Puna
JF-Expert Member
- Oct 9, 2013
- 2,526
- 4,401
Wakuu habarini za jumapili.Kwa wale wanaofahamu basi tukumbushane na wale wasiofahamu basi tuhabarishane.
Kule kwetu Tunduru thamani ya mahindi ni pale yanapokauka na kisha kuyavuna na kuacha maganda machache tu alafu tunahifadhi ghalani na chini ya ghala tunafanya jiko ili ule moshi na joto unayafanya mahindi yasikauke.Yale Mabua na majani mengine mwisho wake ni huko huko shamba huonekana kama uchafu kinachofuata ni moto tu.
Lakini hapa Moshi ni tofauti kabisa huku kila kitu,kuna maghala maalumu ya kuhifadhi mabua kwa ajili ya chakula cha ng'ombe na ni biashara mzuri tu wakati wa kiangazi,ata hivyo Magunzi nayo ni dili ukiwa nayo uwezi lala njaa unaenda migahawani na kufanya biashara kwa hiyo ukiona akina mama wamebebe viloba vya magunzi wapo mitaani wanauza usishangae ni dili ilo.
Lakini ukiangalia maeneo yote yanayolima mahindi utagundua kuwa kitu ambacho hakina thamani kabisa ni zile Nywele lakini kumbe zile nywele zina thamani kubwa katika afya ya mwanadamu kama ifuatavyo:-
Leo tambua kuwa sehemu muhimu zaidi ya mmea huu ni Nywelenywele zake.Hizi nwele zina Alkaloid allantoin na Anodyne (pain-soothing(kutuliza maumivu) ambayo kwa mgonjwa imethibitishwa.Namna ya kuandaa Nywelenywele hukusanywa wakati mmea una mbelewele na kuyaanika kivulini na uyaache yakauke upesi.
UFARANSA:Nywele za mahindi hutumika kuongeza mkojo.
GUINEA,ULAYA NA MAREKANI:Hutumika kwa magonjwa ya njia ya mkojo.
ANGOLA:Kama dawa ya kuongeza mkojo.
ASIA:Kama tiba ya kisukari,oedema na shinikizo la juu la damu.
1.Kisukari:Chukua gram 15 za nywelenwele kavu za mahindi chemsha katika lita 1 ya maji kwa dakika 5.
Kunywa kidogokidogo kwa siku mzima.
NB:Fuata masharti ya milo ya kisukari.Pia changanya mimea mingine ambayo husaidia kupunguza kiwango cha sukari katika damu kama kitunguu maji au green bean(aina ya maharage ambayo inaliwa na maganda yake).
2.Magonjwa ya figo,oedemia,shinikizo la damu,na mawe ya figo:fuata mchanganyiko wa kisukari hapo juu.Unaweza ukanywa chai hii kwa miezi zaidi ya 6 bila kutokea madhara yoyote.
NB:Kwa vile nywelenywele za mahindi mara nyingine hazipatikani unaweza kutumia gunzi badala yake,kwa vile nguvu yake ni ya chini kuliko nywelenywele,tumia gunzi gram 100 badala ya gram 15 za nywelenywele.
Kumbuka Hakuna madhara yanayojulikana,lakini yakitumiwa kwa muda mrefu lazima kuchunguzwa katika kituoa cha afya mara kwa mara,ni muhimu zaidi hasa kwa wenye kisukari na shinikizo la juu la damu.
"MOJA YA MALI ASILI INAYOPOTEA TANZANIA NI PAMOJA NA UJUZI,ULAYA MAKTABA IKIFUNGWA WATU WATAPIGA YOWE HUKU KWETU ZIMEJAA VUMBI HAKUNA WAINGIAJI WA MAKTABA ILA SUBIRI IKOSEKANE SUKARI"