Usultani wa Maalim na usaliti wa Membe na Lissu

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
Mara paap jioni imefika nakutana na picha za maigizo ambazo naona watu wanajidanganya kwamba eti kupitia picha hizo wanaweza kuongoza nchi ikanibidi nicheke kidogo kisha nikashushia na glasi yangu ya wine isiyo na kilevi, kisha nikajiuliza hivi huyu Sultan Maalim Seif, Msaliti Membe na Mtumishi wa Mabeberu Tundu Lissu wanatuchukuliaje Watanzania.

Sultan Seif na Genge la Msaliti Membe na Lissu wakishauriwa na Zitto Kabwe na Mbowe wanawachukulia Watanzania kama mazezeta wanaamini wanaweza kuwapelekesha watakavyo, Niwaambie ndugu zangu hawa watu hasa Sultan Seif na Msaliti Membe na Lissu hawana sifa za kuongoza hata Ng'ombe wa Mchungaji, kwa sababu watawaingiza kwenye migogoro ya wazi na wanyama hao wataishia kupigana na kuuwana.

Hawa watu ninavyowafahamu mimi Msaliti Membe na Sultan Maalim wanataka kuirudisha Tanzania kwenye ukoloni ishindwe kujiamulia mambo yake kama ilivyosasa Maalim amepewa hela za Kampeni na waarabu ili akishasinda Urais aiuze Zanzibar kwa waliompa hela na dalali aliyepanga bei Bernard Membe akitumia cheo chake cha zamani Uwazirti wa Mambo ya Nje, ndiyo maana Maalim kila Uchaguzi yeye ndiyo anagombea hakuna kiongozi mwingine anataka kuifanya Zanzibar kuwa na uongozi wa Kisultan kama waliompa hela za Kampeni, ila sasa aambiwe basi inatosha apishe wengine.

Msaliti Membe amewaahidi endapo na yeye watampa fedha ataiuza Tanzania kama alivyotaka kuiuza Mtwara na Lindi endapo tu atashinda Urais wa Tanzania kwajinsi ninavyomjua Membe hajawahi kuwa na mapenzi na Watanzania kama anavyojionesha sasa zaidi ya uroho wa madaraka kwa kuiuza nchi.

Sasa kilichopo kuna mgogoro mkubwa baina yao na Tundu Lissu nani atakuwa mgombea Urais kati ya Membe na Lissu kila mtu anatamaa ya madaraka na kinachomsumbua Lissu sasa ni kulipa fadhila Kwa Mabeberu ambao waliimpa Mabilioni ya Pesa, azunguke Dunia nzima kuichafua Tanzania halafu akawaahidi akifika Tanzania lazima alete ya machafuko ya kumwaga damu endapo hatapewa nafasi ya kugombea Urais au akishindwa kwenye kura.
 
esther mashiker,

Kwa kizazi cha sasa hizi mada zisizo na mbele wala nyuma siku hizi zinakosa mashiko!!
CCM tuwe na thinkers si watu waa aina ya Polepole!

Ukianza kushambulia characters nawe ujue si mkamilifu utakuta una mapungufu zaidi ya unao wakosoa kibinadamu.

Tunataka sera, sera, sera za mendeleo, acheni huu ujinga!
 
esther mashiker,

Tupe supporting documents za hayo mauzo ya Membe kwa mabeberu. Na kwa nini serikali ipo kimya kwa makosa makubwa kama hayo uunayodai Membe anataka kuuza nchi?

Kama nchi, tuna financial intelligence unit (FIU), mzigo mkubwa kama huo utapitishia wapi paka wao wasijue kwamba kuna pesa chafu imeiingia toka kwa mabeberu?
 
CHILDISH presentation. Unadhani watu wote ni wajinga? Unawajua vyema hao unaowasema au umekurupuka kutoka usingizini kwenye ndoto nzito?
 
Wandugu,
Siwadanganyi, ila niwaombe mfungue macho na akili zenu muone hali halisi ya mambo yanavyokwenda kwenye hii karne ya 21. Kwa hakika wakati umewaacha mno!
 
Ee bwana wewe upo dunia gani? Au unatoka chato? Watu wanataka mabadiliko, ccm mambo ya zamani hayo wewe vipi? Kijana mzima unashabikia ccm ya wauaji na walaji?
 
Back
Top Bottom