Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Watanzania huwa tunapenda sana kudharau taaluma za watu. Taaluma ambazo zinatokew jasho mashuleni na vyuoni pamoja na kupitia uzoefu wa kikazi.
Fastjet walipozuiliwa wasirushe ndege zao watanzania tukaongea mengi sana tukiyahusisha na siasa. Kampuni haikuwa na mtaalam ambaye anapaswa kufanya kazi na mamlaka ya anga TCAA. Mtaalam ambaye anapaswa kuihakikishia mamlaka juu ya usalama wa ndege.
Zikaingia siasa za eti lengo ni kuiwezesha ATCL na ndege zake liweze kushamiri kibiashara. Watu wakasahau kabisa kuwa ndege za Fastjet zilikuwa zinahatarisha maisha ya abiria, kwani zilikuwa ni spana mkononi.
Mamlaka ya anga kama mdhibiti mkuu wa sekta nzima ya anga, haikutaka kuhatarisha uhai wa nguvu kazi ya nchi hii.
Leo hii kampuni ya Boeing imeingia matatani baada ya ndege mbili aina ya 737 kuanguka katika kipindi kifupi. Mamlaka ya anga ya China imezizua ndege za aina hiyo zisiruke katika anga la nchi hiyo.
Weledi huwa na faida kubwa unapoheshimiwa na kupewa uhuru wa kufanya kazi, kinyume cha hapo ni muendelezo wa ajali nyingi huku tukimsingizia Mungu kwamba ni mipango yake.
Yaani Mungu huyo huyo anayeombwa ili maisha ya wagonjwa yapone, awe ni wa kuridhia vifo ambavyo vinaweza kuzuilika!.
Watanzania lipo somo zuri kwetu kupitia namna ambavyo jamii ya kimataifa inavyoliweka katika wakati mgumu kampuni ya Boeing. Sio kila kitu kitazamwe kisiasa, kuna suala la kuheshimu taaluma na weledi wa watu.