Utabiri: Rais ajaye atakuwa kijana, jina mchanganyiko kiislamu na kikristo au ameoa dini nyingine

ImageUploadedByJamiiForums1419839335.981970.jpg

Alichokijibu January
 
Maalim Hassan Hussein, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya Hussein, ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani, likiwamo la kufariki ghafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenye mbio za urais mwakani.
 
Mtu mshamba,muongo na mbabaishaji kuliko wote Tanzania ni Mtoto Wa shekh yahya,anatabiri kwa masirai ya tumbo lake na kujipendekeza kwa viongozi walioko madarakani pia anajifanya yeye ni Mungu kwa kutabilia binadamu ambao yeye akuwaumba.

Alitabilia uongo viongozi kuwa vichaa na kufa kabisa hasa wa upinazani

Alisema hali kadhalika, "kiongozi mmoja wa kisiasa mwenye wafuasi wengi na umaarufu mkubwa, mwishoni mwa mwaka huu ataugua kichaa na kumsababishia kuanguka kisiasa. Hussein alisema mbali na hayo, Tanzania itakumbwa na msiba wa kitaifa huku umaarufu wa Rais Jakaya Kikwete, ukizidi kuongezeka hasa kwa kutatua migogoro mikubwa nchini"

Huyu dogo anatakiwa atambue kuwa viongozi bora wanaosimamia masilai ya UMMA ni mpango wa Mungu,Mungu ndiye mpangaji wa maisha ya Mtu na si mtoto wa shekh yahya hussein,Kwani saut ya UMMA ni saut ya Mungu

Bado anaendeleza mambo ya kipuuzi kama yale yaliyo muua baba yake,kwani shekh yahya .alikufa kwa laana, pia #Mungu_ajalibiwi ,

Biblia inasema yeyote atabiliaye wenzae kifo na hilhali yeye si MUNGU,hufa hakika badala wale aliyowatabilia.

Biblia inasema nebukadneza alikuwa mkuu wa waganga na alitaka kupambana na watu wa Mungu akashindwa akaishia kula nyasi sembuse huyu mtoto wa shekh yahya? "Ee Belteshaza, mkuu wa waganga, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani" daniel 4:9

MUNGU anasema yeye ndiye anayepanga na kuchagua viongozi wa Dunia, " Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa, naye humpa amtakaye, awaye yote. Daniel 4:32.

Onyo mtoto wa sheikh yahya,Maalim Hassan Hussein akiendelea kutabiri mambo yasiyo Adili aweza kufa hata hasione Uchaguzi Mkuu 2015
 
Nadhani kamtabiria Kifo Edward Lowasa. Haya tunasubiri kula ubwabwa

Pathetic indeed!!! Mkuu jaribu kuwa na Utu, na wewe ni binadamu utaionja Mauti pia, akuna anae juwa nan ataanza kutangulia! Kufraia kifo cha mtu mwingine ni Ujinga kaka ata kama ni siasa bt haipendezi, kumbuka ww ni binadamu na una ndugu jamaa na marafiki nao watakufa.
 
Huyo ni mwongo. Hakuna mwanadamu anayejua hatima ya maisha yake/ya mtu mwingine. Naamini njaa inamsumbua maalim. Namshauri atafute kazi ya kufanya aache kutapeli kwa kujifanya mtabiri.
 
Dar es Salaam. Maalim Hassan Hussein, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya Hussein, ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani, likiwamo la kufariki ghafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenye mbio za urais mwakani.

Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali.Akitangaza utabiri wa mwakani, alisema: "Kiongozi huyo atakufa wakati akipelekwa hospitalini."

Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika kutafuta sababu za kifo chake.

Mtabiri huyo alisema nyota inaonyesha kwamba misiba miwili ya kitaifa itatokea mwakani.

Kuhusu uchaguzi wa kiti cha urais mwaka 2015, alisema kati ya kundi la vijana na wazee, nyota zinaonyesha kwamba watakaofaidika ni vijana.

"Lakini kuna wazee pia wanaoweza kufaidika, hawa ni wale wenye sura za ujana, yaani babyface au wenye kupenda mambo ya ujana na kushirikiana na vijana," alisema.

Alisema ili Tanzania ilinde sifa ya kuwa nchi yenye amani na utulivu ni kuwa na Rais kijana mwenye mchanganyiko wa dini mbili au mwenye ndoa ya dini tofauti.

Alisema utabiri unaonyesha kuwa mwaka 2015 utatawaliwa na nyota yenye kupendelea vijana, hivyo ni vyema vyama vya siasa vikawasimamisha kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani.

Kuhusu mauaji, fujo na ghasia alisema vitatawala katika uchaguzi ujao na kwamba Serikali inatakiwa kuweka tahadhari kubwa.

Pia alitabiri viongozi wawili wa siasa na dini kukumbwa na kashfa ya ngono itakayowasababisha anguko la utumishi wa kutukuka na familia zao.

Alisema mwaka ujao utakuwa na mafuriko na dhoruba vitakavyosababisha madhara, hivyo tahadhari ichukuliwe kuanzia sasa.

Alisema kutakuwa na vifo vya ghafla vya wasanii, wanamichezo na watu maarufu kama ilivyokuwa mwaka 2014

Maalim Hussein alisema lile tishio la wahisani kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi, litalegezwa na kuifanya nchi kuingia katika Uchaguzi Mkuu kwa staha.

Alisema wazee wataendelea kushutumiana na kupingana hadharani, hali itakayosababisha migawanyiko ndani ya vyama vya siasa na nchi kwa jumla.

mwananchi

 
[/I said:
Pia alitabiri mwaka 2015 utamweka wazi kiongozi mmoja mashuhuri wa siasa nchini kurukwa kwake kwa akili bila kufichwa au kusitiriwa kama ilivyokuwa katika mwaka 2014.
=========================

Chanzo
:Nipashe

Duh hii Kali! ni Kiongozi gani huyu aliyerukwa na akili mwaka 2014 bila kujulikana? kama yametokea haya basi hatari sana maana mtu anaongoza watu kumbe ni mwendawazimu?
 
Kweli TZ inaendelea kudidimia kwenye u-third world. Ni wakati watu wanapokosa hope na la kufanya ndio watu kama hawa hutokea na kusikilizwa.
 
Ye kajuaje? Kama ye mtabiri kweli mbona alishindwa udiwani pale magomeni 2010...ina maana alishindwa kujitabiria kuwa atashindwa?
je baada ya kushindwa udiwani alikimbilia chama gani?? naskia amehama kule alikogombea huo udiwani
 
kwani yy yupo mioyoni mwetu,kwani yy atafanya maamuzi kwa niaba yetu sisi sote......tunamjua tumtakaye apite mbali na majini yake.
 
Back
Top Bottom