battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,672
- 2,539
Ghassani kasha weka ruhusaAhsante ,niendelee kutoa wito kwa mods waombe idhini za waandishi wa hivi vitabu , waridhie maandiko yao kusomwa hadharani hapa jamii forum kwa Faida ya umma kujifunza walichokiandika.
Binafsi nitakitafuta kwa sababu umeniongezea njia ya kujifunza historia ya Zanzibar
kwa masharti yafuatayo:
Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
Harith Ghassany
info@kwaherikwaheri.com
SOMA HAPA KWANZA
Usambazaji wa kitabu hichi kwa mfumo wa Free Electronic Downloading unafanyika chini ya mkataba wa Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 ambao uko chini ya Sharia za nchi ya Marekani.
Kwa mujibu wa Mkataba na Sharia hii, mtu anayekichukuwa kitabu hichi kupitia mfumo huu ana uhuru pia wa kukigawa, kukirudufu na kukisambaza chini ya masharti yafuatayo:
Kulitaja jina la mwandishi wa kitabu kwa njia isiyohalalisha matumizi • binafsi ya kitabu
Kutokitumia kwa makusudi ya kibiashara wakati kinauzwa katika mfumo • wa kitabu
Kutokubadilisha, kugeuza, au kuongeza chochote kwenye kitabu hichi•
Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: Creative Commons — Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States — CC BY-NC-ND 3.0 US
Kitabu hichi kinatolewa bure katika mfumo huu ili msomaji anufaike na baadaye naye akipendekeze kwa mwenzake ili hatimaye ujumbe wa kusimamisha amani uliomo kitabuni uwafikie walio wengi.
Hata hivyo, mwandishi wa kitabu hiki anafahamu kwamba raha hasa ya kitabu ni kuwamo mikononi mwa msomaji, maana kitabu ni miongoni mwa vitu adhimu na vikongwe kabisa katika urathi wa mwanaadamu.
Kwa hivyo, licha ya kutolewa fursa hii ya mfumo wa kukisoma bure kitabu hichi kupitia kwenye mtandao, ni matarajio ya mwandishi kuwa wako watakaopendelea wawe nacho mikononi na kukisoma kwa nafasi zao.
Kwa vile walengwa wa mfumo huu wa Free Electronic Downloading ni Wazanzibari na Watanganyika wa kawaida, basi ipo haja kwa wale wenye uwezo, wakiwa ndani ama nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa mchango wa kuvinunua vitabu ama kupitia mtandao wa kitabu, http://kwaherikwaheri.com, au moja kwa moja kutoka Lulu na kuwafikishia walimu na wanafunzi walioko kwenye skuli na vyuo vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Skuli, vyuo, maktaba, taasisi na watu binafsi wanaweza kumuandikia moja kwa moja mwandishi kupitia mtandao wa kitabu http://kwaherikwaheri.com ikiwa watahitaji kupata msaada wa wafadhili watakaojitokeza kusaidia. Wafadhili ambao hawatopenda majina yao kujulikana, wamuarifu mwandishi. Majina yao yatahifadhiwa na mwandishi anatanguliza shukrani za dhati kwa ukarimu wao.
Mwandishi pia anatanguliza ombi na shukrani maalum kwa watakaoweza kusaidia kuviwezesha vituo vya mitandao vilivyopo Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara kutoa muda maalum wa huduma za mtandao kwa bei nafuu kwa ajili ya wale watakaopenda kukisoma, kukichukua na ama kukihifadhi kitabu hiki kwenye vyombo vyao.
Kuanzia hivi sasa, Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! kimo machoni mwako. Fungua kurasa zake, zama na zamia kwenye bahari yake na ibuka na lulu zilizomo ndani yake.
Mnakaribishwa nyote—walio karibu na walioko mbali.
http://kwaherikwaheri.com