Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,205
- 33,222
Aah,, sasa unaharibu, unaharibu bana...Mjadala umeibuka nchini baada ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la JMT iliyoachwa wazi baada ya Ndugai kujiuzulu. Hoja bishaniwa imekuwa ni iwapo Dk. Tulia ana sifa au la za kugombea nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge (Na. 3 ya 1988) hususani kifungu cha 41 (1&2), Dk. Tulia kwa sasa ni Kaimu Spika wa Bunge mpaka pale kiti cha Spika kitakapojazwa. Ibara ya 84 (2) ya Katiba ya JMT inaeleza kuwa mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yaliyotajwa na Sheria ya Bunge, hana sifa za kugombea uspika.
Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge inamtaja Dk. Tulia kwa sasa kuwa ni Kaimu Spika, hii ni ofisi/madaraka na imetajwa na Sheria ya Bunge. Dk. Tulia hana sifa za kugombea uspika, asijidanganye kuwa Ibara ya 84 (2) haijamtaja, asome Sheria namba ya 1988 aone kuwa kwa cheo chake cha Kaimu Spika amezuiwa kugombea uSpika. HANA SIFA
View attachment 2079266
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app