KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,589
- 4,599
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, Rais Magufuli aliahidi kumpa Tundu Lissu cheo serikalini kama akishinda.
Binafsi naamini Rais Magufuli atatekeleza ahadi hiyo kwa Mhe. Lissu. Naamini Lissu hatoweza kukataa nafasi hiyo impite kwa kuwa anajua watanzania walimchagua Rais Magufuli kihalali kabisa ndio maana alipotoa wito wa maandamano watanzania walimpuuza hivyo atakubaliana na kila kitu na kukubali kuitumikia nchi yake kama akiteuliwa.
Kwa mfano, siku za karibuni kumekuwa na maneno mitandaoni juu ya nia ya Lissu kuhutubia bunge la Ulaya lakini ameonekana kupinga hilo suala na hii inaonyesha namna gani Lissu anavyojiweka karibu na kukubaliana na serikali. Pia, suala lake la kumuomba Rais Magufuli kutaka maridhiano na wapinzani wake inaonekana pia hajakubaliana na maamuzi ya chama chake juu ya kutochagua viti maalumu .
Uamuzi pekee alionao Lissu kwa sasa ni kukubaliana na serikali ili ajiweke karibu na ahadi ya Mhe. Rais kwa sababu haamini tena chama chake wala viongozi wake wana nia gani kwa mustakabli wa uongozi wa chama na nchi yetu.
Kama Lissu akikubali uteuzi hakika kutakuwa na majuto makubwa ndani ya CHADEMA na watapitia kipindi kigumu katika historia ya chama hicho toka kianzishwe.