Utaalam uheshimiwe, ilipozuiliwa Fastjet watu wakaleta siasa. Boeing wanakiona cha moto

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Watanzania huwa tunapenda sana kudharau taaluma za watu. Taaluma ambazo zinatokew jasho mashuleni na vyuoni pamoja na kupitia uzoefu wa kikazi.

Fastjet walipozuiliwa wasirushe ndege zao watanzania tukaongea mengi sana tukiyahusisha na siasa. Kampuni haikuwa na mtaalam ambaye anapaswa kufanya kazi na mamlaka ya anga TCAA. Mtaalam ambaye anapaswa kuihakikishia mamlaka juu ya usalama wa ndege.

Zikaingia siasa za eti lengo ni kuiwezesha ATCL na ndege zake liweze kushamiri kibiashara. Watu wakasahau kabisa kuwa ndege za Fastjet zilikuwa zinahatarisha maisha ya abiria, kwani zilikuwa ni spana mkononi.

Mamlaka ya anga kama mdhibiti mkuu wa sekta nzima ya anga, haikutaka kuhatarisha uhai wa nguvu kazi ya nchi hii.

Leo hii kampuni ya Boeing imeingia matatani baada ya ndege mbili aina ya 737 kuanguka katika kipindi kifupi. Mamlaka ya anga ya China imezizua ndege za aina hiyo zisiruke katika anga la nchi hiyo.

Weledi huwa na faida kubwa unapoheshimiwa na kupewa uhuru wa kufanya kazi, kinyume cha hapo ni muendelezo wa ajali nyingi huku tukimsingizia Mungu kwamba ni mipango yake.

Yaani Mungu huyo huyo anayeombwa ili maisha ya wagonjwa yapone, awe ni wa kuridhia vifo ambavyo vinaweza kuzuilika!.

Watanzania lipo somo zuri kwetu kupitia namna ambavyo jamii ya kimataifa inavyoliweka katika wakati mgumu kampuni ya Boeing. Sio kila kitu kitazamwe kisiasa, kuna suala la kuheshimu taaluma na weledi wa watu.
 
Kama unafikiri serikali haikuwa na lengo la kuiua Fastjet ili kuiwezesha Air Tanzania basi wewe ni mtu wa kuhurumiwa sana, hujui serikali ya awamu ya tano inavyofanya kazi.

Kimsingi, Magufuli hapendelei sana suala na private sector, hasa pale ambapo kuna chombo cha umma kinatoa huduma kama hiyo. Alianza na huduma za benki - ondoeni fedha za taasisi za serikali kwenye benki binafsi.

Kwa mfano, kitendo cha kuifufua Nasaco kwa jina jipya na kuua mawakala binafsi wa clearing and forwarding, utasema nazo ni siasa?

Unapoongelea utalaamu na siasa angalia pande zote mbili, kwa kuwa serikali yako ya sasa ndio inaongoza kufanya mambo kisiasa badala ya kitaalamu. Hapo wala hata sijataja Chato International Airport
 
Hizo ndege mbili ni mpya na kampuni ya Boeing ni kampuni kubwa sana duniani huwezi kuueleza ulimwengu kuwa Tanzania ina wataalamu wajuzi kuliko wa Boeing; Pia hakuna uhusiano wowote na matatizo ya Fastjet.

Kabla ya kuandika tafakari unachotaka kukiandika.
 
Hatari kubwa kama hizi ndio husababisha MARUBANI kulipwa mishahara mikubwaa na insurance huwa kubwaa, yote sbb wanafanya kazi ambazo ni za akili sana na inahitaji kipaji pia, ila zaidi risks ni kubwaaa.. Hivyo ndio sbb dunia nzima pilots are highly paid.
 
Kuna msemo mmoja unasema usiingize siasa kwenye mambo ya kitaalamu. Watanzania tuna tabia ya kukwepa ushauri wa kitaalamu na sheria inapotubana tunajikinga kwenye mwavuli wa siasa.

Mfano utakuta mtu kajenga chini ya nguzo za umeme mkubwa akiondolewa anadai kaondolewa kwa kua ni wa chama tofauti kumbe ni katika harakati za kumhakikishia usalama.

Wakati wa mafuriko watu wa Dar hua wanapewa tahadhari wakiondolewa kwa nguvu wanadai serikali ya kidikteta lakini mafuriko yakija wanaomba msaada wanasahau kama walipewa onyo.

Ifikie mahali tuheshimu wataalam wetu ingawa kuna wakati makatazo yao yanaingilia maslahi ya biashara au shughuli zetu.
 
Sijakuelewa. Yaani ATCL imekosa mtaalam ndo maana wakasimamisha ndege yao pendwa?? Acha kutupeleka China wakati tuna yetu hapa home. Wadhani China kupiga hiyo marufuku basi tena watu hatutaenda china kwa ndege?? Fikiri kidogo kabla hujaleta bla bla hapa jf
 
Basi sawa baba...na yule aliyeweka depot ya mabasi ya mwendo wa mbio naye ahakikishiwe usalama
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Watanzania huwa tunapenda sana kudharau taaluma za watu. Taaluma ambazo zinatokew jasho mashuleni na vyuoni pamoja na kupitia uzoefu wa kikazi.

Fastjet walipozuiliwa wasirushe ndege zao watanzania tukaongea mengi sana tukiyahusisha na siasa. Kampuni haikuwa na mtaalam ambaye anapaswa kufanya kazi na mamlaka ya anga TCAA. Mtaalam ambaye anapaswa kuihakikishia mamlaka juu ya usalama wa ndege.

Zikaingia siasa za eti lengo ni kuiwezesha ATCL na ndege zake liweze kushamiri kibiashara. Watu wakasahau kabisa kuwa ndege za Fastjet zilikuwa zinahatarisha maisha ya abiria, kwani zilikuwa ni spana mkononi.

Mamlaka ya anga kama mdhibiti mkuu wa sekta nzima ya anga, haikutaka kuhatarisha uhai wa nguvu kazi ya nchi hii.

Leo hii kampuni ya Boeing imeingia matatani baada ya ndege mbili aina ya 737 kuanguka katika kipindi kifupi. Mamlaka ya anga ya China imezizua ndege za aina hiyo zisiruke katika anga la nchi hiyo.

Weledi huwa na faida kubwa unapoheshimiwa na kupewa uhuru wa kufanya kazi, kinyume cha hapo ni muendelezo wa ajali nyingi huku tukimsingizia Mungu kwamba ni mipango yake.

Yaani Mungu huyo huyo anayeombwa ili maisha ya wagonjwa yapone, awe ni wa kuridhia vifo ambavyo vinaweza kuzuilika!.

Watanzania lipo somo zuri kwetu kupitia namna ambavyo jamii ya kimataifa inavyoliweka katika wakati mgumu kampuni ya Boeing. Sio kila kitu kitazamwe kisiasa, kuna suala la kuheshimu taaluma na weledi wa watu.
kwahiya hizi Boeing za kwetu nazo zizilielwe tu.
 
Kuna msemo mmoja unasema usiingize siasa kwenye mambo ya kitaalamu. Watanzania tuna tabia ya kukwepa ushauri wa kitaalamu na sheria inapotubana tunajikinga kwenye mwavuli wa siasa.
Mfano utakuta mtu kajenga chini ya nguzo za umeme mkubwa akiondolewa anadai kaondolewa kwa kua ni wa chama tofauti kumbe ni katika harakati za kumhakikishia usalama.
Wakati wa mafuriko watu wa Dar hua wanapewa tahadhari wakiondolewa kwa nguvu wanadai serikali ya kidikteta lakini mafuriko yakija wanaomba msaada wanasahau kama walipewa onyo.
Ifikie mahali tuheshimu wataalam wetu ingawa kuna wakati makatazo yao yanaingilia maslahi ya biashara au shughuli zetu.
Hauelewi lililotokea na unachochangia, mleta hoja kaleta vitu visivyofanana. Ni ujinga kusema Tanzania ina wataalamu kuliko wa Boeing pamoja na Ethiopian Airlines! Labda anadhani nao huenda uwanjani kupokea ndege mpya! Hajui hata idadi ya ndege walizonazo na za viwango gani, pia kampuni inashika nafasi ya ngapi Afrika na iliazishwa mwaka gani.
 
Nimeelezea zaidi suala la kukwepa ushauri wa wataalamu sijawa specific kwenye suala la Fastjet.
Sidhan kama kuna sentesi hata moja nmegusia suala la Fastjet au Boeing.
Kama mtoa mada amepotosha ni yeye ila mi nimejikita kwenye dhana ya kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalamu pia kusingizia siasa kila serikali inapochukua hatua.
 
Ethiopia na China wamesimamisha matumizi ya Boeing 737 kwa sababu ya kupata pata ajali miezi mitano iliyopita ilipata ajali ndege ya Indonesia nayo ilikua 737 kwa hiyo hayo mashirika mawili makubwa ya usafirishaji wanataka majibu ya kina kuhusu hizo ndege kutoka kampuni ya Boeing ya Marekani...fasjet walisimamishwa ilikua hujuma ili wao wafanye biashara na ndege zao walizoagiza...
 
Sijakuelewa. Yaani ATCL imekosa mtaalam ndo maana wakasimamisha ndege yao pendwa?? Acha kutupeleka China wakati tuna yetu hapa home. Wadhani China kupiga hiyo marufuku basi tena watu hatutaenda china kwa ndege?? Fikiri kidogo kabla hujaleta bla bla hapa jf
Fastjet kasema ya Masha ndio spana mkononi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom