Ustahimilivu wa kisiasa wa Freeman Mbowe

Khalidoun

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,834
4,463
834d6d59abd209b02c9bbe5daf422a25.jpg



Ni Tanzania pekee, mtu aliyetangazwa kuwa mtuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya, anaweza kukaribishwa jirani na viongozi wakubwa wa Serikali, wanapiga stori, wanacheka mpaka kugonganisha mikono.

Hapa Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, akiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Katika picha hizo, Mbowe anaonekana kwa ukaribu pia na Rais mstaafu, Dk Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, vilevile Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Picha hizi zimepigwa leo kwenye msiba wa mama mdogo wa Rais Kikwete, Nuru Khalfan Kikwete, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana kisha kuzikwa leo Bagamoyo.

KUMBUKA

Mbowe alituhumiwa mbele ya kadamnasi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa anahusika na biashara ya dawa za kulevya.

Makonda aliagiza Mbowe aripoti polisi kwa mahojiano. Baadaye Mbowe aliripoti polisi na kuachiwa. Mbowe pia alimfungulia mashitaka ya kikatiba Makonda kuwa maagizo aliyotoa yanakinzana na Katiba ya Tanzania.

MUUZA UNGA KWELI?

Duniani kote mtuhumiwa wa dawa za kulevya ni najisi, hata kama hakuna ushahidi wa kumtia hatiani, hutakiwa awe mbali na viongozi wa nchi maana anaweza kuwanajisi.

Kwa hiyo, Mbowe kupitia tuhuma za Makonda, hatakiwi kuwa karibu na viongozi wa nchi. Hakupaswa kuonekana karibu na Waziri Mkuu.

Hii nchi ina Usalama wa Taifa, maofisa wake ambao walikuwepo kwa wingi leo msibani, waliruhusi vipi Mbowe (mtuhumiwa wa dawa za kulevya) awe karibu na Waziri Mkuu pamoja na Rais Mstaafu?

Je, Usalama wa Taifa walishaziona tuhuma za Makonda ni famba? Kwa hiyo wanaona Mbowe ni mtu safi kuwa karibu na viongozi hao?

TAFSIRI YANGU

Tuhuma za Makonda kuhusu watuhumiwa wa dawa za kulevya haziingii akilini kwa Waziri Mkuu, Usalama wa Taifa, JK, Pinda na Membe ndiyo maana Mbowe leo alikuwa pamoja na viongozi msibani na kupewa heshima kama kiongozi.

Maana kama viongozi hao pamoja na Usalama wa Taifa, wangekuwa wanamchukulia Mbowe kama Makonda alivyomtangaza, leo asingepewa nafasi ya kiitifaki msibani. Zaidi asingeruhusiwa kumkaribia kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu.

Tafsiri ya jumla ni kuwa tuhuma za Makonda haziingii akilini kwa sehemu kubwa ya Serikali.

Makonda anapaswa kuwaomba radhi Watanzania na wote aliowatuhumu ambao imeshindikana hata kuwafungulia mashitaka.

Dawa za kulevya ni kesi nzito, anayetuhumiwa maana yake ni mtu hatari sana. Makonda hakupaswa kutumia vita ya dawa za kulevya kama jukwaa la kuongeza umaarufu.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Jibu litapatikana tu. Hata style yake ya kuwakamata inatia shaka kabisa. Kumpa arrest holiday muuza ngada! Unamtangaza hadharani kuwa ajilete mwenyewe baada ya siku 2 akiwa huru halafu unamwambia kuwa sasa katuoneshe kwako tukayatafute hayo madawa ulio nayo. Maajab gani hayo!! Aseme alikuwa na jambo lake sio ngada
 
834d6d59abd209b02c9bbe5daf422a25.jpg



Ni Tanzania pekee, mtu aliyetangazwa kuwa mtuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya, anaweza kukaribishwa jirani na viongozi wakubwa wa Serikali, wanapiga stori, wanacheka mpaka kugonganisha mikono.

Hapa Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, akiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Katika picha hizo, Mbowe anaonekana kwa ukaribu pia na Rais mstaafu, Dk Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, vilevile Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Picha hizi zimepigwa leo kwenye msiba wa mama mdogo wa Rais Kikwete, Nuru Khalfan Kikwete, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana kisha kuzikwa leo Bagamoyo.

KUMBUKA

Mbowe alituhumiwa mbele ya kadamnasi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa anahusika na biashara ya dawa za kulevya.

Makonda aliagiza Mbowe aripoti polisi kwa mahojiano. Baadaye Mbowe aliripoti polisi na kuachiwa. Mbowe pia alimfungulia mashitaka ya kikatiba Makonda kuwa maagizo aliyotoa yanakinzana na Katiba ya Tanzania.

MUUZA UNGA KWELI?

Duniani kote mtuhumiwa wa dawa za kulevya ni najisi, hata kama hakuna ushahidi wa kumtia hatiani, hutakiwa awe mbali na viongozi wa nchi maana anaweza kuwanajisi.

Kwa hiyo, Mbowe kupitia tuhuma za Makonda, hatakiwi kuwa karibu na viongozi wa nchi. Hakupaswa kuonekana karibu na Waziri Mkuu.

Hii nchi ina Usalama wa Taifa, maofisa wake ambao walikuwepo kwa wingi leo msibani, waliruhusi vipi Mbowe (mtuhumiwa wa dawa za kulevya) awe karibu na Waziri Mkuu pamoja na Rais Mstaafu?

Je, Usalama wa Taifa walishaziona tuhuma za Makonda ni famba? Kwa hiyo wanaona Mbowe ni mtu safi kuwa karibu na viongozi hao?

TAFSIRI YANGU

Tuhuma za Makonda kuhusu watuhumiwa wa dawa za kulevya haziingii akilini kwa Waziri Mkuu, Usalama wa Taifa, JK, Pinda na Membe ndiyo maana Mbowe leo alikuwa pamoja na viongozi msibani na kupewa heshima kama kiongozi.

Maana kama viongozi hao pamoja na Usalama wa Taifa, wangekuwa wanamchukulia Mbowe kama Makonda alivyomtangaza, leo asingepewa nafasi ya kiitifaki msibani. Zaidi asingeruhusiwa kumkaribia kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu.

Tafsiri ya jumla ni kuwa tuhuma za Makonda haziingii akilini kwa sehemu kubwa ya Serikali.

Makonda anapaswa kuwaomba radhi Watanzania na wote aliowatuhumu ambao imeshindikana hata kuwafungulia mashitaka.

Dawa za kulevya ni kesi nzito, anayetuhumiwa maana yake ni mtu hatari sana. Makonda hakupaswa kutumia vita ya dawa za kulevya kama jukwaa la kuongeza umaarufu.

Ndimi Luqman MALOTO
mbowe mtoto wa mjini huyu msukuma kaja mjini na makatambuga eti leo naye anahenyesha wajanja.

ngoja naye tutamyoosha arudo kwao chato akavue samaki kama yule mdogo wake aliyekimbia nchi kukwepa kesi ya jinai
 
Ebu acheni unafki...hiki ulichokiandika jaribu kukifananisha na yale ambayo CHADEMA waliyasema juu ya EDDO....then jiulize ni je WALIMSINGIZIA EDO?????au ni pesa za EDO ndizo ziliwanyamazisha CDM.....ukijibu hili ndio utaweza pata tafsiri
halisi ya picha za leo
 
Huyo ndio Freeman Aikael Mbowe, master wa siasa za bongoland. Huyu mtu anatakiwa apewe heshima kubwa kutokana na mchango wake kwa taifa hili.

Mbowe ni mwanasiasa bora kabisa wa upinzani kuwahi kutokea kwenye nchi hii.
Si kweli kabsa.....huyu mtu ana makndo kando mengi tu machafu......
 
Back
Top Bottom