Utabiri wa Hali ya Hewa wa Siku Tano na Athari Zinazoweza Kutokea

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
TAHADHARI ya Mvua Kubwa imetabiriwa kwa maeneo ya mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma na Morogoro kusini. Tafadhali CHUKUA TAHADHARI UWEZEKANO WA KUTOKEA: WA MKUBWA

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI (Mafuriko kutokea katika maeneo mengi na kuathiri jamii nzima, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kutopitika, hatari kwa maisha kutokana na maji kujaa au yanayopita kwa kasi)

ANGALIZO la Mvua Kubwa imetabiriwa kwa maeneo ya Mikoa ya Singida, Dodoma, Iringa na Tabora.

Tafadhali ZINGATIA NA UJIANDAE UWEZEKANO WA KUTOKEA: WA WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.
(Mafuriko kutokea katika mitaa na kusababisha msongamano wa magari na watu na hivyo kuchelewesha usafirishaji hasa katika maeneo ya mijini
 
Kwanza TMA siwaamini.

Pili,sina cha ku-comment tena.
mimi sitaki hata kuwasikia tangu siku walipotutishia eti kuna tsunami baadae wakadai walikuwa wanatupima watz kama tumejiandaa kukabiri majanga kama hayo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom