Utabiri: Mawaziri hawa wawili wa Magufuli watakuja pata lawama kama waziri Mngai wa Mkapa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,326
Waziri Joseph Mngai alipata na mpaka leo anaendelea kulaumiwa kwa mabadiliko aliyoyafanya alipokuwa waziri wa Elimu enzi za Mkapa.

Kama ilivyo kwa Mungai,Hata Waziri Maghembe wa Magufuli huenda nae akaja kubeba lawama kutokana na swala la ku-introduce VAT kwenye sekata ya Utalii.

Ukiacha Maghembe,Mama Ndalichako,kama waziri mwenye dhamana na Elimu,sidhani kama atakwepa lawama hata kama yeye hahusiki moja kwa moja kutokana na mabadiliko haya hapa chini.

http://www.tcu.go.tz/images/documents/REVISED_ADMISSION_CRITERIA_2016_final.pdf

Tusubiri.
 
Mama Ndalichako anataka kurudisha Elimu Bora au Ubora wa Elimu uliokuwa umepotea kwa miaka mingi sana. Namshauri akaze sana kuepusha watu wasio na uwezo kwenda vyuoni akina Juma K. Ambaye alijigamba kushindana na Mbaraka mwinshehe.

Huyu Mama ana akili sana. Na nmependa anatumia akili zake ipasavyo. Nchi hii itamkumbuka sana kwa jitihada zake za kuleta nidhamu kwenye Elimu
 
Mama Hawezi kulaumiwa kwa hili; atakuja kuonekana shujaa baada ya miaka kadhaa kwa kurudisha heshima ya elimu yetu.
 
Back
Top Bottom