nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Usultani unaujuwa au unausikia tu? cheki huu to start with:
Su huyo tu, na Mbowe na Baba'mkwe wake.
Balozi Kagasheki ni mbunge wa Bukoba mjini. Abubakari Kagasheki ni mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa
Wilaya ya Bukoba Mjini, jumuiya iliyoko chini ya CCM. Abdul Kagasheki anagombea awe Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa kutokea Bukoba Mjini. Suedi Kagasheki anagombea awe mjumbe wa kuwakilisha
Wilaya kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa tokea Bukoba Mjini. Katika hotuba yake kwa wajumbe
waliomchagua Abubakari Kagasheki, amesema na ninamnukuu, " Nawashukuru familia yangu kwa
kuniwezesha Kwa hali na mali katika uchaguzi huu. Kwa namna ya pekee niwashukuru Abdul Kagasheki na
Hamisi Kagasheki kwa kuniwezesha kwa hali na mali kushinda uchaguzi huu. Ndugu wajumbe, Familia
yetu inayo historia kubwa katika CCM kiasi kwamba Marehemu Baba wa Taifa akidai Uhuru alilala kwa
Baba yangu, na ndio maana hivi karibuni niliitwa Ikulu kwa ajili ya kupokea nishani iliyotolewa na
rais kwa ajiri ya baba yangu. Hivyo Familia yetu inaijua CCM zaidi ya yeyote katika wilaya
hii.Hivyo mtu wa FAMILIA YETU AKIGOMBEA TUTA HAKIKISHA ANAPITA KWA NJIA YOYOTE ILE" mwisho wa
kunukuu. Wanachama, wadau, na wakereketwa wa CCM Wilayani Hapa wamebaki na bumbuwazi na kujiuliza
HIVI SIASA ZA CCM BUKOBA MJINI KUHODHIWA NA FAMILIA MOJA, ni kwa ajili ya MASLAHI YA CHAMA,
WANACHAMA NA TAIFA AU NI ZA KUJINUFAISHA BINAFSI? NA JE, KWA VITISHO HIVI CHAMA BUKOBA MJINI KINA
ELEKEA WAPI?