Uswahilini kuna vituko!!!

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
351
Kiongozi wa soka atoa mpya

By Adam Fungamwango, Kinondoni


Kiongozi mmoja wa timu ya Maskani Fresh ya Kawe, aliyejulikana kwa jina moja la Charles, ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kuingia uwanjani wakati timu yake inacheza na kwenda kumzuia mchezaji wa timu pinzani aliyekuwa anakwenda kufunga goli.

Tukio hilo limetokea kwenye uwanja wa CCM Msasani wakati wa mechi ya Ligi ya TFF Kinondoni kati ya Maskani Fresh na Kambarage ambapo Kambarage ilishinda kwa bao 1-0.

Kituko hicho cha aina yake kilitokea katika dakika ya 87, ambapo kiongozi huyo baada ya kuona timu yake imezidiwa na mchezaji wa Kambarage wamewapiga chenga mabeki wake akiwemo kipa, aliingia uwanjani ghafla kwenda kumzuia mshambuliaji huyo asiweke mpira ndani ya nyavu, lakini burudani ya aina yake ilitoka pale na yeye alipopigwa chenga na mpira kukwamishwa ndani ya nyavu.

Kufungwa kwa bao hilo kulimfanya kiongozi huyo kumpiga mfungaji huyo na kuibua vurugu kubwa na kupelekea mwamuzi wa mchezo huo, Klina Kabala kuvunja pambano na kuzua zogo kubwa zaidi.

Kitendo hicho lilisabaisha fujo kubwa kutokea uwanjani napo na pambano kuvunjika na tayari chama cha soka Kinondoni KIFA, kimemfungia kiongozi huyo kutoongoza soka kwa muda wa miezi mitatu.

Katika barua yake yenye kumbukumbu namba KIFA/GF/VOL-V/437/2007 iliyosainiwa na katibu mkuu Frank Mchaki, imesema kuwa baada ya tukio hilo iliwaita waamuzi na kuhoji undani wa suala hilo lililotia doa soka la Kinondoni, walieleza hali ilivyokuwa, lakini kiongozi huyo wa Maskani hakutokea kwenye kikao.

Mbali na kumfungia kucheza soka, pia imemtoza faini ya sh 500,000 kiongozi huyo na pia Maskani imepoteza mchezo huo kutokana na kitendo alichofanya.

KIFA imeonya vikali vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa kwenye baadhi ya michezo ya Ligi hiyo na kusema kuwa itachukua hatua kali kwa wahusika.

SOURCE: Alasiri
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom