Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia

JPM alikuwa na msimamo gani kuhusu UN?

Umesoma kwa utulivu nilichokiandika? Nimeongelea JPM kuwa na misimamo, kwenye mambo yake, hapa tunasifia mtu kutaka kutumia kiswahili, yule alikua anakitumia, alifanya hivyo AU na EAC.
UN hakuwahi hudhuria hadi mauti inamfika.
 
Upuuzi mtupu! Tuna wizara husika, tuna ubalozi UN, kikao Cha UNGA Kiko kwenye calendar ya UN kila mwaka; walishindwaje kufanya maandalizi husika kupata mkalimani?! Wacha kutetea ujinga,

..kuzungumza Kiswahili UN inabidi ulipie.

..kuzungumza Kiingereza UN ni bure.

..pia kuna kitu kinaitwa " working language " ndani ya UN.

..working language maana yake ni lugha ambazo mtumishi wa UN anatakiwa kuzifahamu.

..sasa Kiswahili sio mojawapo ya lugha ambazo mtumishi wa UN anatakiwa kuzifahamu.

..Bahati mbaya Watanzania hatuambiani ukweli kuhusu suala hilo. Tumebakia kudanganyana tu viongozi wetu wanapohutubia kwa Kiswahili ktk mikutano mbalimbali.
 
Wanabodi,

Baada ya Rais Samia kuhutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani kwa kutumia lugha ya Kiingereza safi kilichonyooka, kuna wajinga fulani huku kwenye mitandao ya Kijamii, walimpongeza Rais Samia kwa kuhutubia kwa Kiingereza safi na huku wakimponda mtangulizi wake kuwa alikacha kukanyaga UN kwasababu ya lingua, kitu ambacho sii kweli.

Leo katika pita pita yangu, nikatembelea website ya UN, ndio nikakutana na hii kitu ambayo si wengi nyumbani tuliijua



Kumbe Rais Samia alitaka kuhutubia UN kwa kutumia lugha ya Kiswahili ila hii maana yake ni kuwa, sababu zilizomfanya mtangulizi wa Samia asikanyage UN kuhutubia, sio issues za lingua. Mimi mwenyewe, kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, nimehudhuria vikao vya Baraza Kuu la UN mara kibao nikiwa na Ben na JK, kuna viongozi kibao, wanahutubia UN kwa kutumia lugha zao, kitu kinachofanyika ni kwa ubalozi wa nchi husika hapo UN, kuarifu rasmi Secretariat, na kulipia gharama za mkalimani, Rais wa nchi husika, atahutubia kwa lugha yake, halafu kutakuwa na wakalimani wanne, ambao wataitafasiri hiyo hotuba kwa zile lugha 4 rasmi za UN.

Hivyo hata kama ingekuwa ni kweli, Kiingereza cha kiongozi wa taifa lolote, hakijasimama kuhutubia UN kwa Kiingereza, angeweza kuhutubia kwa lugha nyingine yoyote, hivyo naomba kuwahakikishia wajinga hao, sababu za mtangulizi wa Samia kutohutubia UN, sio lugha.

Pili naomba kuchukua fursa hii kuwatangazia trends za hotuba ijayao ya Rais Samia kwenye 77 UNGA, itatolewa kwa lugha ya Kiswahili. Kitendo hicho, sio tuu kitaipaisha sana lugha ya Kiswahili kimataifa, bali rais Mama Samia, ataacha legacy ya kukipaisha Kiswahili, kukiingiza UN na kukifanya Kiswahili kuwa ni moja ya lugha kuu za dunia.

Hongera sana in advance rais wetu Mama Samia, Chief Hangaya kutaka kuhutubia UN kwa Kiswahili. Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, sasa ndio huu, huwezi kuwa mzalendo, Mkuu wa machifu wa kiasili, halafu uendelee kuhutubia kwa lugha za watu, uzalendo wa kweli ni pamoja na kuuenzi utamaduni wako, na lugha ndio kielelezo cha kwanza cha utamaduni wa jamii.

Kwa sasa Kiswahi tayari ndio lugha ya Afrika, Mama Samia atakipaisha kuwa moja ya lugha kuu za dunia.

2025 Tusifanye Makosa!.

Paskali.

Bado uko hai wewe, kabla ya kupost taarifa yako ipitie kwanza.
 
Haya ndo matatizo ya watanzania! Hawana misimamo zaidi ya kujipendekeza! Nenda ukawanunulie wazee vikombe viwiliviwili vya kahawa!!!, nenda kawanunulie dumu la pombe washiriki uone sifa utakazomwagiwa!
Inasikitisha hata wasomi wetu wamekuwa watu wa kujipendwkeza! Hakuna weledi tena!
Nadhani hili linatokana na mifumo ya ELIMU YETU, haitutengenezi kuwa na CONFIDENCE kwenye maamuzi yetu!
 
Wanabodi,

Hongera sana in advance rais wetu Mama Samia, Chief Hangaya kutaka kuhutubia UN kwa Kiswahili. Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, sasa ndio huu, huwezi kuwa mzalendo, Mkuu wa machifu wa kiasili, halafu uendelee kuhutubia kwa lugha za watu, uzalendo wa kweli ni pamoja na kuuenzi utamaduni wako, na lugha ndio kielelezo cha kwanza cha utamaduni wa jamii.

Paskali.
Ile mida ya hongera hizi ndio imewadia, her this time Mama atahutubia UNGA kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, au tutaendeleza ile kasumba ya mkoloni aliotuachia?.
P
 
Watu wengine mnakaaga wapi, Yaani ufike katika Baraza la UN katika mkutano utumie lugha yako, si ungebaki nyumbani kwako

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mkuu Alvin Slain, wewe mwenzetu umewahi kufika UN kwenye kikao cha Baraza Kuu, ukasikia viongozi wa mataifa wanahutubia kwa lugha gani?. Lugha rasmi za UN ni 6, English, French, Spanish Arabic, Chinese na Russian, je mataifa wasio tumia lugha hizo, jee viongozi wao wanahutubia UNGA kwa lugha gani?

P
 
Nilitaka niseme kitu ila nikakumbuka wewe ni mwanasheria, unamhukumu au kumsifia mtu kwa kukusudia. Hapo nikaishiwa cha kusema.

Lakini kuna Rais yeye hata hakukanyaga UNGA, katuma tu video iliyorekodiwa watu wakasikiliza ukumbini.

Kama Chief alikua na nia na alidhamiria kuhutubia kiswahili na hajatekeleza, tubirie siku akifanikisha hiyo adhma.

JPM alikua na mapungufu yake mengi tu, lakini ikifika jambo la kuonyesha msimamo wake alikua vizuri sana kwenye hilo eneo.

Bila kujali msimamo wake uko hasi au chanya ila alijitahidi kuhakikisha msimamo wake unajulikana bayana.

Binafsi napenda mtu mwenye maamuzi na kusimamia maamuzi yake ( shida yanapokua na matokeo hasi).@The Monk a real man is who stands alone
 
Back
Top Bottom