Ustaarabu wa kujiuzulu na kuomba radhi utafika lini kwetu?

Fredinho

JF-Expert Member
May 18, 2016
971
1,137
Waingereza walipiga kura ya kujitoa umoja wa ulaya majuzi tu,waziri mkuu wao kaamua kujiuzulu kiungwana kabisa kisa?

kashindwa kuwashawishi raia wake wasijitoe katika umoja huo,kule Japani mwezi februari mbunge Kensuke Miyazaki alijiuzulu na kuomba radhi baada ya kugundulika kuwa alitoka kimapenzi na bibie mmoja wakati mkewe akiwa mjamzito.Ni jambo la kawaida kwa wenzetu kuomba radhi na kujiuzulu kiungwana kabisa wanapogundua hawakutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Kinachonishangaza huku kwetu Tanzania hata kiongozi afanye madhambi kiasi gani hawezi kuomba radhi wala nini na hata kujiuzulu ni mpaka afukuzwe,viongozi wote waliopatikana katika kashfa ya escrow kwa mfano badala ya kuomba radhi nakujiuzulu kistaarabu ndo kwanza walianza majigambo,

kiongozi mwingine kadakwa anajibu maswali akiwa amelewa kafukuzwa hata kuomba msamaha kwa wananchi wa jimbo lake tu kashindwa ndo kwanza kaenda kupumzika ughaibuni,nauliza wadau tatizo nini mbona hatujifunzi uungwana huu mzuri toka kwa wenzetu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom