Usuluhisho wa migogoro ya ndoa bora wapi, Baraza la Kata au Dawati la Jinsia?

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,057
Katika pitapita zangu kwenye idara, vyombo au taasisi zenye dhamana ya upatanisho wa migogoro ya wana ndoa, kwa tathimini ya haraka haraka na baadhi ya shuhuda kama Tano (5), nimejiridhisha pasi na shaka wala tashwishi yoyote ya kwamba Bora uwe na mke ukiwa na ugomvi nae aende kushtaki Baraza la Kata kuliko Dawati la Jinsia.

Dawati la Jinsia lililo chini ya Idara ya polisi ni mitumbwi ya vibwengo hawa viumbe ni mcharuko wamekasimiwa majukumu ambayo hawaya wezi.

Hawajui fair judgement, kesi nyingi toka day one wana mtu wao, mshitaki ndio mwenye haki, na wakipewa visenti ndio usipime, wakiwa na urafiki na mgoni, mgomvi, mshitaki wako ndio utajuta, mkeo/mshitaki/mgomvi akiwa na kauzuri fulani au ni Utopolo fulani kichwani wanapita nae mapema sana. na siku ya kupita nao wanaweka mazingira ulale lock up, hawa mende hawa.

Nimeshuhudia ndoa 5 hazijapata msaada Dawati la Jinsia, hata kusimamia utekelezaji wa ahadi za kutunza watoto Kwa walio achana au kutengana Dawati la Jinsia ni Utopolo mtupu umejazana pale, ukiwa na umate mate umepiga Ndoige hamna agenda.

Kinyume kabisa na ufanisi wa Baraza la Kata wako vizuri sana unaona maturity, usikivu, usawa, yaani hawa wanajua kazi yao na dhamana walizopewa.

Kwa visa hivyo vitano ndoa.

Sasa basi, nakazia, mtaoa wenyewe mnaopanda mitumbwi ya vibwengo sisi mabaharia mtuache tutaishi na mademu zetu kigheto ghetto tu.
Poleni sana wanandoa mnaopelekana Dawati la Jinsia

Katika hizo ndoa 5 wake watatu 3 washaliwa na jamaa wa Dawati na wawili jamaa wameona chats zenye tashtiti na hao vibwengo.

Mary at ur own risk

Nice Sunday.......

Wadiz nimeungama.
 
Katika Vitu vinapoteza Muda na pia hakuna Maamuzi ni Baraza la Kata na Bakwata sijui kwanini Serikali hivi Vitu hawavifuti.
 
Migogoro ya ndoa inatakiwa isuluhishwe kule mlipofungia ndoa (mlipounganishwa), iwe kanisani au msikitini; huko kwingine mnawapa majukumu yasiyokuwa ya lazima.​
 
Yote ni ya muhimu maana yapo kwa mujibu wa sheria ya nchi. Soma uzi huu ujue sheria ya mtoto .
 
Back
Top Bottom