njiwamanga
Member
- Oct 21, 2010
- 35
- 3
sifa za kugombea uspika wa tanzania ni zipi?
.....awe mbuge na amependekezwa na chama chake au awe ni mtu yoyote mwenye sifa za ubunge anaweza kupendekezwa na chama na baadae majina kupigiwa kura bungen.......kama ni jina moja tu ndio lililopendekezwa basi tutampa directly kuwa spika..........."mtu yoyote mwenye sifa za ubunge "nadhan utakuwa unaelewa maana yakeangalia katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ibara ya 86
Hiyo ibara inazumgumzia utaratibu wa kumchagua spika na sio sifa za spika .angalia katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ibara ya 86
86.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha
kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikao
cha kwanza chochote mara baada ya kutokea nafasi katika kiti
cha Spika.
(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu wa Spika wakati wo wote
katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya utakaoteuliwa na
Bunge na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge mara
baada ya kutokea nafasi katika kiti cha Naibu wa Spika.
(3) Uchaguzi wa Spika, na vile vile uchaguzi wa Naibu wa
Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
84.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na
Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au
wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge
na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje
ya Bunge.
(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina
nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa
madhumuni ya ibdara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.
(9) Mtu yeyote ambaye si Mbunge atakayechaguliwa kuwa
Spika, atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake,
kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu.