba unavurugwa kwa makusudi na hakuna anayejali
  · Mali zetu zinaporwa na mfano nyumba za serikali na hakuna anayewajibika
  · Wezi wanatunyanganya rasilimali na wanalindwa na sheria na nchi iko kimya, inatuvizia tukupiga kelele wanabadilika mfano – Malipo ya Dowans
  · Matumizi mabaya Madaraka:- Wauaji/na wezi wanasamehewa adahabu za kifo na kupewa kifungo kifupi- kwa JK naye kaja na yake ya kusamehe wezi wa EPA (Ikulu haitoi habari wala ufafanuzi kuhusu usahihi wa hatua husika bali wao watuambia siyo JK ni Mkapa, hawasemi wao wanalionaje hilo?)
  · Kigugumizi cha kuwachukulia hatua wezi wa Kagoda
  · Mapungufu ya wazi na ya makusudi katika chaguzi
  · Sheria zinapitishwa kwa manufaa ya watu wan je na siyo watanzania
  · Ufisadi umekuwa ni itikadi ya nchi na hakuna anayewajibika
  · Uzalendo na utaifa vimekufa na watu wanahamasisha udini, ukabila na ukanda waziwazi na hakuna kiongozi anayekemea na kwa maana nyingine wanayabariki yote
  · Wezi wa EPA wanapewa amnesty kuwa warudishe fedha na hawatashughulikiwa kisheria na pia watanzania hawajulishwi kuhusu hii sheria mpya kwa wezi na ikiwezekana iongezwe katika sheria zetu za makosa ya jinai.

  Hivi wewe huoni kuwa badala ya kutoa habari serikali inahangaika kuzuia yasijukane? Hivi utabiri huu unaupata katika njozi au wapi?

  Nawasilisha!
   
 2. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Hayo yalikuwa maoni yake.
  Hata kila mtu anaweza kusema anatabiri.
  Kuna yule mtu alitabiri kuwa May 21 itakuwa siku ya mwisho na haikuwa.
  Alafu ukizungumzia hizi tuzo za Mo Ibrahim,kumbuka wanaofanya maamuzi ni wanadamu kama wewe na mimi. Hivyo lolote lile linaweza kuwa. Kumbuka kuwa uongozi bora hauthibitishwi na tuzo,bali unathibitishwa kwa matendo,na yale ambayo watu unaowaongoza wanayasema.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hiyo tuzo huwa inaenda kwa watu wenye akili timamu mkuu! Do you think Tanzanians we have one? no ido not think so. The one we had is already dead long time ago.
   
 4. Nduka Original

  Nduka Original JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 753
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nahisi hata Bambo pia atapewa
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  tuko pamoja nimewasoma
   
 6. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu upo sawa na ukubwa na aina ya herufi ulizotumia?
   
 7. Nduka Original

  Nduka Original JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 753
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si umeona aisee
   
 8. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefurahisha na post kwamba hata Bambo atapewa tuzo..... Ina maana JK na Bambo ni sawa na alama hii JK< Bambo ??? Mathematicians mtanisaidia..
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  JK akipewa hiyo tuzo hata umaana wa tuzo utapotea!!!!!!!! And I don't think Mo Ibrahim is ready kuona relevance ya tuzo yao inapotea kirahisirahisi tu.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapa pazito kwa kweli kama Bambo atapata basi Nape pia au Omar Mahita kwa kazi kusema KAFU wana mapanga Au mbunge wa Mtera anaitwa nani huyu ?
   
 11. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Dr Salim Ahmed Salim si mtu wa visasi hata kidogo. Lakini tuhuma alizozushiwa wakati wa kugombea urais wakichuana na JK mwaka 2005 hata ungekuwa wewe zingekuumiza. Kwa sasa ndiyo mwenyekiti wa hiyo kamati inayochagua nani apewe hayo mabillioni ya Mo Ibrahim
   
 12. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Anajipendekeza si unajua kuna post wanapewa waandishi wa habari kama ukuu wa wilaya n.k
  Sasa wewe unadhani pasi kumsifia mkuu wa kaya atajulikana vipi?
   
 13. E

  ESAM JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mizaha mingine tuache bwana, tuzo kwa lipi hasa?
   
 14. M

  Maengo JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pqtqmu hapo!
   
 15. M

  Maengo JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na mimi natabiri: kabla hata hiyo tuzo haijatolewa huyu Vasco Da Gamma atakuwa ukonga akinyea ndoo....!
   
 16. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,139
  Likes Received: 3,328
  Trophy Points: 280
  Unamaanisha tuzo ya utawala mbovu na ufisadi.
   
 17. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  yaaani JK hawezikuipata hata kidogo
   
 18. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Kama tuzo ni zakuchezea,Basi huyo JK wenu atapata.Kazi kwelikweli kuongozwa na JK ni sawa na kuongozwa na kipofu
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Fikiria kabla ya kuandika nyie ndio ambao mnaqifanya hii JF kwa sasa ionekane ni sehemu ya watu kubwabwaja na kujiondolea ile sifa yake ya Great Thinkers. Hata hao walio pewa ni binaadamu na kuna makosa walifanya km hayo kwenye nchi zao , sio kwamba walikuwa clean 100% , hakuna binaadamu wa hivyo labda sasa useme wenye kupewa tunzo hiyo ni malaika tutakuelewa.
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Utabiri huu unafanana sana na wa jamaa zetu wa hali ya hewa kwenye luninga zetu za hapa Tz.
   
Loading...