Usiwaamini sana Polisi hasa wakiwa doria usiku, baadhi yao "si wote" ni majambazi

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Ukikutana na kundi la askari usiku na pengine wakakukagua na wakagundua unavyo vitu vya thamani ikiwa ni pamoja na kiwango kikubwa cha pesa na wakakuacha uendelee na safari yako nakuonya usije kujiamini tena!


Fanya yafuatayo kwa usalama wako;

Wasiliana na ndugu zako kwa sauti ukiwa na askari hao na uwajuze eneo ulilopo na upo na askari Polisi wanakukagua.


Ndani ya muda mfupi jitahidi kuwafahamu baadhi yao kwa majina yaliyopo katika sharti zao na ukiwa unawasiliana na nduguzo uwatajie na hayo majina na wao wakisikia


Usiwe mkweli kwao kwa kuwatajia uelekeo wako sahihi


Baada tu ya wewe kuondoka eneo walilopo kama una gari yako au usafiri wako binafsi tafuta eneo la kuuhifadhi na ondoka kama upo na haraka rejea nyumbani kwa mbinu za kificho na hata huo usafiriyo urejelee siku itayofuata


Usiku mwema!
 
Siku moja nilikuwa napuyanga yale maeneo ya Buguruni kwenye ile chocho inaingia kule nyuma ya msikiti wa pale Sheli.

Jamaa wakanikamata kuwa nazurula usiku, mkubwa wao akawaambia wanichukue, ile tunaelekea kwenye cruiser yao ikabidi nijiongeze, nikamuachia askari aliyenikamata buku 5, jamaa akaniachia nikimbie fastaaaaaa, hiyo ndio ilikuwa pona yangu ya kulala kituoni usiku huo.
 
Nimepanic kivipi? Thibitisha katika reply yangu kuwa kuna sehemu nimeandika ikidhihirisha nimepanic!
Nadhani hujaelewa nilichoandika ndio maana ukabwatuka ulivyobwatuka!
Soma mstari kwa mstari ili uelewe!
Kama haujapanic basi umepandemic...😂😂😂😂
 
Hao watu siwapendi sana,mwaka jana nilinusurika kifo ila MUNGU ni mwaminifu aliniponya....kuna jamaa yuko central mbeya kitengo cha upelelezi jina lake Victor Ngowi huyu namuombea laana imtafune yeye na uzao wake wote. Dont trust the cops
 
Back
Top Bottom