Ahalan wasahlan wamarhaban bikum!
Wapendwa wasomaji na wenye hamu ya kufahamu mambo mbali mbali, nimependa kuwaletea mada hii ili kuweza kujua mbinu mbali mbali wanazotumia binadam wenzetu wenye roho mbaya katika kuumiza binadam wenziwao.
Uchawi ni fani maalum yenye uwanja mpana, ni sayansi ya kimazingara yenye kuhitaji utaalamu, umahiri na ushujaa ili mtu kuweza kukabiliana nao.
Ila kabla ya kulezana mbinu zitumikazo katika kuumiza watu ni vyema basi tukifahamu huu uchawi nini na pia mtu anawezaje kuwa mchawi. Naomba ufuatilie kwa umakini kwani huwenda wewe ukawa mmoja wa hao waathirika wa hii sayansi iliobobea hapa Tanzania.
Uchawi ni maradhi hatari sana na ni silaha ambayo mtu huuitumia dhidi ya adui yake pasi na kumgusa.
UCHAWI NI NINI?
Ni fundo au kisomo kinachosomwa ama kuandikwa au hufanywa kitu kitakacholeta athari katika kiwiliwili cha mlengwa pasi na mlengwa kuguswa.
Elimu hii ya uchawi mara nyingi huambatana na elimu ya unajimu(astrology) kwa kushirikiana na kiumbe khabithi anaejulikana kama jini (demons ama aliens). Elimu hii imezama sana katika tabia asili za kimaumbile.
VIPI MTU HUWA MCHAWI
Fahamu ewe ndugu yangu mpendwa!
Hakika ya binaadamu hawi mchawi mpaka afikie daraja kubwa katika kufuru pamoja na ukhabithi mkubwa wa shetani katika kumfanya binaadamu akufuru yale anayoyatukuza. Namna ya kufuru hii itategemea na dini husika ya mtu kama tujuavyo hakuna mwanadamu asie na dini.
Mfano, ikiwa mtu ni myahudi basi shetani atamfanya akufuru tawrat, na ikiwa ni mkiristo atamfanya akufuru injili, na akiwa muislam atamfanya akufuru Quran.
Kufuru hii huwa ni kuandika maandiko matakatifu ama kwa kutumia damu ya hedhi, au kukitia mkojo hicho kitabu husika, kisha hufuatia na manuizi ya kitalasimu na huwa wanasema maneno yafuatayo. "Ewe mungu nipe katika dunia haya ninayoyataka na ukanichome huko akhera". Na mara tu akikikashifu hicho kitabu basi ataona katika kifua chake kama kitu kimemtoka na ndio hapa sasa huweza kufanya jambo lolote atakalopewa afanye.
Na ili mtu aweze kukubuhu katika hii fani ni lazma azidishe kufuru. Hivo wanaweza kuchinja vichanga, kuzini na mama wazazi wao hata pia na mabinti wao wa kuwazaa. Wafanyao haya ni wale waliobebea katika hii fani bali pia lipo kundi dogo la wachawi ambao hawa maarufu hujulikana kama wanga. Hawa huwa na organization zao ama jumuiya yao ambayo hukutana na kutekeleza mambo yao tofauti tofauti, na huwa wanamakao makuu ya kufanyia mikutano yao [diningi]. Huku watu hufanywa mazuzu ama misukule, hutumishwa kulima na kufanyishwa kazi mbali mbali. Kwa upande wa Unguja inasemekana makao makuu ya hawa watu inasemekana ipo BUMBWINI na upande wa Pemba tokea enzi za gwiji wa uchawi Tanzania BI KIREMBWE ni Ukutini.
YANAYOFANYWA ILI KUTIMIZA MISSION YA KUUMIZA WATU.
1]Wanachukua jina lako na la mama yako, wakishapata hivi vitu kazi yao huwa imekishwa, hapo huwa huna ujanja tena, na utaingia tu katika mtandao wao, wanatumia jina la mama kwakua upande wa mama nasabu(ukoo) haupotei hivo hata kama mtoto atakua baba yake hajulikani basi huwa shida mana siri ya uhalali wa baba wa mtoto huijua mama tu. Halafu hapo hupigwa hesabu kwa mujibu wa herufi za kiarabu zijulikanazo kama abjad. Herufi hizi huwa zina code kwa kila herufi ina ujazo wake ulionzia 1 mpaka 1000.Mfano wakipata 800 basi watagawanya na 12,idadi ya nyota (buruji) hapa wanapata nyota yako, halafu wagawa kwa 7 wanapata siku na saa ya kurusha kombora lao, Kisha wanagawa kwa 4 wanapata kujua tabi yako, hapo sasa ndio utakapokua the walking dead (mfu unaetembea) Kisha zikikamilika hizi hisabu huwa wanakuweka kwenye mtandao wao yaani unakua kama ulioekewa chip na wanakudhibiti na kukuendesha watakavyo.
Wanachozingatia tabia yako Kwani wanasema ulimwengu umegawanyika katika tabia kuu nne.
1)Moto
2)upepo
3)Maji
4)Udongo
Pia huzingatia hali ya mwili wako, kwani miili ya wanaadamu ina hali kuu mbili, bardaa(yaani wenye damu baridi) hawa ni wale ambao msukumo wao wa damu upo wa chini yaani mara nyingi huwa wanapata pressure ya kushuka na Harraa(hawa ni wale ambao wana damu mto) hawa huwa wana damu moto yaani wenye pressure ya kupanda. Hapa ndio tunaona ufanyaji kazi wa hawa watu ni zaidi ya majasusi mana sio kama kukamila kwa vitu hivo na mahesabu hayo huwa ndio umekwisha kabisa kabisa, bali watahitaji vinasaba vyako yaani DNA zako na mara nyingi huchukua vitu vifuatavyo.
1)Nywele zako na ndio mana wanawake wanashauriwa kuhifadhi nywele zao zinazotoka wakati wa kusuka.
2)Wanaweza kuchukua kucha zako unazokata
3)Wanachukua nyuzi ya nguo yako ya ndani na hapa ndio utaona kuwa hukuti wanawake wajuzi wa mambo kuanika nguo zao za ndani nje
4)Wakikosa vyote hivo basi watachukua japo alama zako za nyao za viatu ili kufanikisha mission ya kukudhibiti.
Kwa hio, baada ya hatua tajwa za hapo juu, basi kombora lako litatupwa sehemu husika kama wewe ni tabia yako udongo basi watazika chini ya jiko, kama wewe tabia yako moto watatupa kwenye moto.
wewe ukishakua tayar tu kutaka kutia kinyesi kwenye kitabu unachokiamini nifate yote yatawezekna ayomi nataka uchawi wa kuzuia luku isiishe na nikimkopa mtu ajisahau asinidai kabisa
mwenye huo uchawi aje pm tufanye business
Mtoa maada ni mwongo mpotoshaji mnafiki,ifahamike uchawi hauna maana kabisa uchawi ni nguvu ambayo ili itende kazi inaanzia kichwani au mawazoni mwako.uchawi ni upuuzi tu mtoa mada ni wale wasio jiamini mtu yeyote anae jiamini halogeki
Sent using Jamii Forums mobile app
MmmmhMm imenitokea na mpk sasa nimewekewa majini mwilini mwangu....alieyaweka anaona choxhote nifanyacho nahadikunirekodi matendo yangu...naninamsikia maongezi yakeyote anayofanya na ubaya anaonitendea....huyo hayajamkuta bado
Inawezekana kurogwa, mana wachawi hutumia pia majini katika kupata taarifa za mtu, ama pia hutumika katika kuficha Uchawi sehemu husikaEti ni kweli kuwa mtu wa mbali hawezi mroga mtu ?
Kwamba hadi ashirikiane na mtu wa karibu ya huyo mtu?
Je wachawi kama
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wapi ungependelea nikamilishe?Nawewe mtoa maada kwanini usimalizie uzi wako?
Unalengo gani hasa?
References za uzi wako ziweke hapa kama na wewe bado haujaelewa hitimisho lake ili tujue pa kuanzia kisha tuchangie na sisi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha, hapana mimi professional yangu ni afyaMleta mada nina wasiwasi na wewe ulikua mmoja wao ingawa sina uthibitisho, kwa haya ulioandika sio rahisi kuyajua kama ww sio mtu wao.
sent using samsung galaxy s8
Inawezekana kurogwa, mana wachawi hutumia pia majini katika kupata taarifa za mtu, ama pia hutumika katika kuficha Uchawi sehemu husika
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kumbe BI KIREMBWE aliwahi ku exist kweli, nilikua naskia watu wa kiswahili wakimtajataja shuleni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza ifahamike kuwa kila mwanaadamu ana jini wake wa asili huyu anaitwa kariin (rafiki) jini huyu huambatana na binaadam once tu anazaliwa na atakua nae mpaka siku ya kufa kwake. Kariin huyu hujua mambo yote ya huyo binaadam anaeambatana nae, hivo basi mchawi ama mtu anaetaka kukuroga, anapoenda kwa mganga, mganga hutumia jini lake kisha humtuma aende kwa mtu husika, afikapo huko sasa kwa mlengwa lazima afike kwa kariin ili aweze kupata taarifa zako. Ndio ukienda kwa mganga tu tayari anakua ashajua shida zako ila mchezo unaochezeka ndio huu. Hio ni kwa ufupi tu kama hujafaham basi niambie nikujuze zaidiNimekuelewa kipengele (a) lakini hapo kipengele (b) sijakuelewa vizuri!
Kwamba majini pia hutumika kuficha uchawi sehemu husika ? Kwa vipi? Fafanua kwa mfano ili upate kueleweka vizuri !
Sent using Jamii Forums mobile app
Upumbavu mtupuAhalan wasahlan wamarhaban bikum!
Wapendwa wasomaji na wenye hamu ya kufahamu mambo mbali mbali, nimependa kuwaletea mada hii ili kuweza kujua mbinu mbali mbali wanazotumia binadam wenzetu wenye roho mbaya katika kuumiza binadam wenziwao. Uchawi ni fani maalum yenye uwanja mpana, ni sayansi ya kimazingara yenye kuhitaji utaalamu, umahiri na ushujaa ili mtu kuweza kukabiliana nao.
Ila kabla ya kulezana mbinu zitumikazo katika kuumiza watu ni vyema basi tukifahamu huu uchawi nini na pia mtu anawezaje kuwa mchawi. Naomba ufuatilie kwa umakini kwani huwenda wewe ukawa mmoja wa hao waathirika wa hii sayansi iliobobea hapa Tanzania.Uchawi ni maradhi hatari sana na ni silaha ambayo mtu huuitumia dhidi ya adui yake pasi na kumgusa.
UCHAWI NI NINI?
Ni fundo au kisomo kinachosomwa ama kuandikwa au hufanywa kitu kitakacholeta athari katika kiwiliwili cha mlengwa pasi na mlengwa kuguswa. Elimu hii ya uchawi mara nyingi huambatana na elimu ya unajimu(astrology) kwa kushirikiana na kiumbe khabithi anaejulikana kama jini (demons ama aliens). Elimu hii imezama sana katika tabia asili za kimaumbile.
VIPI MTU HUWA MCHAWI
Fahamu ewe ndugu yangu mpendwa!
Hakika ya binaadamu hawi mchawi mpaka afikie daraja kubwa katika kufuru pamoja na ukhabithi mkubwa wa shetani katika kumfanya binaadamu akufuru yale anayoyatukuza. Namna ya kufuru hii itategemea na dini husika ya mtu kama tujuavyo hakuna mwanadamu asie na dini.
Mfano, ikiwa mtu ni myahudi basi shetani atamfanya akufuru tawrat, na ikiwa ni mkiristo atamfanya akufuru injili, na akiwa muislam atamfanya akufuru Quran.
Kufuru hii huwa ni kuandika maandiko matakatifu ama kwa kutumia damu ya hedhi, au kukitia mkojo hicho kitabu husika, kisha hufuatia na manuizi ya kitalasimu na huwa wanasema maneno yafuatayo. "Ewe mungu nipe katika dunia haya ninayoyataka na ukanichome huko akhera". Na mara tu akikikashifu hicho kitabu basi ataona katika kifua chake kama kitu kimemtoka na ndio hapa sasa huweza kufanya jambo lolote atakalopewa afanye.
Na ili mtu aweze kukubuhu katika hii fani ni lazma azidishe kufuru. Hivo wanaweza kuchinja vichanga, kuzini na mama wazazi wao hata pia na mabinti wao wa kuwazaa. Wafanyao haya ni wale waliobebea katika hii fani bali pia lipo kundi dogo la wachawi ambao hawa maarufu hujulikana kama wanga. Hawa huwa na organization zao ama jumuiya yao ambayo hukutana na kutekeleza mambo yao tofauti tofauti, na huwa wanamakao makuu ya kufanyia mikutano yao [diningi]. Huku watu hufanywa mazuzu ama misukule, hutumishwa kulima na kufanyishwa kazi mbali mbali. Kwa upande wa Unguja inasemekana makao makuu ya hawa watu inasemekana ipo BUMBWINI na upande wa Pemba tokea enzi za gwiji wa uchawi Tanzania BI KIREMBWE ni Ukutini.
YANAYOFANYWA ILI KUTIMIZA MISSION YA KUUMIZA WATU.
1]Wanachukua jina lako na la mama yako, wakishapata hivi vitu kazi yao huwa imekishwa, hapo huwa huna ujanja tena, na utaingia tu katika mtandao wao, wanatumia jina la mama kwakua upande wa mama nasabu(ukoo) haupotei hivo hata kama mtoto atakua baba yake hajulikani basi huwa shida mana siri ya uhalali wa baba wa mtoto huijua mama tu. Halafu hapo hupigwa hesabu kwa mujibu wa herufi za kiarabu zijulikanazo kama abjad.
Herufi hizi huwa zina code kwa kila herufi ina ujazo wake ulionzia 1 mpaka 1000.Mfano wakipata 800 basi watagawanya na 12,idadi ya nyota (buruji) hapa wanapata nyota yako, halafu wagawa kwa 7 wanapata siku na saa ya kurusha kombora lao, Kisha wanagawa kwa 4 wanapata kujua tabi yako, hapo sasa ndio utakapokua the walking dead (mfu unaetembea) Kisha zikikamilika hizi hisabu huwa wanakuweka kwenye mtandao wao yaani unakua kama ulioekewa chip na wanakudhibiti na kukuendesha watakavyo.
Wanachozingatia tabia yako Kwani wanasema ulimwengu umegawanyika katika tabia kuu nne.
1)Moto
2)upepo
3)Maji
4)Udongo
Pia huzingatia hali ya mwili wako, kwani miili ya wanaadamu ina hali kuu mbili, bardaa(yaani wenye damu baridi) hawa ni wale ambao msukumo wao wa damu upo wa chini yaani mara nyingi huwa wanapata pressure ya kushuka na Harraa(hawa ni wale ambao wana damu mto) hawa huwa wana damu moto yaani wenye pressure ya kupanda.
Hapa ndio tunaona ufanyaji kazi wa hawa watu ni zaidi ya majasusi mana sio kama kukamila kwa vitu hivo na mahesabu hayo huwa ndio umekwisha kabisa kabisa, bali watahitaji vinasaba vyako yaani DNA zako na mara nyingi huchukua vitu vifuatavyo.