Uso kwa uso na KARIM AHMED, Tapeli la mtandao la kimataifa kutoka Burkina faso. Chukua tahadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uso kwa uso na KARIM AHMED, Tapeli la mtandao la kimataifa kutoka Burkina faso. Chukua tahadhari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Nov 24, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa kawaida natumia email addres mbili. Moja gmail, nyingine ni ymail. Gmail naitumia kila siku lakini ymail naifungua japo mara mbili kwa wiki. Siku chache zilizopita nilikuta barua katika ymail kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa anaitwa Mr KARI AHMED, Mhasibu katika BANK OF AFRICA Tawi la Burkina faso.

  Kwa kifupi alikuwa anahitaji mshirika kutoka nje ya nchi yake ambaye atamuingizia dola za Kimarekani mil 30 kutoka katika akaunti ya mtu anayeitwa Mr JOHN KOROVO raia wa Jordan aliyekufa kwa ajali ya ndege na familia yake. Kwa maana hiyo bwana KARIM akawa ananiomba nijifanye mrithi wa wa bwana KOROVO ili nidai kitita hicho cha pesa ili baadae tugawane nusu kwa nusu na kuwa nyaraka muhimu na maelekezo yote atanipa. Nikasema Ok, kwa kuwa tayari nilikuwa na habari kuhusu watu hawa. Akaniambia nitume jina langu, anuani zote hadi mtaa, nikatuma za uongo.

  Kwa kutumia anuani zangu akadraft barua na kunitumia ili niweke saini, ilikuwa ni barua ya maombi yangu kwenda benki hiyo. Nikatuma, baada ya muda nikapokea hati ya kiapo kutoka benki hiyo ili kuthibitisha kuwa mimi ni mrithi halali. Nikaijibu, sasa ikaja barua ya kukubaliwa ombi langu ikiwa imesainiwa na kupitishwa na waziri wa fedha wa nchi hiyo. Ikinitaka nitume akaunti yangu yangu ya benki, pamoja na namba ya msimbo ya benki. Nikatuma feki.

  Sasa kimbembe kikaanza hapa:
  Cheti cha kifo cha bwana KOROVO kikatakiwa kipitie kwa mwanasheria ambaye anatakiwa alipwe dola 5000. Jamaa akaniambia tuchangie nusu kwa nusu ili mchakato ukamilike...nikasema ok, lakini akaunti yangu haina pesa. Lakini naweza kuomba mkopo haraka haraka kwa kuwahonga maafisa wa benki. Kwa hiyo anitumie dola 300 tu za kuhonga maafisa wa benk kutoka katika pesa yake halafu mimi niombe mkopo wa dola 2800 kisha nimtumie. Duh, jamaa akabadilika na kuwa mkali kuliko pilipili, mpaka leo hajatuma tena upuzi wake.

  Kuweni makini, wana mbinu nyingi sana.
   
 2. P

  Percival JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,564
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  haya ya kale mkuu, ukipate hizi e-mail zipeleke spams folder tu.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  poa mkuu we drag tupia spam au trash folder na kama ukiwa gmail we ireply halafu uindike ni spam automatic ina move kwenye spam folder..
   
 4. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kuna mwingine anajiita "Mildred benson" yuko senegal ni punguani kweli mm alinijia na style ya kuhamisha fedha za urithi 4.7million$ dollar alizoachiwa na baba yake!nlipombana akasepa!
   
 5. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ilinistua! Nusu nizeeke ghafla.
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mimi pia nilishaamua kucheza huu mchezo na mama mmoja aliyejiita sister Mary!Aliniambia anaumwa Cancer na amebakiza kama miezi minne tu ya kuishi,kwa hiyo anahitaji mtu atakayemwamwini amuachie fedha zake!!
  Mary aliniandikia kwamba angependa pesa zake zitumike kujenga shule,kanisa,na kusaidia yatima!!Nikamjibu kuwa mie niko tayari,akaniambia hapo alipo,yupo na baadhi ya ndugu za mume(marehemu),na wanataka kunyang'anya kwa hiyo atamuambia lawyer wake awasiliane na mimi!
  Nikaanza kupigiwa simu na mtu toka South Africa,kuhusu hii issue!!Eti natakiwa kumtumia jina langu in full,nikamtumia!Akanitumia karatasi ya kujaza nikatoa details za uongo,nikafax!Nikapigiwa tena kwamba hatua iliyopo ni ya kwenda kupewa hela Dubai,ila kuna Usd 5000 natakiwa kulipia!!Nikamwambia kwa sababu hizo fedha nyingi zitakuwa zangu,nimemruhusu huyo Lawyer apewe usd 5000 pia kwa vile Dubai ni mbali kwangu,atumie kiasi cha pesa kubook ticket itakayomleta Nairobi au Dar kwa ajili ya makabidhiano!
  Duh,hakuwahi kunipigia tena,wala Mary aliyekuwa anajiita Sister na kutaja Yesu mara kibao!

  Tunatakiwa kuwa makini,Msitume details za bank kabisa!!
   
 7. K

  Konya JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kweli pesa ndo kila kitu
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Unajua vitu mnavyotahadharisha hapa ni vya kizamani kiasi ambacho mnaonekani nyie ni mambwiga kwelikweli. Fikiria unakutana na rafiki yako leo anakuambia... "Du... nimenunua bonge la radio casset player. Twende nikakuonyeshe"
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ukitaka utajiri wa haraka haraka ndio utakutana na mambo hayo mengi sana.
   
 10. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  haina maana watu wasitahadharishwe, jf kuna wanaojiunga kila siku,na kuna ambao hawafahamu haya!
   
 11. dwight

  dwight JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimeshapokea mails zaidi ya 100 zenye ujumbe huohuo. Mi mmoja alinisumbua sana,alivoona nimeruka kila kiunzi alichon'tegea akaniaga kwamba amepata business partner mwingine toka Brazil na walikuwa wako njiani kwenda Indonesia kuanza biashara,baada ya miezi kadhaa aliniomba eti dola 100 kwani ametapeliwa fedha zoto huko Indonesia. Nikampotezea.
  Na wengine hujidai ni wakimbizi walio kambini afu wanakuunganisha na padri ili umsaide ku claim fedha zilizoachwa na baba yake
   
 12. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Me nilichat na mmoja alijifanya yeye ni demu toka russia jina lake ni Rinna, tulichat karibu 6 month, me toka mwanzo nilijua ni katapeli ka kipopo so nikajifanya nimekolea, demu aliniita majina yote ya duniani na peponi, alinisifia kwa kila neno analolijua, mwisho wa siku alijifanya ku arrange safari ya kuja bongo kuniona, so nikamwacha aendelee na porojo dakika ya mwisho akapiga kirungu kwamba pesa yake ya nauli imepungua so nimwongezee kama $3000. Nikamjibu nilikuwa nazo ila nimeshazitumia kumlipia room ktk 5 stars hotel, so ye akope popote aje.
  Toka siku hiyo sijamskia mpaka leo
   
 13. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kwi kwi kwi....mezea basi.....
   
 14. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huyu alishaniandikia sana na mwingine anayejiita Maureen Kayumba. Huwa nawatumia jibu hilo hapo chini. Samahani kwa shehena ya matusi. Huwa na copy na ku-paste na sasa wanajijua vizuri kiasi cha wengine hata kunijibu kwa ufupi kuwa you are a big fool. Hata kimombo hawakimanyi.

  JIBU LA MATAPELI HAO HILO HAPO
  Hey Black macaque.
  You can fool nobody except yourself. **** you and all of your relations. Stop sitting on your arse use your brain.I am a good ****. So welcome plus all of your relations.
  No sane person can buy your archaic stuff.
  Stop duping as you start thinking about working legally.
  Failure to this, you'll be ****ed into your mouth.
  Importantly, send me your father, brothers and mother.
  I promise them a good **** of the year.
  May God curse you and shame on you bloody ****ing thief
   
 15. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sasa kumbe we ndo mbwiga wa mambwiga. We umekutana navyo zamani, mi nimekutana navyo juzi kwa mara ya kwanza. Kwani kuna mtu kakulazimisha uchangie mada?
   
 16. H

  Haika JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kuna swakati unataka burudani pia unaweza kuwasiliana nao kwa muda (ukiwa aware kuwa hutatoa hela wala account number) ni burudani sana, mie huwa nafanya hivyo wakati mwinigine,
  ila kuna wakati nilipata shida mama yangu alipoambiwa email yake imechaguliwa kwenye draw fulani hivyo amepata dola 10000, alichanganyikiwa sana na ilituchukua watoto muda kumfahamisha actually hakuelewa hivyo nikawa nasupervise email wanazotumiana, na kuhakikisha hatumi account number wala $1000 alizotakiwa kwa ajili ya transactions,
  Tulimuambia tu awaambie kuwa yeye hana hela hivyo anaomba wamsaidie kwa kupunguza hela yake ya zawadi kwaajili ya logistics zote, pia watoe na comission ya kumsaidia balance ndio wamtumie.
  Baada ya hapo ikawa kimya.
  Mama hajanisamehe mpaka leo, anajua nimepeperusha bahati yake!
   
 17. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hata mimi nimeshawahi kukutana na hiyo makitu ila mimi hizo email zinaingia moja kwa moja kwenye sparm
   
 18. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Hata mimi huyo MARY aliwah kunitumia e-mail kuhusu hiyo kitu.Wakat nawasiliana nae nilikuwa S.A(BONDENI)nikamtumia contact za TZ,nae akanipa full addres yake ya South Africa.nilipomfuatilia ktk ofc yake nikajibiwa Huyo mtu alikufa toka mwaka 1995
   
 19. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #19
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Halafu walivyo washenzi. Wanaweka picha za wanawake bomba ile mbaya! Ukiwa mgonjwa wa mambo hayo. Lazima uingie kingi bila kupenda.
   
 20. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #20
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Kuna huyu tracy Kumari. Huwa anasumbua sana.

  Nilikuwa na akaunti yangu ya hotmail, nimeamua kuifunga. Yaani kila siku nilikuwa nakutana na email kama hizo.
   
Loading...