Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,319
- 17,474
Bernie Sanders ndiye atakayekuja kuwa Rais wa 46.
Kuna vita Marekani kati ya matajiri na masikini, mfumo uliopo sasa unakandamiza sana watu wa kawaida. Pengo kati ya matajiri na wafanyakazi limezidi kuongezeka. Mfano, watu watatu matajiri kabisa wanautajiri mkubwa kuliko nusu ya wananchi wa kawaida.
Matajiri wa kupindukia wamezidi kuongeza utajiri wao na hivyo kuhakikisha hali hiyo ikiendelea. Wanafanya hivi kwa kuwatumia wanasiasa kupitisha sheria zinazotungwa kila kukicha ili waendelee kujilimbikizia mali.
Wafanyakazi wa kawaida wanaendelea kuzidi kuwa masikini, kwa kuwa gharama za maisha zimeongezeka, huku vipato vikibaki vile vile. Moja ya gharama kubwa za maisha ni afya ambapo bima za afya zimezidi kuongezeka. Makampuni ya madawa yanaweka gharama juu sana ili hisa za makampuni hayo ziongezeke na hivyo kufanya makampuni ya bima kupeleka gharama hizo kwa wateja wao.
Kwenye elimu nako hakuna uwiano wa pesa zinazotolewa na serikali, kati ya jamii masikini na zile za kati. Hii inasababisha watoto wanaokaa maeneo ya watu wenye vipato vya chini kupata elimu duni wakati serikali inayotoa pesa kwa umma ni moja.
Tukija kwenye huduma za jamii kama maji ni hivyo hivyo, hakuna uwiano wa usafi wa maji baina ya maeneo ya matajiri na masikini. Mfano bomba la mafuta la North Dakota lilibadilishwa njia kutoka kupita kwenye jamii ya watu wenye uwezo na kupelekwa kwa masikini.
Katika chaguzi za Demokrati za kumtafuta mgombea wa chama zinazofanyika mwaka huu, Bernie Sanders ndiye mgombea pekee ambaye sera zake zinawalenga wananchi wa kawaida. Amepanga kongeza wigo wa bima ya wazee ya serikali (Medicare) ili iwe kwa watu wa umri wote. Hii itaondoa ukiritimba wa sasa kwa makampuni binafsi ya bima ya afya kunyanyasa raia wa kipato cha chini.
Pia amepanga kuleta uwiano wa pesa zinazotolewa na serikali katika vitongoji mabalimbali ili watu wote wapate wanachostahili. Pesa hizi ni pamoja zile za shule na maktaba.
Bwana Sanders yeye amekataa kuchukua pesa za matajiri, ambao wanakawaida ya kuhonga wagombea, pesa za kampeni ili waweze kushinda chaguzi zao. Wagombea hao wanaposhinda huenda kuwafanyia kazi makampuni na matajiri badala ya wananchi. Hiki ndicho chanzo cha kuendelea kuwa na pengo la matabaka Marekani ambapo tajiri namba moja duniani, kampuni yake (Amazon) haijalipa kodi (mwaka jana) hata senti moja. Huku mwalimu wa chekechea akilipa kodi 15% ya kipato chake cha mwaka.
Sera hizi za Sanders zimemfanya apendwe sana na wamarekani wengi. Na kuna tetesi kuwa, mwaka 2016 wafuasi wengi wa Sanders walimpigia kura Rais Trump kwa hasira baada ya bwana Sanders kunyang'anywa na chama nafasi ya kuwa mgombea. Mwaka huu watu hao wanategemewa kumpigia mgombea huyo pale atakapo chaguliwa na chama na hatimaye Rais wa nchi.
Wazee wa chama cha demokrati hawamtaki bwana Sanders kuwa mgombea, kwa kuwa wanafaidika na mfumo uliopo sasa. Hivyo, wamekuwa wakitumia njia nyingi ikiwemo vyombo vya habari kumzuia asionekane na wananchi. Hata hivyo kadri siku zinapokwenda mzee wa watu anazidi kuyoyoma na anategemewa kunyakuwa kiti cha mgombea wa chama.
====
Japo siyo kwa umuhimi, niliwahi kutabiri hapa kuwa atachaguliwa mgombea wa chama (December 6th 2019).