Utabiri: Spika ajaye wa bunge la JMT atakuwa mwanaccm asiyekuwa mbunge, Dr Tulia ataendelea kuwa NS iwapo atamshinda Sugu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Ni utabiri wangu tu kwamba Spika ajaye wa bunge hatatoka miongoni mwa wabunge bali atakuwa ni mwanaccm ambaye siyo mbunge ama wa kuchaguliwa au kuteuliwa.

Naibu Spika wa sasa ataendelea na nafasi hiyo endapo atamshinda mbunge machachari na mbishi mh Mbilinyi aka Sugu pale Mbeya mjini.

Pia hapatakuwepo chama kikuu cha upinzani wala KUB kwa sababu kura zao na idadi ya wabunge haitatosha kwa mujibu wa kanuni. Yote kwa yote ACT wazalendo watakuwa ndio kioo cha upinzani wakibebwa na Pemba.

Mbatia hawezi kurudi bungeni lakini atapozwa na ukuu wa mkoa.

Ahsanteni.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nmejiuliza hao wooote kuanzia huyo spika mpk hao wa ukuu wa mkoa na KUB wako wakapigwa na CORONA then mwenyewe akawachukua itakuaje!! Hebu tupambane kwanza na hili lililokwepo watakaobaki ndo wataongelea hayo au we waonaje kamanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..kama hakutakuwa na kambi ya upinzani basi hakuna haja ya Spika kuchaguliwa toka nje ya bunge.

..suala lingine ni ku-save fedha za umma kwa kupunguza idadi ya viongozi wakuu wastaafu hivyo ni bora Spika Ndugai aendelee ktk nafasi hiyo.

..Nadhani Ndugai anaweza kuwa Spika mzuri ktk bunge lisilokuwa na kambi ya upinzani.
 
Dr Tulia ackson mbunge wa mbeya mjini 2020-2025

Sent using Jamii Forums mobile app
Leo kila mmoja akutambue, maana hizi taka ndio zinatuharibia JF.
Siku 3 za kwanza post 680 wastani wa post 9.4 per 1 hrs without sleeping!
Kweli ccm kuna magumegume kuliko Yale ya Kona bar!
Screenshot_20200417-175730.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe katika kipengela cha KUB.
Ili kupata kambi ya Upinzani ni lazima chama cha Upinzani kiwe na wabunge asilimia 12.5 ya wabunge wote.
Pia Kura za Rais zinaamua idadi ya viti maalum.
Hivyo sitegemeo kuwa na KUB next year.
Ni utabiri wangu tu kwamba Spika ajaye wa bunge hatatoka miongoni mwa wabunge bali atakuwa ni mwanaccm ambaye siyo mbunge ama wa kuchaguliwa au kuteuliwa.

Naibu Spika wa sasa ataendelea na nafasi hiyo endapo atamshinda mbunge machachari na mbishi mh Mbilinyi aka Sugu pale Mbeya mjini.

Pia hapatakuwepo chama kikuu cha upinzani wala KUB kwa sababu kura zao na idadi ya wabunge haitatosha kwa mujibu wa kanuni. Yote kwa yote ACT wazalendo watakuwa ndio kioo cha upinzani wakibebwa na Pemba.

Mbatia hawezi kurudi bungeni lakini atapozwa na ukuu wa mkoa.

Ahsanteni.

Maendeleo hayana vyama!

2020
 
Nakubaliana na wewe katika kipengela cha KUB.
Ili kupata kambi ya Upinzani ni lazima chama cha Upinzani kiwe na wabunge asilimia 12.5 ya wabunge wote.
Pia Kura za Rais zinaamua idadi ya viti maalum.
Hivyo sitegemeo kuwa na KUB next year.

2020

Kama wapinzani watakubali kushiriki uchaguzi huu bila kuwa na tume huru vya uchaguzi, tayari Magufuli ana matokeo mfukoni. Na lengo hasa ni bunge la ccm watupu litakalomuongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Ila iwapo kutakuwa na tume huru ya uchaguzi, na wapinzani kusimamisha mgombea halisi wa upinzani na sio hao wazee wachovu toka ccm, uje utoe mrejesho hapa jukwaani.
 
Mbatia kasema atakwepo ata kwa katiba hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom