Usivae glovu kujikinga na Korona

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210302_111518_0000.png


Glovu zinazotumika mara moja huvaliwa katika kazi za kitabibu. Glovu hizi hazina ufanisi katika maisha ya kila siku katika kujikinga na Korona.

Usivae glovu katika mazingira ya kawaida kila siku kama vile unapofanya manunuzi.

Kuvaa glovu kunaweza kukufanya ujihisi kuwa upo salama hali ambayo sio sahihi.

Glovu zinaweza kusababisha ukapiga chafya au kukohoa juu yake, hii hutengenezea mazingira ya virusi kuishi

Unaweza kujisambazia virusi mwenyewe wakati wa kuvua glovu au ukagusa uso na glovu zilizo na virusi

Glovu zinaweza kukufanya usioshe mikono yako mara nyingi kadri unavyohitajika

Hivyo haushauriwi kuvaa glovu ili kujikinga na Virusi vya Korona badala yake osha mikono yako mara kwa mara
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom