Usitumie usaliti kama suluhisho

April26

JF-Expert Member
Jul 14, 2020
1,403
2,118
"USITUMIE USALITI KAMA SULUHISHO"

Elewa tabia za kudanganywa na mpenzi wako. Watu hudanganya kwa sababu nyingi na sio kila wakati kuhusu ngono.

Wakati mwingine watu hudanganya (usaliti) kwa sababu wanatafuta uhusiano wa kihisia, kujaribu kukabiliana na hasara au migogoro au kutafuta ku escape zaidi aidha kwa wapenzi wao.

Watu wengi niliyo bahatika kuzungumza nao wenye matatizo ya kusalitiwa ikiwemo na wasaliti pia wamekuwa wakieleza zaidi kuhusu wanachodhani ni kutoridhika au kutoridhishwa na tendo la ndoa (sex)

Kitu ambacho wengi hawajui ni kwamba matatizo mengine yanaweza kujitokeza katika mahusiano ambayo hayahusiani na sex na kuanza kuvuruga akili na hisia za wapenzi na kupelekea hasa zaidi kukosekana kwa mawasiliano na mahusiano mazuri (love and romantic affection) ambapo huweza kwenda moja kwa moja kuathiri hisia (emotions) zao na kupelekea taratibu kutofanya tendo la ndoa kwa kiwango kinachotakiwa, hapo ndipo mapungufu huanza,then ndo maana wengi hudhani na kudai zaidi sex isiyoridhisha ndicho chanzo kumbe hayo ni matokeo tu ya sababu nyingine japo pia inaweza kuwa sababu mojawapo

Usifikiri kuwa udanganyifu wa mwenzako mara zote ni kuhusu ngono tu.Jua na kuelewa kiundani kwa nini anadanganya (kusaliti) kabla ya kuendelea kuamini kuhusu tendo la ndoa pekee kama wengi wanavyodhani.

Jaribu kumuuliza mpenzi wako, mwambie ninahitaji kujua ni kwa nini ulidanganya (usaliti).Tafadhali kuwa waaminifu kwangu na uniambie kilichotokea kufikia kunisaliti.Huenda hakuwa na mawazo kwa undani kuhusu hilo jambo la kusaliti labda sababu yenyewe hawezi kuielezea kinagaubaga,hiki ni kiashiria kuwa amesaliti pasipo kuwa na sababu kubwaa sana,

Hili ndilo tatizo kubwa sana kwa wasaliti wengi hujikuta wanasaliti lakini hawana sababu yenye mashiko au hata kama walifanya bado hawawezi kujua kwa nini. Na kunaweza kuwa na sababu zisizoeleweka kikamilifu, lakini kutambua inaweza kuwa jibu la uaminifu.

Baadhi ya sababu za kawaida za usaliti ni pamoja na:

Kuvutiwa na mtu tofauti:

Hapa wasaliti hushindwa kuwatengeneza wenzi wao na kujikuta wanatamani watu wengine walikwisha pendeza kwa gharama za watu wengine (tamaa) hivo unapokuwa na mwenzi wako mfanye awe unavyopendezwa nae ili kupunguza tamaa.

Kuwa kwenye ndoa au mahusiano yenye matatizo:

Ukiwa na ndoa inayoyumba na kupepea bendera nyekundu na ukaamua kutoka nje ya ndoa au mahusiano yako, hiyo sio suruhisho ya kujenga ndoa au mahusiano bali unazidi kuharibu sana na sana. Kubqa zaidi ni kuhakikisha unaweka sawa mahusiano kwa kutatua migogoro kwa gharama yeyote ili ikiwa wewe unapenda mahusiano yako yadumu.

Mawasiliano (yasiyoeleweka) mabaya:

Mawasiliano yasiyokuwa mazuri huchangia sana usaliti kwa asilimia kubwa sana either mkiwa mnaishi pamoja au kwa umbali fulani, kuwasiliana kunajumuisha kwa njia ya simu, kimwili, kihisia, jinsi ya kupeleka taarifa na kurudisha mrejesho katika ndoa au mahusiano. Hivyo shirikisha mwenzako vike unavojisikia kuhusu mwenendo wa mawasiliano ili myaweke sawa kufikiria malendo yenu. Usaliti sio dawa.

Ugonjwa wa akili kama msongo wa mawazo & sonona:

Hii hali huweza kutokea kwa sababu ya mpenzi wako kuwa na tabia usizopenda au anakuwa anakutendea visivyo, na unaweza kuwa umejaribu kutatua changamoto hizo mwenyewe kufikia kuchoka na kuanza kupata msongo wa mawazo na sonona ambapo huweza kupelekea utendaji wako wa akili kudhoofika na kusababisha hata kutofanya kazi zako vizuri. Then hapa solution sio kuchepuka na kusaliti bali unaweza kuwaona watumishi wa Mungu, wazazi na walezi wenye busara unaowaamini, wataalamu wa saikolojia na afya ya akili kwa ajiri ya kupanuliwa wigo wa mawazo na kubadirisha radha ya kufikiri ili uwe na mwazo chanya na mtazamo mpya dhidi ya chanagamoto kama hizo.

#Note: Kuna sababu nyingi sana za usaliti ambazo mara zote hukosa utetezi kamili kama njia ya suluhisho la mahusiano,bali wengi hudai kubadirisha radha ya mahusiano kwa namna mbalimbali, lakini pia kuna mambo kama; uchafu, wapenzi vuvuzela, wapenzi wababe, wasiojua kutunza bajeti ya matumizi, ulevi wa pombe na uvutaji, ubishi, umbea na unafiki, uvivu na kutojishughuriaha na kazi, matatizo ya kimwili kama magonjwa, tamaa za mali na ngono n.k. Hizo zaweza kuwa sababu nyingine za usaliti lakini dawa ni kupitia mazungumzo tu.

Kumbuka: Sio kila anekusaliti hakupendi, pengine hujapatia namna ya kuishi nae, ukirejea mifano ya sababu zinazopelekea usaliti hapo juu unaweza kuona moja ama zaidi kuhusu mapungufu yanayopelekea usaliti. Pil, Kama una uhakika ndani ya moyo wako kuwa wewe ni mwaminifu kabisa, angalia sana kama unasalitiwa na mpenzi wako, huenda sio bahati yako,unapojaribu kutatua tatizo na ukaona linaendelea ni vema ukaachana nae kuliko wewe pia kuanza usaliti hii ni hatati sana maana huweza kuleta shida kubwa ndani yako.

UHAI NI ZAWADI YAKO PEKE ULIYOPEWA NA MUNGU, UNAPOAMUA KU-SHARE NA MTU LAKINI MTU HUYO AKAAMUA KUCHEZEA ZAWADI HIYO NI VEMA KUMNYANG'ANYA ILI KUJITUNZA MAANA HAKUNA AJUAE THAMANI YA MWINGINE KAMA HAJAPENDA.
 
Baada ya miaka kadhaa pengine (huenda) mawazo yakawa tofauti na haya.

BTW duniani hakuna jipya i.e yalikuwepo~yapo~yatakuwepo
 
Back
Top Bottom