Usiyoyajua kuhusu Daraja la Tanzanite. Kongole Rais Samia!

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Daraja limejengwa mita chache kutoka daraja la zamani la Salenda. Lina Urefu wa takribani Mita 1030, Upana wa Mita 20.3 na Urefu wa Barabara Unganishi yenye KM 5.2 zilizojengwa kwa kiwango cha lami. Daraja limekamilika kwa asilimia 100%.

Tofauti na madaraja mengi ya namna hii barani Afrika, Watumiaji hawatalipa tozo yoyote pindi watumiapo daraja hili (TOLL FREE). Pia, Daraja hili lenye uwezo wa kuhimili tani 180 za uzito litaweza kusafirisha watu wapatao 55,000 kwa siku.

Kwa Takwimu zilizopo, Daraja hili litakuwa kati ya madaraja 10 marefu zaidi barani Afrika likiwa nyuma ya Daraja la Wouri kutoka Cameroon lenye urefu wa takribani Mita 1800 likiwa katika nafasi ya nane kwa urefu Afrika.

Gharama za ujenzi zimetolewa kwa ushirika kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Korea. Ujenzi ulioanza rasmi mwaka 2018 umeigharimu serikali ya Tanzania kiasi cha takribani dola za kimarekani milioni 104.5.

Hadi kufikia mwaka 2017, Takwimu zilionyesha watumiaji wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kufikia kiasi cha magari 42,000 kwa siku. Barabara hii ni kati ya Barabara muhimu kiuchumi lakini pia ni kati ya Barabara zenye foleni, hivyo kukamilika wa Tanzanite Bridge ni mafanikio makubwa kiuchumi.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika mwaka 2021, wakazi wa Jiji la DSM wenye kipato cha TZS 90,000 hupoteza hadi kiasi cha 39% ya mapato yao kutokana na gharama zinazosababishwa na foleni. Daraja la Tanzanite ni kati ya mipango mingi madhubuti ya kukabiliana na foleni ndani ya Jiji.

Mwisho nimpongeze Rais Samia Suluhu kwa kutekeleza ahadi ya kuhakikisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Magufuli inatekelezwa. Mh. Rais anazidi kuonyesha umahiri mkubwa katika uongozi wake. Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele tumebarikiwa kuwa na viongozi makini.

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
 
Wa Kigamboni wanalipia, Matajiri wa Masaki Bure
20220201_194351.jpg
 
Yeye anamalizia ya jpm yakwake mingapi ameanzisha?
Kwa vile hana vision inafaa anga'ang'ane na ile ya jpm japo akitoka 2025 aache sifa ya kukamilisha miradi ya jpm.
Mengine tunaona tu akimcritic jpm kwa vitendo. Bado tu kuruhusu ushoga😂.. maana mabeberu ndio anawahusudu sana.
 
Akafie mbali, ameligawa Taifa vipande vipande. Na katuachia umaskini kwa kukopa hela nyingi na kujenga kiwanja cha ndege chato na kununua ndege zisizo zalisha. Ametuachia majanga.
Dah...!
Nyange, punguza munkar.
Marehemu hafi. Huyo ameshafunga kitabu chake, kumshambulia hakubadili chochote...wewe pambana tu na hali yako.
Btw, JPM wengi wanamkumbuka sana awamu hii.
 
Hata wewe umekosea inaitwa Sealander, wabongo wakaona waiite salenda
Daraja linaitwa Selander na lilijengwa mwaka 1929 wakati wa Ukoloni na liliitwa hivyo kwa heshima ya kumuenzi jamaa Mzungu wakati wa Tanganyika aliekuwa anaitwa John Einar Selander aliekuwa Mkurugenzi wa kwanza mambo ya Ujenzi (Tanganyika's first Director of Public Works)
 
Back
Top Bottom