Uswazi ukiiba simu unachezea maisha yako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uswazi ukiiba simu unachezea maisha yako!

Discussion in 'Jamii Photos' started by masopakyindi, Sep 29, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Jamaa inaelekea analalamika "Yaani nimeiba blakiberi tu ndo mnataka kunichoma ka mshikaki!"
  Tuache tabia hii wajameni.
   
 2. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wizi mbaya sana jamani. lakini hali ya maisha nayo ni ngumu. hao mafisadi wanaoiba mabilioni nao wanapaswa kupata adhabu pengine kubwa kuliko hii. Hali ya maisha Tanzania inasikitisha sana.
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Da jamani, hawa vibaka maisha hatarini kabisa. Social problems emanating from poverty.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  imagine mtoto wako ndo anachomwa hivyo...imagine kama tungekuwa tunatenda dhambu palepale Mungu anakamata anatuchoma hivo nani angebaki? kama Mungu angehesabu maovu, nani angesimama?....nimeibiwa sanaa nimeumizwa sana na wezi, lakini kitendo icho siwezi kufanya. kuna kipindi miaka ile ya zamani nilikuwa nimepigikaaa,maisha magumu nikawa na vibiashara vyangu, walikuwa kukwangua kila kitu hadi cable za umeme yaani wakachukua hadi carpet....lakini bado tu kitendo icho hapo kwenye picha sikukubali....mbona kuna Mengi tu Mungu kanisamehe mimi kwanini niue kwasababu ya mtu kanikosea, kama Mungu angeniua mimi nikifanya kosa hata leo hii nisingekuwepo kwasababu nimefanya makosa mengi mno mbele zake.
   
 5. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na wachawi nao wangechomwa ningesapoti lakini hao hapana ni ukatili aisee.
   
 6. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Jamani tuwe na ubinadamu kidogo maana sasa hata wanyama wanatushinda.Tupunguze ubinafsi na tumwone kila mtu ana haki sawa mbele ya muumba wake
   
Loading...