Usiweke Pesa nyingi kwenye A/C yako ya akiba ya simu ya mkononi si salama hata kidogo.

Kweli hata miye nimeshastuka, nimesikia Wastara JUma amelia kuwa ameibiwa, pia baadhi ya watu kama wanne hivi nimeowaona kwa macho yangu wakilalamika kuwa wamepigwa fedha zao. Wizi huu lazima utakuwa wanacheza watu wenye mitandao na mbaya zaidi tigo ndiyo inayooongoza, je kuna usalama katika kampuni hiyo?
 
Nafikiri hata zile hela za michango kwa ajili ya yule muigizaji zimepotea katika mazingira kama haya.
 
tigo si salama msiweke pesa nyingi kabisa nimeshuhudia watu kila siku kilio icho mimi ni wakala ila inaniuma sana kwa tigo kulifumbia macho suala hili voda waliweza dhibiti kinachotokea ni kuwaweka hawa wanaowaita freelencer wanao renew line za tigo ndo wanaofanya mchezo huo mchafu kurenew line za wateja bila kufuata taratibu.
Ushauri wangu kwa tigo wafuteni hao freelencer wanao tembea mitaani ku renew line
 
nlishuhudia mama mmoja analia kaibiwa elf 25 wanakomba kilichopo bila huruma
 
What? Jamani mtanifanya leo nisilale kwan kunajembe nimem2mia pesa toka sa9 lkn mpaka haijamfikia na kwenye salio langu hakuna pesa! Nimejalibu kupiga voda wananiambia niende kesho ofisini kwao!! Ee mungu nisaidie mbona nitaumbuka mie!!
 
Kizazi cha nyoka hiki, magamba wametulithisha kitu kibaya sana....
 
Na hivi sheria zipo silence katika hilo, hawa watu watatuliza sana coz naamini wafanyakazi ndo washirika wakubwa kabisa!!
 
Poleni walioibiwa kwa njia hii, bahati nzuri sana sina hata akaunti ya mtandao wa Simu.
 
Hilo ni wazo zuri sana, fikiria simu ikiibiwa, au network ikikatika na wewe ulitaka kutuma hela sehemu fulani, huwezi kabisa, mpaka umpate wakala ni muda mrefu, na usumbufu kibao
 
hivi hawa watu wamitandao hawajui kuhusiana na hili ama wanaamua kukaa kimya tu? Tigo ndio hakufai kabisa watapoteza wateja wengi wasipo kua makini!.
 
wATANZANIA tujifunze matumizi ya m-pesa na tigo pesa.hii njia si ya ku-deposit na kutulia ni njia ya kurahisisha usafirisha ji wa pesa hizi ni sawa to western union money.lakini leo tumebadilisha na kufanya account za kuhifadhi.tutalia sana kwa kuibiwa just safirisha pesa na pokea pesa full stop
 
Back
Top Bottom