Usiweke Pesa nyingi kwenye A/C yako ya akiba ya simu ya mkononi si salama hata kidogo.

Pamoja na kasoro hizi, tulio wengi tumenufaika na njia hii ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao. hasa M- pesa, inafika mahali ambapo benki haipo na wala haitaa iwepo!
 
Nimekwapuliwa visenti vyangu kwenye line yangu ya tigo, bora tuvirudie vibubu vyetu jamani
 
kwa kweli af na haya mabank kama
hili la kwangu la exim ***** kila mara network inakuwa down
unaharaka zako unasimamishwa weee,af hata viti vya kupumzikia hawaweki
Pamoja na kasoro hizi, tulio wengi tumenufaika na njia hii ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao. hasa M- pesa, inafika mahali ambapo benki haipo na wala haitaa iwepo!
 
tigo si salama msiweke pesa nyingi kabisa nimeshuhudia watu kila siku kilio icho mimi ni wakala ila inaniuma sana kwa tigo kulifumbia macho suala hili voda waliweza dhibiti kinachotokea ni kuwaweka hawa wanaowaita freelencer wanao renew line za tigo ndo wanaofanya mchezo huo mchafu kurenew line za wateja bila kufuata taratibu.
Ushauri wangu kwa tigo wafuteni hao freelencer wanao tembea mitaani ku renew line

Wajameni kwani ile Akaunti ya Mtandao, ninavyojua kuna "Password" kwani hata ukiFLASH line lazima itahitaji pswd kuingia katika akaunti ile.

Sasa hao Freelancers wanachukuaje hizo fueza wajameni!!!!!!

Naomba mtufumbue macho nasi tuweze kujua.




MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
hivi hawa watu wamitandao
hawajui kuhusiana na hili ama wanaamua kukaa kimya tu? Tigo ndio hakufai
kabisa watapoteza wateja wengi wasipo kua makini!.

Hivi TCRA wana kazi gani?
 
Back
Top Bottom