Ustaarabu udumishwe viongozi wanapowasilisha hoja kwa watumishi wa umma

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Ukizingatia changamoto tulizo kuwa nazo ni vyema kuona kwamba tumevuka mwaka 2020 salama.

Kitu ambacho ningependa kujadili na wenzangu leo ni hali ambayo imekuwa ikijitokeza na kujumuisha viongozi serikalini kutumia njia ya ukali usio wa lazima na kwa vipindi vingine njia ya kuwa dhalilisha watumishi wa umma hadharani.

Haya ni maoni tu na kwa vyovyote vile ni vyema kupongeza serikali ya Magufuli kwa mema yaliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ya awali.

Nikijaribu kutafakari yanayoendelea, napata picha ya kiongozi wa juu sana aliyepewa nafasi ya kuongea mbele ya umati wa watu jukwaani. Baada ya muda mrefu wa yeye kujaribu kadri ya uwezo wake kupata vigelele na makofi kwa yale yote aliyopanga kusema. Ghafla "Yuko wapi mkandarasi wa kituo hiki cha afya? NATAKA UWE UMEMALIZA KUJENGA KITUO HIKI WIKI IJAYO!!" Ikifuatiwa na mabango ambayo kwa uhalisia yasingefaa kuwekwa hadharani. Baada ya haya yote umati uliotega sikio kwa makini una shangilia na kupiga makofi kwa hatua iliyo chukuliwa.

Haya yote yana ashiria mfano wa mwajiriwa aliye mkosea bosi kwa njia moja au nyingine. Chochote kile kinaweza kusuluhishwa kwa njia ya kistaarabu na kibinafsi zaidi kwaku zingatia kwamba aliye kosea ni binaadamu na mtu mzima pia. Ni vyema kwa wanasiasa kuzingatia kwamba chochote kinachooneshwa kwenye runinga lazima kina angaliwa na watu wengi, ambao wanaweza kuwa mashuhuri sana duniani.

Kashfa na ukali hadharani visiwe njia ya kupata umaarufu kwa wananchi vile vile kashfa na ukali hadharani haviwezi kutumika kupima utawala bora.



 
Kashfa na ukali hadharani visiwe njia ya kupata umaarufu kwa wananchi vile vile kashfa na ukali hadharani haviwezi kutumika kupima utawala bora
Ni viongozi wapumbavu tu wasiojiamini kwenye nafasi walizopewa ndio wanapenda kutumia kashfa hadharani!
 
Back
Top Bottom