"Ustaadhi" amiliki Danguro la watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Ustaadhi" amiliki Danguro la watoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lokissa, Jan 18, 2011.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ustaadhi' amiliki Danguro la watoto Monday, 17 January 2011 10:35 WAKATI asasi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zikiwa katika harakati za kutetea haki za watoto ili kuwaepusha na majanga mbalimbali, jitihada hizo zimeonekana kugonga mwamba kwa kuwa asilimia kubwa ya watoto imejiingiza katika biashara ya ukahaba Temeke.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika danguro lenye wanachama zaidi ya 40 katika nyumba moja iliyopo Tandika inayodaiwa kumilikiwa na 'Ustadhi' (jina tunalo) ambaye pia inasemekana ni mjumbe wa shina (namba ya shina tunalo), umebaini katika nyumba hiyo wamo na watu wazima pia wanaojiuza pamoja na watoto hao.

  Imedaiwa kuwa watoto hao, ambao wako chini ya umri wa miaka 18, wengi wao ni wanafunzi wa shule za msingi na wengine huwa wanazitoroka familia zao kwa ajili ya kujitafutia maisha.

  "Ukimwangalia mtoto mdogo kama huyu, utadhani kuwa hawezi kustahimili vishindo na mikiki tunayokumbana nayo sisi wakubwa, lakini ukimkatalia asifanye kazi hii huwa wanatutukana sana na kudai kuwa sisi siyo wazazi na kwamba wako kikazi kama sisi tulivyo," amesema mama mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuhofia kupoteza wateja.

  Kahaba mwingine katika eneo hilo amesema licha ya changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa watoto hao, pia wamekuwa wakimlipa mmiliki wa nyumba hiyo kiasi cha sh. 3,000 hadi 5,000 kwa siku kwa kila kizimba ambacho kitanda cha futi tatu kwa sita kinaingia.

  "Kitanda cha (futi) tatu kwa sita, ukichoma ndani dakika moja unahudumiwa kwa kiasi cha sh. 2, 000 hadi sh. 3,000 na baada ya kazi kila siku huwa tunalipia sh. 3,000 hadi 5,000 kwa kizimba, hiyo ni sawa na sh. 90,000 hadi sh. 150,000 kwa mwezi na kama unaona tunafanya kazi mbaya unadhani tutaishi vipi hapa!" amehoji kahaba huyo.

  Baadhi ya watoto hao walipohojiwa na gazeti hili wamedai kuwa wao siyo watoto kama wanavyofikiriwa.

  "Ninaweza kumridhisha mteja wangu kama hawa watu wazima, kama ni shule sisomi na hapa sikuja kufanya biashara, nimekuja kuishi kama wanavyoishi wengine. Hivyo kama na wewe unataka huduma ingia ndani," amesema mtoto huyo ambaye jina lake tunalo.

  Hata hivyo, kiongozi wa makahaba hao aliyejitambulisha kwa jina Marieta Ally, maarufu kwa jina la Mchicha Mboga ya Haraka, amekiri kuwapo kwa biashara hiyo na jambo linalowakera ni kuwpao kwa watoto hao wadogo katika eneo hilo na hivyo anaiomba Serikali na mashirika mengine ya kutetea haki za watoto yaingilie kati suala hilo.

  "Wanatutukana, na nikijaribu kuwaonya wasiendelee na biashara hii wananiona mimi ni mnafiki sana, matusi mengi yanaporomoshwa kwangu hadi ninaona aibu mwenyewe. Hivyo naiomba Serikali iingilie kati kuwaondoa watoto hawa ili kuwaepusha na majanga mbalimbali na ikiwezekana wapelekwe shule," amesema Marieta.

  Hata hivyo, jitihada za kukutana na 'Ustadhi' huyo anayemiliki nyumba hiyo hazikufanikiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa yupo safarini na kurudi kwake haijulikani kwani yupo huko kikazi.

  "Yupo kikazi hivyo jitihada za kumpata labda arudi kutoka safari na hatujuhi hatarudi lini hivyo basi kama unahitaji ufafanuzi wa nyumba hii pita huko nyuma utapata maelezo zaidi," amesema mama mmoja ambaye alikuwa nje ya nyumba hiyo.

  Uchunguzi zaidi umegundua kuwa wakati makahaba hao wanapopata mimba na kujifungua, huwapeleka watoto hao kwa majirani wa eneo hilo kwa ajili ya kuwatunzia kwa gharama ya sh. 1,000 kwa siku.

  wanataka tutengane, wanaona maaskofu kama wauaji,wanadai nchi inaongozwa na maaskofu,je matendo yao ?????
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hii ni kweli kabisa, maustadh miyeyusho wanatutia aibu waislam.
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,117
  Trophy Points: 280
  Hilo jina la Marieta tu, hilo tu nikivutio tosha "Mchicha mboga ya haraka" labda na hivi vitoto vikubwa vyenzetu vinatafuta mchicha, yes it is a shame
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Duhh, habari hizi ni za kusikitisha zikihusisha kibwagizo "Ustadh" lakini cha kushangaza ni kuwa hakzikusema ni "Ustadh" wa madrasa au shule ipi? Au hajui maana ya "Ustadh"?

  Inawezekana ni "Ustadh" john wa kuuza wadada? Vyovyote iwavyo, itafikia kiwango cha ukahaba wa vitoto na vidada poa unaofanyika kwa kiwango cha ki-mataifa cha ufuska wa pale Mbowe? Aka Bilicanas?
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Matumizi ya neno USTADH,was it necessary??shida hapa ni kuwaaibisha waislamu kwa sababu ya mtu mmoja au ni kutoa ujumbe kuwa kuna danguro liko sehemu fulani serikali au wananchi wachukue hatua???naona hapa ni kutafutana ubaya bila sababu ya msingi na kuzidisha chuki.
  Sidhani kama umeileta hii thread ili hao watoto wadogo wasaidike bali kuleta mjadala wa udini...........:ban:
   
 7. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #7
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  CRAP, kafanye upuuzi wako pale uone utakachofanyiwa.
   
 8. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ustaadh mwenyewe ndio yupi sasa kati ya hawa?.,au hii picha ina uhusiano gani na hii thread
   
 9. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndo marketing ya Bongo, nasema hivo kwa sababu hata mimi nilivutika nikanunua gazeti la dar leo baada ya kuona heading kubwa front page
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kabla sijasilimu nilikuwa naenda pale kuopoa!
   
 11. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Ustaadhi isichukuliwe ndo uislam, ni mtu tu kama walei kanisani au wallimu wa dini kanisani
   
 12. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haina mshiko, eti ustadh halafu mjumbe wa shina, halafu tumeshindwa kumpata kuzungumza nae. mwisho wa siku mtu akitwa John utasikia padri fulani kwa kuwa kaitwa John. gazeti hili limekuwa la udaku
   
 13. father

  father Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Upupu mtupu, habari nzima haina maana kwa kuwa haionyeshi ustadhi anahusikaje
   
Loading...