Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Sep 15, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,617
  Trophy Points: 280
  Katika pita pita zangu mchana wa leo jiji Dar es Salaam,

  Nimekutana na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila katika ofisi fulani, yeye kaja na yake, nami na yangu hivyo tukaa waiting room pamoja kumsubiria mwenyeji wetu.

  Kwanza kwa ule uafrika wa kawaida mtu ukifika mahali na ukakuta watu, its normal kuwasalimia ndipo unakaa!, Mchungaji Mtikila aliingia tuu na kukaa huku tunaangaliana!, hata bari hakuna!. Kwa vile yeye ni public figure, nikamsalimia kwa jina lake, huwezi amini alinichangamkia sana na tukaanza kuchat.

  Kwanza nilimuuliza kwa nini wapinzani hawaungani?.
  Jamaa alishusha nondo nzito kwa kubonda wapinzani wote kuwa Tanzania, hakuna mpinzani yoyote isipokuwa ni yeye tuu!, tena kuhusu Chadema, ndio usiseme kabisa, eti ni afadhali ya CCM!. Alisema mengi kwa lugha kali na matukano kibao, huku akizungumza kwa sauti ya juu, ofisini kwa watu!.

  Nikamsisitizia, kwa vile chama tawala ni CCM, vingine vyote ni upinzani, jee haoni kuikandia Chadema na CUF at this time ya kuelekea uchaguzi mkuu ni kuikampenia CCM kwa mlango wa nyuma?, au ameshikishwa kidogo dogo?!.

  Jamaa aliwaka sana akasema CCM imshikishe nani pesa, hapa nilipo, japo sina pesa ila nimekataa hongo ya milioni 100! toka kwa ....(akamtaja jina....) naomba nilihifadhi ili kuilinda hadhi ya JF, maana huyu mtu kwa JF, ni "mtakatifu fulani" sana humu jf, na ni mmoja wa waheshimiwa wetu kitaifa, hivyo anaheshimiwa sana tuu humu jf!

  "Niligundua kuwa ... (akamtaja) ni muuaji, anatoa pesa kutuma assasins kutekeleza mauaji mbali mbali na kisha kufake accidents!, alitoa shilingi milioni 120 kuwapa Wakenya fulani wawili kumuua ...(akamtaja..), ushahidi ninao!.

  Mtikila akaendelea kudai kuwa, Mfanyabiashara huyo tajiri alipomgundua siri yake ya mauaji imefichuka, kwanza alimuita kwenye(Mtikila) kwenye moja ya vitega uchumi vyake (akataja siku, muda na mahali) akampa offer ya hongo ya Sh. Millioni 10 ili afute jina lake kwenye dossier ya wauaji. Mtikila akamkatalia.( Akimaanisha analo andiko hilo la mauaji!).

  Mara ya pili (tajiri) huyo alimuita ofisini kwake, (akataja siku, muda na osisi ilipo!) akapanda dau toka ile milioni 10! mpaka milioni 50!, bado Mtikila alizikataa!. Ndipo tajiri huyo akamuita Mtikila nyumbani kwake (akataja siku, muda na eneo nyumba ilipo!) akampa offer ya Sh. Millioni 100!. Ndipo Mtikila alimkubalia kwa shurti ya tajiri huyo, kwanza ampigie magoti yeye Mtikila na akiri dhambi zake, na pili atubu kwa Mungu, Mungu akishamsamehe ndipo yeye Mtikila, ataipokea hiyo pesa kama asante yake!.
  .
  Tajiri akagoma kukiri na akagoma kutubu!. Ndipo Mtikila akasimama akatoka nje!, ila anadai kila kitu amerekodi kwenye digital sound recorder yake, na sasa anasubiri tuu time muafaka ili amlipue!.

  Ila pia Mtikila alikiri kupokea kitita cha fedha, milioni kadhaa kutoka kwa Rostam Aziz, akisema ni kweli nilikuwa na shida, nikaenda kukopa, ila nilipozipata fedha za kulipa, nilimpelekea ili nilipe, akakataa kuzipokea, hivyo deni ameshalipa sasa zimegeuka sadaka.

  Nikamuuliza yeye kama mtu wa Mungu, anajua wazi ufisadi wa Rostam, anakwendaje kwake kukopa, hivi hizo sio sehemu ya pesa chafu za Kagoda?. Alijibu kuwa pesa hata ziwe chafu vipi, zimeibiwa au za madawa ya kulevya, ukizitumia kutenda wema kama basi pesa hizo zinakuwa zimesafishika nna kutakasika, hivyo ni pesa safi kwa sadaka.

  Na baada ya maelezo yote haya ya kukataa hongo ya milioni 100!, Mchungaji Mtikila alimalizia kwa ...(nakihifadhi) ili ndio uthibitisho kuwa he is not normal!.

  My Take.
  Mtikila is insane. Ningekuwa ni mwandishi wa habari, hayo aliyoyasema nikayaandika gazetini na majina yao, kesho yake mimi na gazeti langu tungeishia mahakamani for defamation!.

  Update:
  RIP Mchungaji Christopher Mtikila!.

  Nisamehe kwa yote!.

  Pasco


   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,279
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pasco,

  Huyo ni Mtikila au Tikila (mzee wa saa ya ukombozi ni sasa). Sijui zile volumes zake kwenye tapes zimefikia namba ngapi?

  Jamaa ni kama kinyonga fulani. Kuna wakati anafanya vitu vya maana sana (kama zile kesi zake) ila mara nyingi anachakachua si kawaida. Ipo siku tutajua kama kweli ni ajenti au basi tena ni tatizo la udhaifu wa kibinadamu au njaa.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Pasco nimesoma kwa mshangao post yako hapo juu na kumalizia kwa kuvunjika mbavu
  Dogo MTIKILA amelewa TIKILA
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,617
  Trophy Points: 280
  .
  Ukimsikiliza huku unamuongalia expressions usoni kwake, ndipo utamjua ni insane, anasema mambo makubwa, very sensetive with smilling face. Nlimuuliza kama anao ushahidi kama huo kwanini asiupeleke mbele ya vyombo vya sheria, muuaji ative nguvuni, akadai wahusika wote wa suala hilo ni kabila la muuaji!, hivyo ameona sipoteze muda.

  Amesema leo pia ametoka mahakamani, na anakwenda NEC kumuwekea pingamizi mgombea fulani wa CCM ili kumsaidia mgombea wa Chadema, jimbo fulani.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  he is not insane.... he has given up hope!!
   
 6. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyo Mtikila ni mpiganaji kweli kweli ila ni CHIZI! Pia ni mtu asiyeaminika sana. Miaka ya nyuma nilikuwa namkubali sana huyu kamanda lakini nilipogundua kuwa ni chizi sikumfagilia tena. Pia ana kinyongo na Chadema. Si mnakumbuka kuna wakati alihamia Chadema baadaye wakamtosa walipoona anataka kuwaharibia chama?
   
 7. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Iwapo CHADEMA ndo usiseme iweje afanye haya! kweli chizi
   
 8. E=mcsquared

  E=mcsquared JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,904
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 180
  Mkuu baada ya maongezi nafikiri ukajisikia umekunywa laga ya SAFARI!!
  Maneno yake yanalewesha>
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,617
  Trophy Points: 280
  Leo baada ya kushinda kesi yake, na kugomea kukamatwa, nimemkumbuka, na kuipitia tena hii post, huku nikijiuliza kama nimebadili msimamo kuhusu Mtikila, nimejikuta sijabadili, bali insanity yake very unpredictable, sometimes he works for the better, and sometimes he works for the worse!.
  P.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,022
  Likes Received: 5,191
  Trophy Points: 280
  ulivyoiandika, mmmmmmmh kiudakuudaku.... ila si hilo ninalotaka kuuliza,

  hivi assasian amchukue ampaleke kwake then ambembeleze?
  kabisa matikila anataka kutuaminisha hayo?
  kabisa na wewe umetuletea hayo?
  kama ni muuaji angemmaliza bila yoyote kujua...... hapo mtikila kama anataka kujipaisha hivi...

  mmmmmh  kwenye hili sina la kusema, mwenye masikio asikie, mwenye macho atazame...   
 12. Salathiel m.

  Salathiel m. JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mi naona MTIKILA NI BORA KULIKO MAFISADI MNAOWAONA WANAAKILI TIMAMU, kuna mambo mengi mazur aliyoyafanya ila kuna watu wanaonekana not insane lakin wapuuzi tu!
   
 13. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 9,853
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  kwa kupokea hela za rostam,chochote atakachosema au kufanya hawezi kuitwa mpambanaji tena...mtikila is done,game over..kama nakumbuka vizuri rostam alitokeza kwenye vyombo vya habari na kusema anamdai mtikila pesa zake,..it's just the matter of time kumsikia akisema pesa alizompa zitto(kama tuhuma ni za kweli),.but this is hard sababu rostam alimlipua mtikila kipindi ambacho alikuwa anamsema rostam kwa ufisadi kila mara lakini sikumbuki lini zitto kamtaja rostam ni fisadi kwa jina zaidi ya generalization,.sikumbuki
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,487
  Likes Received: 1,851
  Trophy Points: 280
  ungemuuliza kwa nini siku hizi haiti wahindi g.a.b.a.c.h.o.l.i?kisa walimlipia deni mkopo NBC la nyumba yake mikocheni
   
 15. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,803
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Huyo babu ni mtambo mi nawaambieni, shauri yenu mkimfatilia-haeleweki sana. Yesu kidogo, rushwa kidogo, uongo kidogo mh! Ni vuguvugu kwa kwenda mbele-sio jana, leo wala kesho-mwangalieni tu.
   
 16. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pasco huwa simwamini huwa ana mambo mengi sana ya kupika, kwa post hiyo keshafanya kazi kubwa sana wenye akili tumeiona
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu Johnsecond, tena hapo nimehifadhi majina, na nimemsetiri Mtikila, ningesema mpaka kilichofuatia baada ya mazungumzo yale, ingekuwa ni aibu!. Mtu mwenye akili timamu, ukimuona binadamu mwingine, anafanya jambo la aibu, ukimjua ni insane, unawajibiki kumsetiri aibu yake!.
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,666
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sijui lile dili lake na Rwakatare kummaliza Kakobe limeishia wapi.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu Salathiel.M, hapa nakubaliana na wewe, ni heri insane anayefanya jambo la maana kwa vitendo, kama kutafuta demokrasia mahakamani na kustahili kuitwa "Shujaa wa Demokrasia!" kuliko wanajojifanya kupigania demokrasia kwa maneno matupu na vitendo sifuri, wakiisubiria huruma ya Watanzania kwenye sanduku la kura!.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nyabhingi, by the time RA anatoa hela, hakujua ana deal na mtu wa aina gani!. Huwezi amini, huyo mfanya biashara ambaye Mtikila anadai ni "muuaji", ndiye huyo huyo aliyeigharimia ile kesi yake ya mgombea binafsi!, ndiye huyo huyo aliyemgharimia Mtikila kushiriki uchaguzi mdogo wa Tarime!, lakini leo ndio amegeuka "muuaji!". The man is insane!.
   
Loading...