Usiyoyajua kuhusu Tundu Antipas Mughwai Lissu

MAMBO 11 USIYOYAJUA KUHUSU TUNDU LISSU

1. Je Wajua Tundu Lissu Aliwatoa Gerezani BURE Wananchi 466 Wa Tarime Waliofungwa Kwa Kupinga Mwekezaji Asiwanyanganye Ardhi Yao?

2. Je Wajua Tundu Lissu Alishawai Kupigwa Marufuku Asikanyange Nyamongo Kwasababu Ya Harakati Zake Za Kuwatetea Wananchi Dhidi Ya Wawekezaji?

3. Je Wajua Tundu Lissu Alipambana Na Kaka Yake Alute Lissu Mahakamani Kwenye Kesi Ya Kupinga Ubunge Wa Lema, Alute Akiitetea CCM Na TL CHADEMA?

4. Je Wajua Tundu Lissu Akiwa JKT Itende Alidhaniwa Kuwa "Usalama Wa Taifa" Kutokana Na Tabia Yake Ya KUHOJI Bila Woga?

5. Je Wajua Tundu Lissu Alipambana Na Serikali Ya Mkapa ISIUZE Rufiji Delta Kwa Mwekezaji Nolan, Hadi Bank Ya EIB Ikagoma Kutoa Mkopo Kwa Nolan?

6. Je Wajua Mwaka 2004 Freeman Mbowe Alimuomba Tundu Lissu Ajiunge CHADEMA Baada Ya Kumtetea Chacha Wangwe Kwenye Kesi 10 Za Jinai?

7. Je Wajua Tundu Lissu Alianza Kushtakiwa Kwa "Uchochezi" Mwaka 2001 Na Mpaka Leo Hajawai Kukutwa Na Hatia?

8. Je Wajua Kwenye Kampeni 2010 Kikwete Aliwai Kusema Ni Heri Dr.Slaa Awe Rais Kuliko Tundu Lissu Awe Mbunge?

9. Je Wajua 70% Ya Kesi Anazozisimamia Tundu Lissu Halipwi Chochote Na Watu Anaowatetea, Yeye Hufurahi Akiona Mtu Haonewi Wala Kunyanyaswa?

10. Je Wajua Tundu Lissu Hutumia Mshahara Wake Wa Mbunge Kusafiri Maeneo Mbalimbali Nchini Kuwatetea Walalahoi BURE Mahakamani?

11. Je wajua Tundu Lisu alipigwa risasi 16 hakufa?

C&P

9...........ingeeleweka kama ingesomeka.."Yeye hafurahi akiona mtu anaonewa au kunyanyaswa". Nilifikiri ni kiingereza tu kinatupa shida!
 
sawa ndiyo anaichafua nchi je ni nani/ niwatuwasiojulikana kama unawajuwa hebu wataje maana polisi au mtu yeyote hajawahi kuwaona au kuthibitisha kuwa ni fulani huo ni uhayawani wa lissu tu kuongea asicho kijua hawezi kuongoza nchi
Sijui kama uko sawa upstairs, mimi sijamtuhumu mtu ila nimesema anayefanya matendo hayo ndiye ataichafua nchi yetu kwenye uso wa dunia, labda niongezee kuwa wanaoacha vitendo hivi viendelee kushamiri bila kuvikomesha nao pia wanashiriki kuichafua nchi.
 
MAMBO 11 USIYOYAJUA KUHUSU TUNDU LISSU

1. Je Wajua Tundu Lissu Aliwatoa Gerezani BURE Wananchi 466 Wa Tarime Waliofungwa Kwa Kupinga Mwekezaji Asiwanyanganye Ardhi Yao?

2. Je Wajua Tundu Lissu Alishawai Kupigwa Marufuku Asikanyange Nyamongo Kwasababu Ya Harakati Zake Za Kuwatetea Wananchi Dhidi Ya Wawekezaji?

3. Je Wajua Tundu Lissu Alipambana Na Kaka Yake Alute Lissu Mahakamani Kwenye Kesi Ya Kupinga Ubunge Wa Lema, Alute Akiitetea CCM Na TL CHADEMA?

4. Je Wajua Tundu Lissu Akiwa JKT Itende Alidhaniwa Kuwa "Usalama Wa Taifa" Kutokana Na Tabia Yake Ya KUHOJI Bila Woga?

5. Je Wajua Tundu Lissu Alipambana Na Serikali Ya Mkapa ISIUZE Rufiji Delta Kwa Mwekezaji Nolan, Hadi Bank Ya EIB Ikagoma Kutoa Mkopo Kwa Nolan?

6. Je Wajua Mwaka 2004 Freeman Mbowe Alimuomba Tundu Lissu Ajiunge CHADEMA Baada Ya Kumtetea Chacha Wangwe Kwenye Kesi 10 Za Jinai?

7. Je Wajua Tundu Lissu Alianza Kushtakiwa Kwa "Uchochezi" Mwaka 2001 Na Mpaka Leo Hajawai Kukutwa Na Hatia?

8. Je Wajua Kwenye Kampeni 2010 Kikwete Aliwai Kusema Ni Heri Dr.Slaa Awe Rais Kuliko Tundu Lissu Awe Mbunge?

9. Je Wajua 70% Ya Kesi Anazozisimamia Tundu Lissu Halipwi Chochote Na Watu Anaowatetea, Yeye Hufurahi Akiona Mtu Haonewi Wala Kunyanyaswa?

10. Je Wajua Tundu Lissu Hutumia Mshahara Wake Wa Mbunge Kusafiri Maeneo Mbalimbali Nchini Kuwatetea Walalahoi BURE Mahakamani?

11. Je wajua Tundu Lisu alipigwa risasi 16 hakufa?

C&P
Nimesoma na Tundu Lisu Ilboru, namjua ni mtu mwenye akili sana na hupenda kusoma na pia hupenda na kusimamia haki. Tukiwa ilboru form one kaka yake TL yaani Alute tayari alikua mwanasheria wa serikali Arusha akikaa soweto. You can imagine TL aliweza kumshinda kesi kakake huyo mzoefu wa sheria.
 
Leo asubuhi nimeaka na mawazo kama haya tofauti kidogo nikiwaza ingekuwa mmbunge yoyote wa CDM kavuliwa ubunge kwa situation yake. Tundu Lissu sasa hivi angekuwa keshafungua kesi ya pingamizi.
Niliamini hata mimi wanasheria wa CDM wangefungua pingamizi kuweka pingamizi kama ambavyo angefanya Lisu kama ingetokea kwa mbunge yeyote mwingine wa CCM
 
pamoja na hayo yote lakini hafai kuwa rais wa nchi ambayo haipendi kama tz maana huwezi kuikashfu nchi yako mwenyewe halafu uje uombe ridhaa ya kuiongoza hana sifa ya kuwa rais hata kidogo
Sijawahi kumuona/kumsikia Lisu akiikashifu nchi.Ila nilishawahi kushuhudia akiwakosoa viongozi vihiyo wasijali wananchi wao.

Hivyo nafikiri wewe haujui tofauti ya kuikashifu nchi na kukosoa serikali.
 
sawa ndiyo anaichafua nchi je ni nani/ niwatuwasiojulikana kama unawajuwa hebu wataje maana polisi au mtu yeyote hajawahi kuwaona au kuthibitisha kuwa ni fulani huo ni uhayawani wa lissu tu kuongea asicho kijua hawezi kuongoza nchi
Nani aliyeondoa walinzi area D getini???
 
Back
Top Bottom