Usiyoyajua kuhusu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Dkt. Athumani Kihamia alivyovuruga Halmashauri

klaymoo

Member
Oct 3, 2018
7
19
1. Alipokuwa Kaliua kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri aliundiwa Tume na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora baada ya kuvunja mikataba ya ujenzi wa majengo ya ofisi za Halmashauri, nyumba za watumishi, Hospitali ya Wilaya na mabanda ya maonesho ya nanenane chini ya mkandarasi SARAM Contractors na kuisababishia halamshauri kuwa na kesi mahakamani, huu ni ubabe usiokuwa na maana.

2. Aliwahi kupingana na mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Ndugu FRANSIS MSUKA (ambaye pia ni diwani wa kata ya UKUMBI SIGANGA) baada ya kuonekana anafanya matendo yasiyofaa katika zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 katika eneo la Zugimlelo Wilayani Kaliua kwa kukataa kuwaandikisha wananchi akidai kuwa ni wafugaji wanaohamahama.

3. Aliwakata madiwani posho walizokuwa wakilipana kiholela na kusababisha mgogoro hadi serikali ya mkoa ilipoingilia kati na kurekebisha hali hiyo, hata hivyo aligoma kutekeleza. Halmashauri hiyo inaongozwa na CCM kwa asilimia 85 (85%).

4. Alivunja mkataba wa upangaji kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Kaliua bila kibali cha madiwani na kuihamishia ofisi porini kwenye vijumba vya watumishi ili kumkomoa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo, Prof Juma Athumani Kapuya , pamoja na matatizo yote hayo ya kutumia ubabe badala ya utaratibu bado alihamishiwa Jiji la Arusha lililopo chini ya Chadema kama Mkurugenzi wa Jiji.

5. Alipotua tu Arusha bila hata kutulia alikata posho za nauli, vikao na ukaguzi wa miradi kwa waheshimiwa madiwani na posho za motisha na masaa ya ziada kwa maafisa wa ngazi ya juu wa jiji hilo bila hata kutaka ushauri wa kitaalamu kwa watumishi hao, hali hiyo ilisababisha vurugu kubwa sana ikiwemo vikao halali vya madiwani kuvunjika mara kwa mara, na kulikosesha Jiji la Arusha utulivu na wakati mwingine alijificha kuogopa kipigo baada ya kutibua mambo.

6. Alivunja mikataba halali ya upangishaji maduka ya jiji na kuwanyang’anya waliokuwa wakiyamiliki kwa madai kuwa walipewa kinyume cha utaratibu zaidi ya maduka 1000 (elfu moja) lakini cha ajabu akayagawa kwa watu ambao walishindwa kesi mahakamani ambao wengi wao ni makada wa CCM hali hiyo iliikosesha halmashauri ya jiji mapato na wataalamu waliojitokeza kumpinga aliwajengea chuki na kuwahamisha au hata kupoteza kazi zao wakiwemo mwanasheria, afisa maendeleo ya jamii, mhandisi wa ujenzi, mweka hazina, afisa manunuzi na baadhi ya maafisa wa idara zingine.

7. Aliwazuia watumishi hasa wakuu wa idara kusafiri kwa magari ya serikali wakienda safarini kikazi na kuwataka wasafiri kwa mabasi na akaenda mbali zaidi hadi kumzuia hata Meya wake kutumia gari ambayo ilinunuliwa kwa ajili ya Meya na kumtaka afike ofisini pale tu atakapomuita, jambo ambalo Mheshimiwa Mbunge Godbless Lema alililalamikia sana lakini haikusaidia.

8. Alilipa fedha shilingi milioni mia moja na sabini (170) kwa watu kama madeni ya likizo zao bila kibali cha mamlaka yake au madiwani wala TAMISEMI na alipoulizwa alijibu majibu ya kibabe.

9. Alikwenda kuhutubia mkutano wa wananchi Kata ya Ngarenaro na alitumia muda wote wa zaidi ya masaa mawili kumponda diwani wa Kata hiyo Doita Isaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji ya Jiji la Arusha kwa kumtuhumu kuivuruga hamashauri ya Jiji la Arusha.

10. Alivunja uongozi mzima wa kiwanda cha nyama cha Arusha Meat Company kinachomilikiwa na Jiji hilo la Arusha na kusimika uongozi mpya alioteua yeye mwenyewe bila kibali cha mamlaka yake kwa kisingizio kuwa wameshindwa kazi na kuwatuhumu madiwani wawili kuhusika na zabuni kiwandani hapo.

11. Anatuhumiwa kwa kutofuata ushauri wakati wa manunuzi yake mengi jambo ambalo siyo zuri kwenye utawala bora kwa nafasi ya juu kama yake, hii ni pamoja na kukataa kuwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wa kata waliokuwa na makosa ya ubadhirifu wa fedha za wananchi na hata watumishi wa sekta za afya na elimu walipotuhumiwa yeye aliwakalia kimya.

12. Ofisi ya TAMISEMI ilipogundua kwamba Tuhuma dhidi ya Mkurugenzi huyo zimezidi iliundwa Tume mwaka 2017 kuchunguza tuhuma hizo chini ya wakurugenzi kadhaa wa TAMISEMI lakini cha ajabu hadi leo Tume hiyo haijatoa ripoti yoyote na hata sekretarieti ya maadili ya umma haijatoa ripoti wala kuchukua hatua zozote dhidi yake, licha ya kuwasilishwa tuhuma zake kwa nyakati tofauti mara zote ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha zilisimama kidete kumtetea hata kama makosa yake yanaonekana waziwazi ya kuvunja kanuni za kudumu za baraza la madiwani la Jiji la Arusha.

13. Alikuwa mstari wa mbele kuwahimiza baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri, kuwafanyia fujo madiwani na kuwanyima stahiki zao, haswa zile halmashauri zinazoongozwa na upinzani.

14. Hata hivyo mkurugenzi huyo anajua kujieleza vilivyo haswa pale anapokumbwa na tuhuma. Hakika ni Dikteta.
15. Dkt. Kihamia kihalisi ni mtu mpole, msikivu, mwaminifu na anaouwezo mkubwa sana wa kupanga, kuchambua na kusimamia anachokiamini kuondoa ubaguzi wa kisiasa ambalo vyama vya siasa vya upinzani haviamini kwamba anaweza kuvitendea haki.

16. Mkurugenzi huyo hapendi kufanya kazi sehemu iliyotulia, anapenda rabsha nyingi na misuguano ili awe bize na ndio maana Mwenyekiti wa Chadema, Ndugu Freeman Mbowe alimtuhumu kwenye vyombo vya habari na kihamia hakuchelewa kujibu mapigo, hivyo ndivyo alivyotaka vitokee.

17. Dkt. Kihamia ni mpenzi mkubwa na mwanachama wa club ya Yanga, anayeheshimika lakini katika uchaguzi wa mwaka 2016 alipogombea ujumbe walimnyima kwa kuhofia angeenda kuvuruga kamati ya utendaji ya Klub hiyo kutokana na kuwa muumini wa kubana matumizi na kutopenda kushaurika.

AJABU NI KWAMBA
Pamoja na tuhuma zote hizo zinazomkabili za ubabe kwa madiwani, wenyeviti wa mitaa, watumishi wa halmashauri na wanasiasa wakiwemo wa chama tawala CCM, bado inashangaza kuona anateuliwa kwa nafasi ya juu na kupewa rungu kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, jambo ambalo baadhi ya madiwani wa Arusha walitoa maoni kwamba ameenda pale Tume kuua upinzani.

USHAURI
Dkt. Kihamia apunguze ubabe kwa kuwa vyama vyote vina haki sawa ya kutoa maoni kwa Tume, hivyo lazima Tume ionyeshe kuwa ipo huru kwa Vyama vyote.

Dkt. Kihamia aache kufanya kazi kiushindani, kibabe na kidikteta, asikilize ushauri na kufuata Demokrasia ya vyama vingi.
FB_IMG_1538624997411.jpeg
 
Kweli fitna titi la paka, mtu akifanya kazi lazima ashambuliwe. eti sijui kada sijui nini, mbona kuna sehemu kawashughulikia CCM pia? au ukada ni pale tu anapowaumiza wapinzani? kwa hiyo akiwashughulikia CCM hawi upinzani lakini akiwashughulikia wapinzani anakuwa CCM, huyu jamaa anaonekana ni mtu wa kazi na watu kama hawa Tz hawapendwi.
 
View attachment 886088
Hongera Kihamia. Mm ntazungumzia jambo moja tu ninalilijua vizuri: la kuvunja mikataba ya (1) ujenzi na (2) upangaji wa ofisi Kaliua hotelini kwa Kapuya, millennium . Hongera Kihamia.

Iko hivi wakati mama Fatuma Mwasa alipokuwa RC Tabora yeye na mmewe waliunda kampuni la ujenzi... Kisha kwa kutumia nafasi yake kama RC alishnkiza, akapewa karibia tenda zote za ktk halmashauri za Tabora: tenda za ujenzi wa hospitals, ofisi, stendi, mabarabara nk. Akashindwa kukamilisha...hakukuwa na namna isipokuwa kuvunja. Hongera Kihamia.

Kapuya alishnkza kupangisha hoteli yake kwa bei ambayo ni "bei kichaaa", Tsh 400 million kwa mwezi, ndiyo bei aliyotenda. PM Mizengo Pinda akakataa. Mwisho Kapuya akapunguza hadi Tsh 200mil, wakati huo Ded akiwa bwana Ngondu. Kihamia alipokuja, akasema huu ni mkataba wa kinyonyaji, ukavunjwa. Hoteli yenyewe sasa hv n gofu... Hongera Kihamia!
 
"Lakini watu ni watu,
watu si mangodi katu,
beberu angajigamba,
angaruka, angatamba,
ni mtu hana mabawa,
naye hufa bila dawa."
Maneno haya ni utenzi wa mwalimu, J.K. Nyerere yaliyomo kwenye mwongozo wa TANU wa mwaka 1972.
 
Hongera Kihamia. Mm ntazungumzia jambo moja tu ninalilijua vizuri: la kuvunja mikataba ya (1) ujenzi na (2) upangaji wa ofisi Kaliua hotelini kwa Kapuya, millennium . Hongera Kihamia.

Iko hivi wakati mama Fatuma Mwasa alipokuwa RC Tabora yeye na mmewe waliunda kampuni la ujenzi... Kisha kwa kutumia nafasi yake kama RC alishnkiza, akapewa karibia tenda zote za ktk halmashauri za Tabora: tenda za ujenzi wa hospitals, ofisi, stendi, mabarabara nk. Akashindwa kukamilisha...hakukuwa na namna isipokuwa kuvunja. Hongera Kihamia.

Kapuya alishnkza kupangisha hoteli yake kwa bei ambayo ni "bei kichaaa", Tsh 400 million kwa mwezi, ndiyo bei aliyotenda. PM Mizengo Pinda akakataa. Mwisho Kapuya akapunguza hadi Tsh 200mil, wakati huo Ded akiwa bwana Ngondu. Kihamia alipokuja, akasema huu ni mkataba wa kinyonyaji, ukavunjwa. Hoteli yenyewe sasa hv n gofu... Hongera Kihamia!

Hii nimeipenda Big up kutufafanulia, hilo ni moja nina uhakika na mengine yote yana majibu kama haya. Naamini ye sio kichaa na mwandishi hasemi kwa nini alivunja au kufuta jambo, kwanza kwa Mtazamo wangu viongozi kama DR KIHAMIA ndio tunawataka tena ni wachache katika nchii.
DR KIHAMIA songa mbele ukijua mti wenye matunda ndio upigwao mawe SERIKALI ya JPM sio kipofu wala sio kiziwi yangekuwa ya kweli usingeteuliwa kushika wadhifa huo wa UKURUGENZI WA UCHAGUZI (NEC) .Kanyaga Mafuta Twende wakileta shida FYEKA wakileleta shida zaidi FYEKELEA MBALIIIIII
 
Halafu huyo ndio ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi. Wapinzani poleni sana mnapitia kipindi kigumu, sijui 2020 itakuaje
 
Hongera Kihamia. Mm ntazungumzia jambo moja tu ninalilijua vizuri: la kuvunja mikataba ya (1) ujenzi na (2) upangaji wa ofisi Kaliua hotelini kwa Kapuya, millennium . Hongera Kihamia.

Iko hivi wakati mama Fatuma Mwasa alipokuwa RC Tabora yeye na mmewe waliunda kampuni la ujenzi... Kisha kwa kutumia nafasi yake kama RC alishnkiza, akapewa karibia tenda zote za ktk halmashauri za Tabora: tenda za ujenzi wa hospitals, ofisi, stendi, mabarabara nk. Akashindwa kukamilisha...hakukuwa na namna isipokuwa kuvunja. Hongera Kihamia.

Kapuya alishnkza kupangisha hoteli yake kwa bei ambayo ni "bei kichaaa", Tsh 400 million kwa mwezi, ndiyo bei aliyotenda. PM Mizengo Pinda akakataa. Mwisho Kapuya akapunguza hadi Tsh 200mil, wakati huo Ded akiwa bwana Ngondu. Kihamia alipokuja, akasema huu ni mkataba wa kinyonyaji, ukavunjwa. Hoteli yenyewe sasa hv n gofu... Hongera Kihamia!
Kama ni hivyo basi ni mtu mwema na Mungu azidi kumlinda, azidi kumuongoza lakini lile suala la Korogwe CCM kupita bila kupingwa na kwa maelezo ya dharau na jeuri aliyoyaonyesha, Mungu wetu mwema atatoa hukumu ya haki. Hukumu ya haki kama iliyotolewa kwa Ditopile wa Mzuzuri.
 
Kweli fitna titi la paka, mtu akifanya kazi lazima ashambuliwe. eti sijui kada sijui nini, mbona kuna sehemu kawashughulikia CCM pia? au ukada ni pale tu anapowaumiza wapinzani? kwa hiyo akiwashughulikia CCM hawi upinzani lakini akiwashughulikia wapinzani anakuwa CCM, huyu jamaa anaonekana ni mtu wa kazi na watu kama hawa Tz hawapendwi.
Sifa ya ukada ipo namba ngapi mkuu?
 
Sifa ya ukada ipo namba ngapi mkuu?
Tuhuma zinazomuandama hiyo ni moja wapo, ila nauliza mbona kuna sehemu pia kawashughulikia CCM? kwa hiyo huyu jamaa anasura mbili au ni mtu wa kunyoosha mstari bila kujali vyama? na kama ni mtu wa kutenda haki bila upendeleo nongwa ya nini sasa?
 
Back
Top Bottom