Ussi Salum Pondeza - Tukiimarisha Suma JKT na Kiwanda cha Nyumbu wataweza kutengeneza ajira rasmi na zisizo rasmi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939

MBUNGE USSI PONDEZA - TUKIIMARISHA SUMA JKT & KIWANDA CHA NYUMBU WATAWEZA KUTENGENEZA AJIRA

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Mhe. Ussi Salum Pondeza akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliyosomwa na Waziri Mhe. Innocent Bashungwa bungeni jijini Dodoma amesema "Tukiimarisha Suma JKT na Kiwanda cha Nyumbu wataweza kutengeneza ajira rasmi na zisizo rasmi"

"Jeshi lina hospitali ya Bububu kule Zanzibar, ni hospitali kubwa na maalum pia kwa viongozi wakubwa lakini ina hali mbaya, inahitaji ukarabati mkubwa pamoja na vifaa tiba. Ukiangalia hadhi ya hospitali hii ya jeshi na jeshi lenyewe haviko sawa" - Mhe. Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni

"Zile fursa za majengo na vyeo jeshini zitoke kwa uwiano na kwa wakati, kuna maafisa ambao ni wa JWTZ ambao wamechukuliwa kufanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaonekana wanasahaulika wakati wa kupanda vyeo, tuwaangalie kwa jeshi letu linafanya kazi pande zote" - Mhe. Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni

"Suma JKT wanafanya kazi moja nzuri na kubwa sana katika nchi yetu, hata Ikulu yetu ya Chamwino imejengwa chini ya usimamizi wa JKT lakini bajeti na fedha ambazo wanaomba hawapewi kwa wakati. Tukiimarisha Suma JKT na Kiwanda cha Nyumbu wataweza kutengeneza ajira rasmi na zisizo rasmi" - Mhe. Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni

"Suma JKT wanafanya kazi moja nzuri na kubwa sana katika nchi yetu, hata Ikulu yetu ya Chamwino imejengwa chini ya usimamizi wa JKT lakini bajeti na fedha ambazo wanaomba hawapewi kwa wakati. Tukiimarisha Suma JKT na Kiwanda cha Nyumbu wataweza kutengeneza ajira rasmi na zisizo rasmi" - Mhe. Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni

"Kiwanda chetu cha Nyumbu kinafanya mambo mengi mazuri, licha ya kufanya mambo hayo yote bado hakipelekewi fedha kwa wakati, lakini pia serikali haitoi fedha kukiimarisha kiwanda chetu cha Nyumbu" - Mhe. Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni

"Swala la mipaka kati ya maeneo ya jeshi na wananchi bado ni tatizo, na sio kwamba wananchi hawalipendi jeshi, hapana jeshi wanalipenda na ni jeshi lao. Tatizo linakuja kwamba, kambi nyingi za jeshi maeneo yao hayana hati ingawa katika maeneo ya wananchi wapo ambao wana hati" - Mhe. Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni

"Nashauri zile nafasi za ajira za jeshi uziangalie (Waziri wa Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) kama ambavyo namna jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linavyoendeshwa, Waziri unaposema na kile kinachofanyika hakuna uhalisia, nayasema haya nikiwa na ushahidi" - Mhe. Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni
Fw5hiXQWwAUVu8W.jpg
Fw5hxdyX0AQO4EX.jpg
Fw5iFoFWYAgbdz-.jpg
 
Back
Top Bottom