Uso kwa uso na KARIM AHMED, Tapeli la mtandao la kimataifa kutoka Burkina faso. Chukua tahadhari

Ni vema kama watu wameyajua hayo, kwani hawa jamaa ni wajanja sana na kama mmoja alivyosema wakijua wewe ni mwanaume huyo tapeli anajifanya ni binti tena picha yake utakoma. Big up kwa kupeana taarifa kama hizi. Nimemshangaa sana huyo jamaa anayesema haya ni mambo ya kizamani labda ni wakala wao.
 
Unajua vitu mnavyotahadharisha hapa ni vya kizamani kiasi ambacho mnaonekani nyie ni mambwiga kwelikweli. Fikiria unakutana na rafiki yako leo anakuambia... "Du... nimenunua bonge la radio casset player. Twende nikakuonyeshe"
acha wehu, sasa kama wewe uliyapata zamani hao wa leo wasiojua watajuaje?
ama hujui hiyo zamani uliyoipata hii habari ilikuwa pia imesha expire? tumieni busara kujibu watu, bado kuna vizazi vingi ndo vinaanza kutumia mitandao na vinahitaji kuelimishwa sio kuponda,
 
Kwa kawaida natumia email addres mbili. Moja gmail, nyingine ni ymail. Gmail naitumia kila siku lakini ymail naifungua japo mara mbili kwa wiki. Siku chache zilizopita nilikuta barua katika ymail kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa anaitwa Mr KARI AHMED, Mhasibu katika BANK OF AFRICA Tawi la Burkina faso.

Kwa kifupi alikuwa anahitaji mshirika kutoka nje ya nchi yake ambaye atamuingizia dola za Kimarekani mil 30 kutoka katika akaunti ya mtu anayeitwa Mr JOHN KOROVO raia wa Jordan aliyekufa kwa ajali ya ndege na familia yake. Kwa maana hiyo bwana KARIM akawa ananiomba nijifanye mrithi wa wa bwana KOROVO ili nidai kitita hicho cha pesa ili baadae tugawane nusu kwa nusu na kuwa nyaraka muhimu na maelekezo yote atanipa. Nikasema Ok, kwa kuwa tayari nilikuwa na habari kuhusu watu hawa. Akaniambia nitume jina langu, anuani zote hadi mtaa, nikatuma za uongo.

Kwa kutumia anuani zangu akadraft barua na kunitumia ili niweke saini, ilikuwa ni barua ya maombi yangu kwenda benki hiyo. Nikatuma, baada ya muda nikapokea hati ya kiapo kutoka benki hiyo ili kuthibitisha kuwa mimi ni mrithi halali. Nikaijibu, sasa ikaja barua ya kukubaliwa ombi langu ikiwa imesainiwa na kupitishwa na waziri wa fedha wa nchi hiyo. Ikinitaka nitume akaunti yangu yangu ya benki, pamoja na namba ya msimbo ya benki. Nikatuma feki.

Sasa kimbembe kikaanza hapa:
Cheti cha kifo cha bwana KOROVO kikatakiwa kipitie kwa mwanasheria ambaye anatakiwa alipwe dola 5000. Jamaa akaniambia tuchangie nusu kwa nusu ili mchakato ukamilike...nikasema ok, lakini akaunti yangu haina pesa. Lakini naweza kuomba mkopo haraka haraka kwa kuwahonga maafisa wa benki. Kwa hiyo anitumie dola 300 tu za kuhonga maafisa wa benk kutoka katika pesa yake halafu mimi niombe mkopo wa dola 2800 kisha nimtumie. Duh, jamaa akabadilika na kuwa mkali kuliko pilipili, mpaka leo hajatuma tena upuzi wake.

Kuweni makini, wana mbinu nyingi sana.

KUNa mziki fulani wa Bongo Flava, ULISEMA maneno haya; " Aliuza cheni ya dhahabu FEKI kwa hela Feki ngoma ikawa droo"
Tafakari chukua hatua "HAKI ......... gwe gwe" hiyo ndo dawa yao. Umefanya vizuri.

Ila mimi MPAKA leo sijaamini na sijuwi kama nitakuja kuamini, MTU asiyekufahamu wala hujawahi kumuuona akupe pesa, tena nyingi.

Pia huwa naamini siwezi kutapeliwa kwa maneno, MIMI naamini naweza kutapeliwa na watumia nguvu tu, yaaani kunikaba.
 
Asanteni wana jf, hapa nilikuwa najibu email ya dada mmoja anajiita rita ni msudani ila anaishi kwenye kambi ya wakimbizi senegal anadai wazazi wake walishafariki hivyo tuwe business partner ktk kutransfer kiasi cha usd 3 milion alizoachiwa na wazazi wake.kaweka picha yake ni mzuri kwa kweli, lakini tapeli. Shukrani kwa jamii forum.
 
Asanteni wana jf, hapa nilikuwa najibu email ya dada mmoja anajiita rita ni msudani ila anaishi kwenye kambi ya wakimbizi senegal anadai wazazi wake walishafariki hivyo tuwe business partner ktk kutransfer kiasi cha usd 3 milion alizoachiwa na wazazi wake.kaweka picha yake ni mzuri kwa kweli, lakini tapeli. Shukrani kwa jamii forum.

mku usitunyime maraha hayo. Hebu tuwekee picha yake hapa pls pls tupate uhondo na sisi.
 
Back
Top Bottom