Utabiri TMA: Kimbunga Batsirai kupiga katika maeneo ya kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa Kimbunga Batsirai katika maeneo ya kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi.

TMA imesema Kimbunga hicho tangu kilipojitokeza katika bahari ya Hindi Januari 27, 2022 na kwa sasa kimesogea katika maeneo ya kisiwa cha Madagascar.

Kwa taarifa iliyotolewa Februari 4, 2022 na Mamlaka hiyo imesema uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonyesha kutokuwepo kwa uwezekano wa Kimbunga hicho cha Batsirai kufika katika Pwani ya Tanzania.

Imeeleza kuwa uwepo wa kimbunga hicho baharini unatarajiwa kuathiri mifumo ya hali ya hewa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha ongezeko la mvua, vipindi vya upepo mkali unaofika na kuzidi kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa baharini yanayozidi mita 2 hasa kwa maeneo ya ukanda wa pwani.

Taarifa hiyo imetaja maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua kubwa kutokana na uwepo wa kimbunga hicho baharini kati Februari 4 hadi 8 mwaka huu ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi , Ruvuma, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa.

Hata hivyo mvua za Msimu zinaendelea katika maeneo mengine yanayopata mvua hizo.

=====

Dar es Salaam, 04 Februari 2022:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga Batsirai katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi. Mamlaka imeendelea kufuatilia kimbunga hicho tangu kilipojitokeza katika bahari ya Hindi tarehe 27/01/2022 na kwa sasa kimesogea katika maeneo ya kisiwa cha Madagascar.

Uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kutokuwepo kwa uwezekano wa kimbunga Batsirai kufika katika Pwani ya Tanzania. Hata hivyo uwepo wa kimbunga Batsirai baharini unatarajiwa kuathiri mifumo ya hali ya hewa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha ongezeko la mvua; vipindi vya upepo mkali unaofika na kuzidi km 40 kwa saa na mawimbi makubwa baharini yanayozidi mita 2 hasa kwa maeneo ya ukanda wa pwani.

Maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua kubwa kutokana na uwepo wa kimbunga hicho baharini kati ya tarehe 04 hadi 08/02/2022ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa. Hata hivyo mvua za Msimu zinaendelea katika maeneo mengine yanayopata mvua hizo.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na kutoa mrejeo kila itakapobidi.

Mawasiliano
Kurasa za Karibu
Tovuti Mashuhuri
Nifanyaje?
 
Usikute kuna mzigo unapita. Zile tani kadhaa za sembe zilipopatikana tu, na kimbungakikaisha.
 
Huwa sihangaikagi nao hasa ni haya matangazo.

NB: Sijadharau mtu yeyote wala taasisi yoyote inayohisika na TMA bali ni mtizamo wangu binafsi.
 
Back
Top Bottom