Utaalam uheshimiwe, ilipozuiliwa Fastjet watu wakaleta siasa. Boeing wanakiona cha moto

Mtakuwa na akili sana kama sababu ndio zilukuwa hizo
Yaani mmezuia ajali nyingi hahaha
Hayo mabasi yanauwa watu kila kukicha hayana wataalamu?
Na hayo mashangingi yanauwa wenye elimu hao hao nao tuwaweke kundi gani?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Kama unafikiri serikali haikuwa na lengo la kuiua Fastjet ili kuiwezesha Air Tanzania basi wewe ni mtu wa kuhurumiwa sana, hujui serikali ya awamu ya tano inavyofanya kazi.

Kimsingi, Magufuli hapendelei sana suala na private sector, hasa pale ambapo kuna chombo cha umma kinatoa huduma kama hiyo. Alianza na huduma za benki - ondoeni fadha za taasisi za serikali kwenye benki binafsi.

Kwa mfano, kitendo cha kuifufua Nasaco kwa jina jipya na kuua mawakala binafsi wa clearing and forwarding, utasema nazo ni siasa?

Unapoongelea utalaamu na siasa angalia pande zote mbili, kwa kuwa serikali yako ya sasa ndio inaongoza kufanya mambo kisiasa badala ya kitaalamu. Hapo wala hata sijataja Chato International Airport
Whatever the reason lakini hapo kwenye kufufua mashirika ya umma namuunga mkono, Tanzania kitu ambacho kipo kwa watu wachache kama nyinyi ni siasa na ufinyu wa kufikiri

Kwani ATCL haijaajiri watanzania? Kwenu mnaona fahari sana kutetea company ya kigeni kuliko shirika la umma ambalo faida yake yote inaishia hapa Tanzania kwa akili zenu eti mnafikiri ndio kuikomoa ccm poor you
 
Hatari kubwa kama hizi ndio husababisha MARUBANI kulipwa mishahara mikubwaa na insurance huwa kubwaa, yote sbb wanafanya kazi ambazo ni za akili sana na inahitaji kipaji pia, ila zaidi risks ni kubwaaa.. Hivyo ndio sbb dunia nzima pilots are highly paid.

' Dalasa la saba' Joseph Msukuma kwa Mwezi anakula Mzigo Mkubwa Kuliko Rubani wa Air Tanzania
 
Watanzania huwa tunapenda sana kudharau taaluma za watu. Taaluma ambazo zinatokew jasho mashuleni na vyuoni pamoja na kupitia uzoefu wa kikazi.

Fastjet walipozuiliwa wasirushe ndege zao watanzania tukaongea mengi sana tukiyahusisha na siasa. Kampuni haikuwa na mtaalam ambaye anapaswa kufanya kazi na mamlaka ya anga TCAA. Mtaalam ambaye anapaswa kuihakikishia mamlaka juu ya usalama wa ndege.

Zikaingia siasa za eti lengo ni kuiwezesha ATCL na ndege zake liweze kushamiri kibiashara. Watu wakasahau kabisa kuwa ndege za Fastjet zilikuwa zinahatarisha maisha ya abiria, kwani zilikuwa ni spana mkononi.

Mamlaka ya anga kama mdhibiti mkuu wa sekta nzima ya anga, haikutaka kuhatarisha uhai wa nguvu kazi ya nchi hii.

Leo hii kampuni ya Boeing imeingia matatani baada ya ndege mbili aina ya 737 kuanguka katika kipindi kifupi. Mamlaka ya anga ya China imezizua ndege za aina hiyo zisiruke katika anga la nchi hiyo.

Weledi huwa na faida kubwa unapoheshimiwa na kupewa uhuru wa kufanya kazi, kinyume cha hapo ni muendelezo wa ajali nyingi huku tukimsingizia Mungu kwamba ni mipango yake.

Yaani Mungu huyo huyo anayeombwa ili maisha ya wagonjwa yapone, awe ni wa kuridhia vifo ambavyo vinaweza kuzuilika!.

Watanzania lipo somo zuri kwetu kupitia namna ambavyo jamii ya kimataifa inavyoliweka katika wakati mgumu kampuni ya Boeing. Sio kila kitu kitazamwe kisiasa, kuna suala la kuheshimu taaluma na weledi wa watu.

Am sorry but what you wrote here is full idiotic bullshit. Ni wapi na lini ilisemwa kuwa sababu ya kuwafungia leseni Fastjet ilikuwa ni safety issues? Kulikuwa na Boeing ngapi kwenye fleet ya Fastjet? Na kama ndege za Boeing zina matatizo, hiyo dreamliner anayoringia jiwe ni aina gani, Cessna?
 
Jamaa yangu PHILLIPO kama wewe ni msomi na sio mtu anayeweka siasa mbele, ni vyema ukafikiri kwa kina na kujaribu kujadili mambo mbalimbali ukiwa na mtazamo huru tofauti na hapo unaweza kudharaulika na kushusha heshima yako.

Nimejaribu kuandika mambo mengi yanayohitaji akili ya kawaida ya darasa la saba kuyafikiri lakini nimefuta, JARIBU KUFIKIRI MKUU PASIPO KUFIKIRI KISIASA TUIJENGE NCHI NA TUACHE PROPAGANDA ZA KITOTO.
 
Acha porojo hizi ndege Fastjet hawana, wana boeing 737 lakini sio MAX!
Nilichomuelewa mleta uzi kasema serikali ilipozuia fastjet isifanye biashara hadi kuna baadhi ya mambo fulani fulani warekebishe kwa ajili ya usalama wa abiria,baadhi ya watu hapa JF waliona serikali inawafanyia roho mbaya fastjet ili labda ATCL wanataka kuhodhi(monopoly)biashara ya anga pekee yao.

Mwisho mleta UZI amesisitiza maamuzi kama hayo waliotoa wataalamu wa mamlaka ya anga kwa fastjet ili warekebishe baadhi ya mambo kulinda usalama wa abiria lengo kuepuka ajali kama hiyo ya Ethiopian airline.

Pia kasema tuache wataalamu wafanye kazi zao kuliko kuingiza siasa kama tulivyokuwa tunadhani serikali inaleta ukiritimba(monopoly) dhidi ya fastjet.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jamaa nimemshangaa sana serikali ilitoa sababu zake (za kipuuzi) hii ya spana mkononi haikuwepo jama sijui kaitoa wapi? alafu anaongea kwa sauti kubwa kumbe ujinga mtupu.
Hiyo ni hali ya kujipendekeza mkuu.

Kama mamlaka imetoa sababu na sio hizi anazotaka kuaminisha watu, tujiulize hizi zake yeye kazitoa wapi?

Basi tu ili aonekane anaitetea serikali.
 
Watanzania huwa tunapenda sana kudharau taaluma za watu. Taaluma ambazo zinatokew jasho mashuleni na vyuoni pamoja na kupitia uzoefu wa kikazi.

Fastjet walipozuiliwa wasirushe ndege zao watanzania tukaongea mengi sana tukiyahusisha na siasa. Kampuni haikuwa na mtaalam ambaye anapaswa kufanya kazi na mamlaka ya anga TCAA. Mtaalam ambaye anapaswa kuihakikishia mamlaka juu ya usalama wa ndege.

Zikaingia siasa za eti lengo ni kuiwezesha ATCL na ndege zake liweze kushamiri kibiashara. Watu wakasahau kabisa kuwa ndege za Fastjet zilikuwa zinahatarisha maisha ya abiria, kwani zilikuwa ni spana mkononi.

Mamlaka ya anga kama mdhibiti mkuu wa sekta nzima ya anga, haikutaka kuhatarisha uhai wa nguvu kazi ya nchi hii.

Leo hii kampuni ya Boeing imeingia matatani baada ya ndege mbili aina ya 737 kuanguka katika kipindi kifupi. Mamlaka ya anga ya China imezizua ndege za aina hiyo zisiruke katika anga la nchi hiyo.

Weledi huwa na faida kubwa unapoheshimiwa na kupewa uhuru wa kufanya kazi, kinyume cha hapo ni muendelezo wa ajali nyingi huku tukimsingizia Mungu kwamba ni mipango yake.

Yaani Mungu huyo huyo anayeombwa ili maisha ya wagonjwa yapone, awe ni wa kuridhia vifo ambavyo vinaweza kuzuilika!.

Watanzania lipo somo zuri kwetu kupitia namna ambavyo jamii ya kimataifa inavyoliweka katika wakati mgumu kampuni ya Boeing. Sio kila kitu kitazamwe kisiasa, kuna suala la kuheshimu taaluma na weledi wa watu.
Mkuu usipotoshe hili la kuzuia fastjet,Serikali yako ilianza kudeal na fastjet kuwaletea mizengwe kwa kuwaambia hamna sheria za low coast airline Tanzania ,Waendeshe biashara kijima kama ATC kitu ambacho wazungu wakaona upuuzi,Aliyeleta ndege mbovu ni Masha baada ya kumwachia brand name ya kampuni isitoshe SOPs za fastjet baba zilikuwa juu sana,Ndiyo maana viongozi wenu fastjet walikuwa wanaheshimu muda,Sasa rubani TC anachelewesha ndege ili kumsubiri Waziri,
Nakumbuka kisa kimoja Kilimanjaro Gambo alikuwa VIP sisi wote Abiria tuko ndani ya ndege yeye anajivuta, akaja na mizigo mingi ambayo haiwezi kufiti juu wala chini ya kiti kupeleka Cargo hold hataki, anamdindia bwanamdogo crew,Crew akareport kwa rubani na Captain alikuwa mzungu akamuuliza are you going or not,alichojibu gambo ni kumwambia mzungu,Iam regional Commission.
Yule mzungu akamwambia congratulation but safety is our priority jamaa akanywea.
 
Nimeelezea zaidi suala la kukwepa ushauri wa wataalamu sijawa specific kwenye suala la Fastjet.
Sidhan kama kuna sentesi hata moja nmegusia suala la Fastjet au Boeing.
Kama mtoa mada amepotosha ni yeye ila mi nimejikita kwenye dhana ya kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalamu pia kusingizia siasa kila serikali inapochukua hatua.
Huenda ni hoja nzuri ila siyo mahali pake!
 
Whatever the reason lakini hapo kwenye kufufua mashirika ya umma namuunga mkono, Tanzania kitu ambacho kipo kwa watu wachache kama nyinyi ni siasa na ufinyu wa kufikiri

Kwani ATCL haijaajiri watanzania? Kwenu mnaona fahari sana kutetea company ya kigeni kuliko shirika la umma ambalo faida yake yote inaishia hapa Tanzania kwa akili zenu eti mnafikiri ndio kuikomoa ccm poor you
Ni watu wasio na uwezo wa kufikiri kama wee ambao hufanya kazi kwa hulka. Mashirika ya umma yalikuwapo, yakafa. Sasa niambie, leo unapoyafufua, ni kitu gani tofauti kipo leo kitafanya yafanikiwe kuliko huko nyuma? Ikiwa umepata jibu hilo basi ni vema. Lakini kukurupuka bila kujibu hayo maswali, ukidhani kwamba suluhisho ni kuweka wine ya zamani kwenye chupa mpya, unajidanganya.

Na jambo unalopaswa kujua ni kwamba, Magufuli atakuwa raisi kwa miaka kumi, na mashirika anayofufua yataendelea kuwapo baada ya Magufuli kuondoka. Kwa hiyo, ni kitu gani kitakachofanya yawe sustainable beyond Magufuli leadership era ya kufanya kazi kwa kumwogopa Magufuli? Au tunayafufua ili yaje kubinafsishwa tena baada ya Magufuli kuondoka? BRT na upya wake inawashinda kuendesha kama taasisi ya umma, na ipo Dar es Salaam tu, njia sana sana moja.

Acheni kufanya mambo kwa kukurupuka, wewe, Magufuli na wengineo. Haya mambo yanahitaji tafakuri ya kutosha sio kufanya kwa mihemuko ya uzalendo uchwara
 
Hatari kubwa kama hizi ndio husababisha MARUBANI kulipwa mishahara mikubwaa na insurance huwa kubwaa, yote sbb wanafanya kazi ambazo ni za akili sana na inahitaji kipaji pia, ila zaidi risks ni kubwaaa.. Hivyo ndio sbb dunia nzima pilots are highly paid.

HAIHITAJI AKILI NYINGI KUWA RUBANI BALI INAHITAJI HELA NYINGI KUWA RUBANI.
 
Kuna msemo mmoja unasema usiingize siasa kwenye mambo ya kitaalamu. Watanzania tuna tabia ya kukwepa ushauri wa kitaalamu na sheria inapotubana tunajikinga kwenye mwavuli wa siasa.

Mfano utakuta mtu kajenga chini ya nguzo za umeme mkubwa akiondolewa anadai kaondolewa kwa kua ni wa chama tofauti kumbe ni katika harakati za kumhakikishia usalama.

Wakati wa mafuriko watu wa Dar hua wanapewa tahadhari wakiondolewa kwa nguvu wanadai serikali ya kidikteta lakini mafuriko yakija wanaomba msaada wanasahau kama walipewa onyo.

Ifikie mahali tuheshimu wataalam wetu ingawa kuna wakati makatazo yao yanaingilia maslahi ya biashara au shughuli zetu.

Mkuu ulitaka kuandika nini labda, kuhusiana na topic iliyopo mezani vs ajali ya Ethiopia Airline?
 
Watanzania huwa tunapenda sana kudharau taaluma za watu. Taaluma ambazo zinatokew jasho mashuleni na vyuoni pamoja na kupitia uzoefu wa kikazi.

Fastjet walipozuiliwa wasirushe ndege zao watanzania tukaongea mengi sana tukiyahusisha na siasa. Kampuni haikuwa na mtaalam ambaye anapaswa kufanya kazi na mamlaka ya anga TCAA. Mtaalam ambaye anapaswa kuihakikishia mamlaka juu ya usalama wa ndege.

Zikaingia siasa za eti lengo ni kuiwezesha ATCL na ndege zake liweze kushamiri kibiashara. Watu wakasahau kabisa kuwa ndege za Fastjet zilikuwa zinahatarisha maisha ya abiria, kwani zilikuwa ni spana mkononi.

Mamlaka ya anga kama mdhibiti mkuu wa sekta nzima ya anga, haikutaka kuhatarisha uhai wa nguvu kazi ya nchi hii.

Leo hii kampuni ya Boeing imeingia matatani baada ya ndege mbili aina ya 737 kuanguka katika kipindi kifupi. Mamlaka ya anga ya China imezizua ndege za aina hiyo zisiruke katika anga la nchi hiyo.

Weledi huwa na faida kubwa unapoheshimiwa na kupewa uhuru wa kufanya kazi, kinyume cha hapo ni muendelezo wa ajali nyingi huku tukimsingizia Mungu kwamba ni mipango yake.

Yaani Mungu huyo huyo anayeombwa ili maisha ya wagonjwa yapone, awe ni wa kuridhia vifo ambavyo vinaweza kuzuilika!.

Watanzania lipo somo zuri kwetu kupitia namna ambavyo jamii ya kimataifa inavyoliweka katika wakati mgumu kampuni ya Boeing. Sio kila kitu kitazamwe kisiasa, kuna suala la kuheshimu taaluma na weledi wa watu.
Hujui kitu
 
Kama unafikiri serikali haikuwa na lengo la kuiua Fastjet ili kuiwezesha Air Tanzania basi wewe ni mtu wa kuhurumiwa sana, hujui serikali ya awamu ya tano inavyofanya kazi.

Kimsingi, Magufuli hapendelei sana suala na private sector, hasa pale ambapo kuna chombo cha umma kinatoa huduma kama hiyo. Alianza na huduma za benki - ondoeni fedha za taasisi za serikali kwenye benki binafsi.

Kwa mfano, kitendo cha kuifufua Nasaco kwa jina jipya na kuua mawakala binafsi wa clearing and forwarding, utasema nazo ni siasa?

Unapoongelea utalaamu na siasa angalia pande zote mbili, kwa kuwa serikali yako ya sasa ndio inaongoza kufanya mambo kisiasa badala ya kitaalamu. Hapo wala hata sijataja Chato International Airport

Tumekusikia tumekuelewa, haya njoo utuambie na haya mabasi y amwendombio au kwa maana nyingine wa njia maalum nayo ni nini kimetokea wanajazwa kama mkaa kutoka kilwa kivinje kwenye gunia la manila
 
Whatever the reason lakini hapo kwenye kufufua mashirika ya umma namuunga mkono, Tanzania kitu ambacho kipo kwa watu wachache kama nyinyi ni siasa na ufinyu wa kufikiri

Kwani ATCL haijaajiri watanzania? Kwenu mnaona fahari sana kutetea company ya kigeni kuliko shirika la umma ambalo faida yake yote inaishia hapa Tanzania kwa akili zenu eti mnafikiri ndio kuikomoa ccm poor you
Acha kuandika uharo hapa..

Haya Mashirika ya umma si yalikuwepo huko nyuma, umejiuliza ni kitu gani kilichoyauwa ambacho hakitaweza kuyauwa sasa hivi yanapofufuliwa??Je zile sababu zilizosababisha yakafa huko nyuma hazipo tena?

Lingine usiseme Watanzania tunapenda kutetea Makampuni ya Kigeni, hakuna kitu kama hicho. Watu siku zote (mtanzania au yeyote yule) anataka huduma bora..na huduma bora inakuwepo hasa pale kunapokuwa na ushindani katika huduma husika..

Tatizo lipo palepale jamaa haipendi kabisa sekta binafsi, sijui anafikiri atainyanyua Nchi kwa public sector peke yake..KICHAA.
 
Back
Top Bottom