Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,154
- 10,809
Mimi kama mkereketwa wa sera za upinzani leo najitokeza hadharani kuhoji hiki kinachoendelea ndani ya CHADEMA.
Kabla ya ujio wa Edward Lowassa, CHADEMA tulitamba sana kwa kutetea wananchi masikini, siku zote tulitetea wamachinga, mama ntilie, wakulima, na wafugaji. Mitaani CHADEMA tulikuwa na mvuto wa kipekee kwa sababu ya hoja na sera zetu za kuifikirisha serikali.Tulikuwa ukivaa magwanda na kupita nayo mtaani unashangiliwa kila kona.
Mara baada ya Edward Lowasa kujiunga chadema, mambo mengi yamebadilika ndani ya chama. CHADEMA ya leo haina mvuto kwa wananchi kabisa, hata ukivaa magwanda na kupita nayo mtaani unaonekana kama lofa fulani tu.
Kwa nini imekuwa hivi?
1.Ni kwa sababu CHADEMA ya leo si mtetezi wa wanyonge tena. Watu maskini wanabomolewa nyumba zao lakini hutasikia wakiwatetea .
CHADEMA ya leo ni rafiki na mtetezi wa wakwepa kodi, wauza madawa, wala rushwa, majangili na wachawi.
2. Imezuka falsafa mpya ndani ya CHADEMA kuwa chama ni watu, kwa hiyo ili mradi tu wewe ni mtu hata kama ni fisadi, mchawi, mkwepa kodi, muuza madawa ya kulevya na mchawi njoo CHADEMA utapokewa.
Je maadili na miiko ya CHADEMA imeenda wapi?
Kutokana na sababu hizo hapo juu nimeamua kutema nyongo kwa Edward Lowassa aturudishie chama chetu, hii siyo CHADEMA tuliyoizoea.
Sent using Jamii Forums mobile app