Usiusemee moyo Wanawake chukueni hili funzo toka kwa dadayenu Jaydee

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Katika nyimbo zote za Jaydee naipenda sana hii ya USIUSEMEE MOYO japo katupiga madongo sana wanaume lakini yani ukweli ndani yake, wanawake mkichukua hili funzo mtaishi kwa amani sana.

Fuatilia hii mistari.

"Umepika chakula huli, huoni chapoa
Umpweke mwenye moyo duni nakupa pole dada
Kula dada kwani huyu haji, ati yuko nawashkajii na akirudi matokeo yake ugomvi hawishii.
Uko aliko mbali na upoeo wa macho yako,
Atafanya baya atakalo bila idhini yako

Uko na rafiki zako mko nyumbani kitako, mnapeana michapo huku mkicheka na vicheko.

Wawapa habari zako jinsi bwana anavyo kutenda hutojua moyo wake kwani ni vigumu kufungua moyoo..."

Usijigambe eti akapenda hujui nini atendalo kwako,
Eti wampenda, katu usiusemee moyo wa mwenzi wako x2

"Mmelala ni usiku sana usiku wa mananee, aliki yake kumbe yamuwaza kimwana mwinginee,

Milio ya simu na ujumbe mfupi vinazidi kwa Sana, ukiuliza bwana kulikoni utaambiwa ni stori,

Nawe moyo wako punde unaanza kwenda mbio, mara siku akuage kwamba anakwenda kutukio,

Muulize kwani hato kujibu mwenzio, mara na siku zingine simu yake iko busy nusu saa."


Ussijigambe eti akapenda hujui nini atendalo kwako,

Eti wampenda, katu usiusemee moyo wa mwenzi wako x2

"Angejali moyo wako asinge kuumiza huyo,
Angeacha atendayo ili wewe upate faraja,
Lakini umuulizapo juu yeye hukujua
Hatojali moyo wako, na wala halijali hilo lako pendo."


Ussijigambe eti akapenda hujui nini atendalo kwako,

Eti wampenda, katu usiusemee moyo wa mwenzi wako x2

HII NDIO THE BEST JAYDEE SIDHANI KAMA ATAWEZA TENA KUTUNGA MISTARI KAMA HII.
 
watakuja, anyway nasikia yule video queen kwenye huo wimbo ni mke wa mtoto wa Dandu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom