Usultani mpya ktk siasa za Tanzania

inawezekana

Member
Jul 17, 2009
29
3
Katika miaka ya karibuni, kumekuwa na hali ambayo watafiti wa mambo ya kisiasa wameyaita kama usultani katk sura mpya. Mifano halisi ipo Zanzibar ambapo marehemu rais Abeid Amani Karume alimrithisha mwanae madaraka, Amani Abeid Karume, ktk hali isiyoaminika bado ndugu yake rais wa sasa ZNZ yaani Amani Abeid Karume aitwaye Ali Karume yuko mbioni kuja kugombea kiti cha urais ZNZ???

Mtiririko huo pia tumeuona kule mjengoni wakati spika wa bunge letu tukufu Samwel Sitta, na mkewe Magreth Sitta wakiwa mjengoni (hii ni familia moja) bado Pius Msekwa spika aliyepita na mkewe Anna Abdallah wote walikuwa mjengoni pia.

Swali linakuja nani spika anayekuja na mkewe atakuwa na madaraka gani, STAY TUNED

Haya tuangalie hali ya kinyang'anyiro cha ubunge katika kisiwa cha Mafia, ambako mbunge aliyethubutu hata kukitaka kisiwa cha MAFIA kiwe nchi wakati wa utawala wake uliodumu kwa takribani miaka 25 duh!, mwanawe ambaye ni diwani wa Kijitonyama anaitwa Omari Kimbau, anayeimbwa na AKUDO anayetaka kuwania kiti cha ubunge wa jimbo la Mafia.

Hojaji za wasiasa zimethibitisha kuwa, Baba yake Omari, Kanali Omari Kimbau ni mtu aliyeifikisha mahali pabovu ambapo Mafia ipo sasa. Je hatuoni kuwa ni wakati muafaka Mafia ifikirie kuondoa usultani huu sasa??

Naomba kuwakilisha
 
Sio TZ tu. Marekani kuna George H.W. Bush na George H. Bush; Botswana kuna Sir Seretse Khama na Ian Khama; Togo kuna Eyadema na Eyadema mtoto; Gambia nako nasikia anakuja Bongo mtoto; DRC yuko J Kabila baada L Kabila baba kuuwawa! Orodha ni ndefu nisikuchoshe. Itoshe tu kusema kwamba Mwalimu hakuwa na malezi ya kutosha kwa wanae 7!
 
Sio TZ tu. Marekani kuna George H.W. Bush na George H. Bush; Botswana kuna Sir Seretse Khama na Ian Khama; Togo kuna Eyadema na Eyadema mtoto; Gambia nako nasikia anakuja Bongo mtoto; DRC yuko J Kabila baada L Kabila baba kuuwawa! Orodha ni ndefu nisikuchoshe. Itoshe tu kusema kwamba Mwalimu hakuwa na malezi ya kutosha kwa wanae 7!

Mifano uliyotoa haifanani na mada iliyoko. Ni kwamba jee kila mtoto wa mtawala anafaa kuwa mtawala??
 
Absolutely mkuu, nashukuru umenisoma tunachozungumzia hapa ni uroho wa madaraka bila kuangalia uwezo wa hao wanaofikiria kuchukua madaraka ambao wazee wao walikuwa nayo.

Ni wazi kuwa kwa vile wanafikiri hawana dili jingine ku-win maisha zaidi ya madaraka hasa ya kisiasa hasa kwa wale ambao shule iliwapiga chenga. Ni vema tukawachunguza kwa kina hawa wanaokuja kutaka uongozi, kwani kwa uhakika wakiwa viongozi wataaongoza kwa kutumia sera na mawazo ya waliowatangulia, "mwana wa nyoka ni nyoka" na "mtoto wa nyoka hafundishwi kuuma".

Kwa mfano huyo tunayemzungumzia Omari Kimbau, baba alikuwa mbunge kwa miaka 25 na mama ni mbunge hadi sasa na yeye pia. Ila hii yote ni kutokana na uroho wa madaraka bila kuangalia nini wataleta kwa wananchi, ni suala la wananchi kuangalia kwa upande mwengine kuwa wanafaa? au wanakuja kwa njaa zao tu?

Mafia kama kisiwa kilicho nyuma kimaendeleo ni wazi kinahitaji kiongozi makini, msomi mwenye uelewa na mtazamo chanya ili kuweza kusaidia kujenga miundo mbinu katika wilaya ya Mafia.
 
Jamani kwani sio sisi tunaowachagua watu hawa?..Ikiwa wewe mwananchi umepewa nafasi ya kumtazama mgombea kwa sifa ulizozitaka iweje leo kosa lilwe la mgombea wakati sisi tuna uwezo wa kutowapa kura zetu..

Ikiwa watu hawa wanashinda basi machoni mwa wapiga kura hawa jamaa wana sifa zote..Kisha basi sii kweli Marekemu Karume alimrithisha mwanaye na wala hawa viongozi wamewavuta wake na watoto wao ktk uongozi. Mh. Msekwa na mama Anna Abdallah wote hawa wamekutana ndani ya uwanja wa siasa hivyo sii dhambi wao kuoana.

Njia pekee ya kuwaondoa hawa vijana ni sisi wenyewe kujiandikisha upinzani dhidi yao. Nikiwa na maana kwamba ikiwa mtoto wa Kimbau anagombea Ubunge wa Mafia basi utatusaidia sana sisi wananchi ikiwa nawe utagombea Ubunge wa Mafia na kueleza machovu yote ya mtoto wa Kimbau kwa wananchi..Bila shaka tutakupa kura zetu, lakini hizi habari za kuomba dua misikitini na makanisani wakati hatuingii uwanjani haziwezi kutusaidia kitu.
 
Jamani kwani sio sisi tunaowachagua watu hawa?
Swadakta.
Na kama ni uroho wa madaraka, hata ambao hawana ndugu ambao ni viongozi wanaweza kuwa nao pia. Sidhani kama ni dhambi kwa mtoto wa kiongozi kuwania uongozi kama anazo zifa zote zinazomwezesha kushika wadhifa huo. haitapendeza tufike mahali kuwa mtoto wa kiongozi iwe ni sifa ya kukuondolea sifa za kuwania uongozi
 
Hojaji za wasiasa zimethibitisha kuwa, Baba yake Omari, Kanali Omari Kimbau ni mtu aliyeifikisha mahali pabovu ambapo Mafia ipo sasa. Je hatuoni kuwa ni wakati muafaka Mafia ifikirie kuondoa usultani huu sasa??

Naomba kuwakilisha

Baba yake Omari siku hizi anaitwa Omari na sio Ayoub/ Ayubu?
 
Sasa kama Kilangao na Malecela sii walionana na kupendana Bungeni? Msekwa na Anna..kila mmoja ana ana historiaa ya utendaji Tz mda mrefu!

Sasa mbona Hilary..ni Waziri wa Nje sasa na mme wake alikuwa raisi..je Hilary sii ana uwezo??

Basi wakati wa kuoana basi pia muangalie mwezi mwenye uwezo!

Uwezo kwanza..ndo mengine!

Mbegu ya ubaguzi sii nzuri!
 
Back
Top Bottom