Utabiri: Mabadiliko ya Kikatiba kuongeza idadi ya wabunge wa kuteuliwa na Rais yanaweza kutokea

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
Kama kweli kuna nia na dhamiira ya dhati ya kuwajibishana bila kuangaliana usoni na hali hii ikawa endelevu kwa muda ulipbaki,basi itafika mahali Raisi ataomba aongezewe idadi ya wabunge wa kuteuliwa ambapo Bunge litaombwa kufanya mabadiliko hayo ya kikatiba ili Raisi aweze kuteua watu wengine anaoona wanafaa maana naona upo uwezekano mkubwa wa nafasi hizo kumi alizonazo sasa kikatiba kujaa ndani ya muda mfupi tu na msishangae hata mrithi wa Kitwanga akatoka nje ya wabunge wa kuchaguliwa.

Utabiri huu umetokana na mambo matatu:

Mosi,Raisi kuchukua muda mrefu kutangaza Baraza la Mawaziri tofauti na ilivyokuwa imezoeleka.

Pili,hata baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri,Raisi bado alishindwa kuwapata baadhi ya mawaziri-hapa bila shaka pana tatizo tena kubwa tu la nani anafaa awe waziri wangu miongoni mwa hawa wabunge.

Tatu,sitarajii watu hawa watabadilika na hivyo kama kweli Raisi ana dhamira ya kubadili mindset ya mawaziri wanaotokana na CCM kwa kuwawajibisha kwa mtindo huu,basi atafukuza wengi na kujikuta ameishiwa wa kuteua.

Tusubiri unless hili la waziri Kitwanga lina sababu zingine kama baadhi yetu tunavyohisi.
 
Ni kweli kabisa. Idadi ya wateuliwa iongezwe.
Suluhu hapa sio kuongeza idadi ya wabunge wa kuteuliwa na raisi bali ni kutekeleza Katiba ya Mzee Warioba ambayo inapendekeza mawaziri wasitokane na wabunge.
 
Back
Top Bottom