usitupe taka hapa...

NG'ADA

Senior Member
Sep 2, 2011
152
15
hizi sehemu zinanishangaza....
sehemu imeandikwa ;
usitupe taka hapa....sehemu hiyo unakuta imejaa taka kibao...
si ruhusa kukojoa mahali hapa....harufu ya mkojo kwa kwenda mbele
usikae hapa, by utawala....watu kibao wamekaa....
na mengineyo mmeona...

haya matangazo yamewekwa juu ya uchafu?...au ni sisi watanzania tunapenda kwenda kinyume?
 
Hospital kumeandikwa usipige kelele ila ukiwakuta hao manesi wanavyopayuka..utachoka!!
 
matangazo mengi wanayaweka sehemu ambayo tayari ilishakua chafu kuonya wakati watu washaazoea kutupa taka hapo...............walitakiwa kuweka sehemu watu hawajatupa taka ili wasitupe au waziondoe zilizoko hapo kuwe kusafi then ndio waweke tangazo so mtu akija na taka ataona hakuana taka pale wala shimo so hatatupa
 
Sasa kuna kibao kinasema ''usitupe taka hapa'' wakati HAKUNA kibao kinginge kinachosema ''TUPA taka hapa''. So, watu wanabwaga pale pale kupeleka messsage kwa wahusika
 
Back
Top Bottom