UTABIRI: Miaka kadhaa ijayo CCM itafumuliwa na kuundwa upya. Watabadili jina?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,509
8,823
Huwezi kutaja Sserikali ukaacha kuitaja CCM, CCM na Serikali ni pande mbili tofauti zilizo kwenye sarafu moja, Dkt. Bashiru hakukosea kusema "mwenye dola atabaki madarakani", hiyo kauli ni halali iwapo kuna vyama imara vya upinzani.

Migogoro, tamaa ya madaraka na hujuma ndani ya CCM zinachelewesha maendeleo kwa wananchi, Mfano kumhujumu Rais kwa kumpelekea mtu asiyefaa kwenye taasisi nyeti ili aonekane nafanyi kazi huko sio kumkomoa raisi ni kuwakomoa wananchi.

CCM imejiunganisha na dola, makundi ndani ya CCM ndio haya yanayosababisha siri za serikali kuvuja, chuki na kuhujumiana,

Kadri siku zinavyokwenda tishio la kugombea madaraka ndani kwa ndani ndivyo linavyozidi kuongezeka.
Na hill tishio ili liishe kuna namna mbili pekee?

1. Kuvipa nguvu vyama vya upinzani?
2. Kuivunja na kuisuka upya CCM kwa kuitenganisha na Serikali?

Je, baada ya miaka 20 tutakuwa na siasa za namna gani?
 
Kama vipi hiyo CCM ife kabisa. Maana haina faida yoyote ile kwa nchi yetu. Zaidi tu yakupigana vikumbo kwenye kuitafuna keki ya Taifa.
 
Huwezi kutaja Sserikali ukaacha kuitaja CCM, CCM na Serikali ni pande mbili tofauti zilizo kwenye sarafu moja, Dkt. Bashiru hakukosea kusema "mwenye dola atabaki madarakani", hiyo kauli ni halali iwapo kuna vyama imara vya upinzani...
Kwani kuifuta kabisa kwenye usajili wa vyama vya siasa ni bei ngapi??.
 
Kama vipi hiyo CCM ife kabisa. Maana haina faida yoyote ile kwa nchi yetu. Zaidi tu yakupigana vikumbo kwenye kuitafuna keki ya Taifa.
Itakufa na kujibadili, ila kitakachobadilika ni jina tu,

Unaweza kuniambia kwanini TAA ilibadili jina na kuamua kujiita TANU?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom